Kula la hero huko aliko, uwiiiii uwiiiiMwanafunzi wa Kidato cha Tatu katika Shule ya Sekondari Nyanungu Tarafa ya Ingwe wilayani Tarime mkoani Mara, Charles Chacha (19), amekutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia kamba ya katani.
Diwani wa kata hiyo ya Nyanungu, Mang’enyi Ryoba amesema Chacha alijinyonga Februari 23, mwaka huu usiku, baada ya yeye na wenzake wawili wa kike kupewa barua shuleni siku hiyo ya adhabu ya kutodhudhuria shuleni kwa siku 14.
"Sababu ya kupewa barua hiyo ya adhabu haijafahamika. Tunafutilia kujua tatizo la wanafunzi hao lilikuwa ni nini.Tulitoa taarifa kituo cha Polisi Kegonga na Nyamwaga ambao walifika na kuuchukua mwili wa marehemu huyo,” alisema Diwani Mang’enyi.
Kamanda wa Polisi Tarime/ Rorya, Gemini Mushi alithibitisha kutokea kwa kifo hicho na kueleza kuwa chanzo kinachunguzwa.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Wilaya.
Walimu wawe wanatoa ushauri nasaha baada ya kutoa adhabu
Nahisi hata balehe inachangia kuingia Katika matatizo Kama hayoKwa miaka 19 alipaswa kuwa f6. Adhabu tu imfanye ajinyonge? Kwani walisimamishwa kwa wiki 2 pasipo wazazi kujua? Jamani, watoto wafundishwe na wazazi kumwogopa Mungu. Wanadhani kujiua ni kupumzika kumbe ndipo kulia na kusaga meno kunaanza.
amekwenda kujipeleka mwenyewe kwenye kulia na kusaga meno mwache ameamua kujiwahisha kuzimuKwa miaka 19 alipaswa kuwa f6. Adhabu tu imfanye ajinyonge? Kwani walisimamishwa kwa wiki 2 pasipo wazazi kujua? Jamani, watoto wafundishwe na wazazi kumwogopa Mungu. Wanadhani kujiua ni kupumzika kumbe ndipo kulia na kusaga meno kunaanza.
halafu hiyo kamba tena imemkwida mwingine wa harare ruvuma naye ni mtumzima kajonyongea nayo kisa amechoka kudai hela zake kwa watu wasiotaka kumlipa yaani binadamu wanashangaza sana kweli mtu unaamua kujimaliza kwa vitu ambavyo havina thamani ya uhai wako aiseeInasemekana hiyo kamba aliyojinyongea inahitajika sana kwenye masuala ya Sayansi ya Kiafrika
unashangaa adhabu mkuu yuko mwingine amejikwida kisa kudai hela zake kwa aliowakopesha sasa sijui tunakwenda wapiKujiua tena, kisa adhabu!
Maisha yamebadilika sana, sijui tunaelekea wapi jamani.unashangaa adhabu mkuu yuko mwingine amejikwida kisa kudai hela zake kwa aliowakopesha sasa sijui tunakwenda wapi