Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 752
- 1,810
Mwalimu wa Chuo cha Ufundi cha Arusha (ATC) Lusato Kanyika anashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani hapa kwa madai ya kukutwa na mwanafunzi wa chuoni hapo katika nyumba ya kulala wageni akidai rushwa ya ngono.
Akizungumza chuoni hapo Afisa Habari wa ATC,Gasto Leseiyo alikiri mwalimu huyo kutuhumiwa kudai rushwa ya ngono kwa lengo la kumsadia kufaulu somo la mafunzo viwandani (IPT).
Hata hivyo alishangazwa na hatua ya mwalimu huyo kukumbwa na pepo LA ngono wakati yeye ni mwokovu anampenda yesu.
Alisema chuo hicho kimeshtushwa na taarifa hiyo ya rushwa ya ngono na itatoa ushirikiano kwa Takukuru endapo wakiitwa kuhojiwa kwa Mwalimu huyo
Alisema chuo kinatoa pole kwa familia ya mwanafunzi huyo wa kike pamoja na wanafunzi chuoni hapo lakini tunajiuliza kwanini mwanafunzi huyu wa kike alipoona anasumbuliwa na Mwalimu Kanyika hakutoa taarifa kwa kamati ya maadili ya shule au hata msimamizi wake
Ukiangalia Mwalimu mwenyewe ni mtu ameshika dini tunashangaa kwa tuhuma hizi za rushwa ya ngono
Awali Kwamujibu wa Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani hapa,Frida Wikesi alikiri kuchunguza tuhuma hizo na endapo ikidhibitika ni kweli mwalimu huyo aliomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi huyo watatoa taarifa rasmi
Wikesi alidai kuwa mwalimu huyo yupo nje kwa dhamana baada ya kukamatwa Agosti 2 mwaka huu baada ya kuwekewa mtego akiwa katika nyumba moja ya kulala wageni(Jina linahifadhiwa)jijini hapa.
Alisema jalada la kesi hiyo limepelekw kwa mwanasheria wa serikali kuandaliwa mashtaka na kwamba iwapo litarejea watamfikisha mahakamami muda wowote uchunguzi ukikamilika.
Ends......