Mwananchi: Aliyemtishia Nape bastola ni miongoni mwa wanaoshikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara Mtwara

Course Coordinator

JF-Expert Member
Jul 27, 2019
1,729
3,198
Dunia inazunguka kwa kasi.

Askari huyu, tarehe 23.3.2017 alimtishia Nape Nnauye bastola asiongee na waandishi wa habari baada ya kutumbuliwa na Rais Magufuli kwa sakata la Makonda kuvamia Clouds FM usiku.

Leo hii ni miongoni mwa maaskari waliokamatwa kwa tuhuma za mauaji mfanyabiashara mkoani Mtwara, Mussa Mussa kijana aliyekuwa anajitafutia maisha yake.

Sirro na Makonda walijua Mtwara ni mkoa wa kusadikika wakimficha mtu wao huko hatajulikana kama ambavyo tuliaminishwa kuwa hafanyi kazi Jeshi la Polisi.

Askari huyu wa Sirro ni ndugu Gilbert Kalanje na anashikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya mfanyabiashara wa madini mkoani Mtwara

Pia soma:

Nape Nnauye atishishiwa Bastola na kusukumizwa kwenye gari


Screenshots_2022-01-28-06-55-40.png

Gazeti la mwananchi la leo tarehe 28.1.202

Wasiojulikana wanaendelea kujulikana.

images (5).jpeg

Askari wa Sirro akiwa na bastola na pingu mwaka 2017.


20220128_054904.jpg

 
Karma haijawahi kumuacha mtu salama
IGP Sirro aliwahi kusema mtu huyo alikimbia na Jeshi la Polisi linaendelea kumtafuta. Amesema kuonekana kwa picha za mtu huyo haina maana kwamba atapatikana kwa urahisi hivyo jeshi hilo linaendelea kumtafuta.

“Mheshimiwa Nape amefungua kesi. Ujue picha kuonekana haina maana kwamba yule mtu ataonekana kirahisi lakini upelelezi unaendelea kumtafuta aliyefanya tukio hilo. Wananchi watusaidie, maana suala la kumpata mhalifu ni ushirikiano, sisi tunaenda kwa taarifa, bila taarifa ya uhakika hatuwezi kufanikiwa,” amesema.

Kumbe baada ya tukio wakampeleka Mtwara halafu akaenda kujiongelesha Mtwara.
 
Yametimia, ukizoea kula nyama ya mtu, huwezi kuwacha, yule askari aliyemtolea waziri Nape Nnauye bastola ni miongoni mwa askari Polisi wa Mtwara wanaokabiliwa na kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini.

Ni wakati muafaka sasa kwa Nape Nnauye kutumia madaraka yake, ili kuifufua na kesi ya kutishiwa kuuawa na hii kima ili kukomesha tabia hizi.

Screenshots_2022-01-28-06-55-40.png
 
Back
Top Bottom