Mwanafunzi adaiwa kumuua mwenzake wakibishania umri

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,197
4,474
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha pili (miaka 17) kwa tuhuma za kumuua rafiki yake, John Lema (18) chanzo kikielezwa kuwa, mabishano ya umri.

Mwanafunzi huyo mkazi wa Mtaa wa Kalimani, Wilaya ya Moshi inadaiwa yeye na Lema walikuwa marafiki na siku ya tukio walikaa kijiweni wakivuta sigara, wakaanza kubishana kuhusu umri kwamba nani mkubwa kati yao.

Inadaiwa kuwa, Lema alidai yeye ndiye mkubwa, jambo ambalo halikumfurahisha mwenzake aliyekuwa akidai ndiye mkubwa.

Inadaiwa baada ya mwanafunzi huyo kuona Lema anang’ang’ania ukubwa, aliamua kumshambulia kwa kumkata shingoni na mkononi kwa panga na kusababisha kifo chake.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Septemba 12, 2024, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema tukio hilo lilitokea Jumatatu Septemba 9, mwaka huu, saa nne usiku, katika Mtaa wa Kalimani, eneo la Dampo, Kata ya Kaloleni, Wilaya ya Moshi.

Amesema chanzo cha mauaji hayo ni mabishano ya nani mkubwa kati ya marehemu na mtuhumiwa.

“Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi kwa uchunguzi wa kidaktari,” amesema kamanda huyo.

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kalimani, Ndama Masule amedai kuwa, vijana hao walikuwa wamekaa kijiweni wakivuta sigara, ndipo mabishano ya umri yalipoanzia.

"Waliendelea na mabishano kwa muda mrefu; marehemu (Lema) akamwambia mtuhumiwa mimi ni kaka yako nisalimie, marehemu akasema hawezi kumsalimia shikamoo kwa sababu wangeenda wote sekondari wangekuwa darasa moja," amesema mwenyekiti huyo.

“Marehemu alimwambia mtuhumiwa, angekuwa anasoma kama yeye wangekuwa wote kidato kimoja, hiyo kauli ilimuudhi mwenzake akamshambulia kwa panga.”

Hata hivyo, amewasihi wazazi kukaa na kuzungumza na watoto wao wajue wanakabiliwa na changamoto gani ili wazitatue (hakufafanua zaidi).

Baba wa marehemu, Francis Lema amesema watoto hao walikuwa wanataniana, utani uliozua mauti kwa mmoja.

“Ulikuwa kama utani ambao uligeuka kuwa mabishano makali mpaka wakapigana mwilini, mtuhumiwa (anamtaja jina) alipoona anazidiwa nguvu, akakimbilia kuchukua panga na kumkata mwenzake shingoni na kiganja cha mkono, mwanangu amekufa, sina la kusema,” amesimulia baba huyo huku akibubujikwa machozi.

Hata hivyo, amesema maziko ya mwanawe yatafanyika kesho Ijumaa, Septemba 13, 2024, baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika.

Chanzo: Mwananchi
 
Shetani Yuko kazini,.
Ila Watoto wa Miaka 17 saa4 usiku kijiweni wanafanya nini?,. Wazazi mnatakiwa kujitafakari
 
Maamuzi mengine ni ya kipuuzi sana
rip huyo dogo ni bora angekubali tu kuwa yeye ni mdogo
VERY SAD.
 
Back
Top Bottom