Nimekutana na mwalimu wangu, mtu mzee kiasi kwani kanifundisha sekondari. Kasema oho, unaona Magufuli anayofanya?
Nikamuuliza anafanya nini, akanijibu kazuia safari za nje, kakamata wezi bandari, katimua TRA, nk. Nikasema BURE KABISA. Mwalimu akanishangaa, akaniuliza we ya Magufuli huyaoni? Nikasema nayaona, lakini bure kabisa.
Akasema we ulikuwa mwanafunzi mbishi tokea zama zile. Nikamuuliza kwani unafanya kazi gani siku hizi? akasema, bado mwalimu. Nikamuuliza umewahi kumsifia mwanafunzi wako yoyote, achilia mimi niliyekuwa naongoza na bado hukunisifia. Akasema, ningekusifia ungevimba kichwa.
Nikamuuliza, sasa mbona unamsifia Magufuli? Aha, akajibu. Sasa nimekupata mwanafunzi wangu. Magufuli bure kabisa.
Unasemaje na wewe. Maana hadi sasa tumeona pasi na chenga nyiiiingi. Je, kuna goli? Magufuli bure kabisa. Unamuunga mkono mwalimu wangu?