Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,663
- 8,796
Hali ya simanzi imetanda katika kijiji kimoja huko Kapsabet kaunti ya Nandi Nchini Kenya baada ya Mwanajeshi wa Kikosi cha Ulinzi cha Kenya (KDF) kumkata sehemu za siri kisha kumuua Kasisi wa Kanisa la ACK baada ya kumfumania akifanya mapenzi na Mkewe juu ya kitanda cha Mwanajeshi huyo.
Askari huyo alipewa taarifa za siri na Wasamaria wema kuhusu Mkewe ambaye ni Mama Mshirika na pia ni Kiongozi wa Kanisa hilo kuchepuka na Kasisi huyo aliyetambulishwa kwa jina Rev Kime ndipo alipoamua kumvizia nyumbani kwake ambapo alirejea nyumbani kimyakimya usiku bila kumpa taarifa Mkewe na akaingia katika chumba kimoja bila ya Mkewe kujua ili kuthibitisha taarifa hizo.
Baada ya muda kidogo akaingia chumbani kwake na kumfumania Mtumishi huyo wa Mungu mwenye umri wa miaka 43 katika kitanda chake na Mke wake ndipo alipochukua uamuzi wa kumchoma na kitu chenye ncha kali mgongoni na kumkata sehemu zake za siri na kisha Askari huyo akatoweka kusikojulikana na Mkewe ambaye amejeruhiwa hajulikani alipo.
Majirani wameuambia mtandao wa The Star kuwa kabla ya kumuua Mchepuko wa Mkewe, Askari huyo alimfunga Mkewe kwenye kona ya nyumba ili amshuhudie wakati akimuua Mchepuko wake huyo ambapo ripoti zinasema Kasisi huyo alikuwa akisafiri KM 30 hadi kwa Mwanamke huyo na kufanya nae ngono pale Mumewe anapokuwa kwenye kazi zake za ulinzi wa Nchi.
Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Nandi Dickens Njogu amesema “Ilikuwa tu asubuhi ya leo wakati Mkuu wa Kanisa kuu la St. Barnabas Mchungaji Nillah Bassy alipotoa ripoti rasmi ya tukio hilo la kusikitisha sana ambalo Maafisa wa Polisi walikwenda kushuhudia”
Ripoti zimesema baada ya tukio hilo Majirani walimpeleka Mchungaji huyo Rev Kemei katika Hospitali ya Kapsabet Level 5 akiwa katika hali ya umahututi na baadaye alipelekwa Eldoret na kisha akapelekwa Hospitali ya Top Hill ambako alifia akiendelea na matibabu.