Mwanamke usijichanganye mambo haya hayajawai kumtetemesha mwanaume hata punje

Abby Uladu

JF-Expert Member
Dec 16, 2022
2,106
4,400
Mwanamke usijichanganye mambo haya hayajawai kumtetemesha mwanaume hata punje.

Ndugu yangu Sexless naomba nikurekebishe katika uzi wako uliotaka kuwaingiza mkenge wanawake unaosema..https://www.jamiiforums.com/index.php?posts/48866649

20231221_152235.jpg


Enyi wanawake, mambo haya hayajawai kumuumiza kichwa mwanaume wala usije ukajidanganya utakuja juta maisha yako yote.

Kumbebea ujauzito(mimba) kwa nia ya kumkomoa mwanaume.Hakuna mwanaume atatishika wala kuogopa eti kisa una mimba yake ,kigezo cha kumbebea mwanaume mimba haimfanyi atulie na wewe daima.

Kuolewa ni majaliwa sio kutegesha mimba utachina mapema mama.Kama huna akili utabeba hata mimba kumi na hutaolewa.

Hivi kama mimba ingekuwa ndio kigezo cha kuolewa unafikiri kungekuwa na single mothers wengi.Acha ujinga stuka.

Usifikiri kuishi na mwanaume muda mrefu ndio atakuoa au hawezi kukuacha.Dada yangu acha kujidanganya eti nimeishi nae miaka 4 "pika pakua" hawezi kuniacha ,utaumia.

Wengine wanafika mbali zaidi kusema kwakuwa tumeishi muda mrefu serikali inatutambua kama wana ndoa.Hakuna ndoa ya kuishi muda mrefu pasipo sheikh au padri au mchungaji au kiongozi wa kimila anayetambulika kisheria kuifungusha ndoa hiyo .

Unaweza kuishi na mwanaume hata miaka 10 na akakuacha mataa hutaamini.

Kuwajua ndugu wa mwanaume wako sio tiketi ya kudumu au kuolewa na mwanaume huyo.Dada yangu kumujua mama,Baba,dada,shangazi haikufanyi uolewe kama hupendwi kaa ukijua unajisumbua tu.

Pia tabia ya kupigia wazazi wa mwanaume wako kujifanya una wasalimia ni utovu wa nidhamu subiri uolewe acha kujipa umuhimu kwenye maisha ya wazazi wake.

Nyongeza.

Ukitaka kuishi na mwanaume unatakiwa kumkubali alivyo na umpende ulivyo muda wowote anaweza kubadilika.

Mwanaume akikupenda hapendi usumbufu ata kubadilisha kutoka kuwa wa mpango ukawa chombo cha starehe.

Mwanaume atosheki na mwanamke mmoja.

Abby Uladu
Psychologist and journalist
Mbezi beach finest.
 
Sasa kama mwanaume hampendi na hana mpango naye huyo mwanamke kwann anaganga miaka kibao?? Hapo ndiyo sielewi yaani.

Hupendi halafu unaganda??!! Nini kinamgandisha kama siyo kavutiwa?
Mwanaume huwa anaangalia utulivu mara nyingi.
Hivi kama mwanamke ana utulivu wa maneno,ufanyaji kazi na maono mwanaume ni rahisi Sana kumuoa mwanamke huyo..

Sababu kubwa ya kuishi muda mrefu na bila ndoa ni kutoridhika kimapenzi na mwanamke ,au kumpendea kwa lengo maalumu.
 
Back
Top Bottom