Mwalimu Nyerere na sifa zisizobishaniwa

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,197
7,676
Bahati mbaya vijana wengi humu JF hawakuwahi kumwona wala kumwelewa Mwalimu Nyerere. Mimi nilibahatika nyakati hizo nikiwa shule ya msingi, kiongozi wa chipukizi, nilipeana mkono naye kara moja. Na mara ya pili na ya tatu l, akiwa amestaafu.

Nilipata kuvisoma vitabu vyake vichache, na wakati fulani kuyarudia maneno kwenye matukio mbalimbali rasmi ya kiserikali. Nukuu hizi zilitoka kwenye vitabu vyake alivyoviandika kwa lugha ya Kiingereza. Baadhi ya sifa zake zisizobishaniwa, ni pamoja na:

1) Mwalimu alikuwa super intelligent kwa kiwango ambacho hatujawahi kubahatika kumpata Rais wa kiwango hicho.
Na hilo lilithibitika na hata historia yake katika kumudu masomo yake. Mwalimu alikuwa miongoni mwa watanzania watatu wa mwanzo kuwa na kiwango cha elimu ya chuo kikuu.

2) Mwalimu alikuwa na karama ya uongozi. Hilo linadhirika tangu akiwa shuleni. Kila ngazi, wanafunzi wenzake walimchagua kuwa kiongozi. Nafasi zake zote za uongozi zilitokana na ushawishi na siyo nguvu ya dola. Ikumbukwe Mwalimu hakuanzisha TAA, lakini alipojiunga TAA, viongozi wa wakati huo kwa hiari yao waliamua kumwachia Mwalimu awaongoze. Viongpzi wetu wa leo, wanatumia hila mbalimbali ikiwemo kuiba kura, kutoa rushwa na wakati fulani kuwaengua wapinzani wao kwa hila. Ni kwa sababu hawana ushawishi. Uwezo wa Mwalimu wa kushawishi, hakuna Rais hata mmoja aliwahi kuufikia hata kwa 50%. Ushawishi wa Mwalimu uliweza hata kuwafanya wakoloni waipe Tanganyika uhuru bila ya kumwaga damu. Viongozi wetu wa leo, wanategemea zaidi vipigo toka polisi, utekaji wa wasiojulikana ili kubakia kwenye nafasi zao.

3) Mwalimu Nyerere alikuwa na upeo mkubwa kuzidi Rais yeyote aliyefuatia. Mwalimu Nyerere alitambua kuwa nchi haiwezi kupata maendeleo bila ya kuwa na taasisi za utafiti ambako unatarajia upate ukweli wa mambo mbalimbali. Alianzisha vituo vya utafiti wa magonjwa, utafiti wa zana za kilimo, vituo vya utafiti wa samaki, vituo vya utafiti wa kilimo, n.k. Waliofuatia waliviua vituo hivyo na wala hawakuweza kuanzisha vituo vingine vipya. Taasisi mbalimbali zilizoanzishwa na Mwalimu Nyerere, hata majengobyake tu, huwezi kulinganisha na ya sasa. Kwa mfano, angalia UDSM, linganisha na UDOM. Itazame hosputali ya rufaa ya Muhimbili wakati huo, linganisha na hospitali za rufaa utitiri zilizopo leo.

4) Mwalimu, ndani ya mfumo wa chama kimoja, alijenga mifumo imara ya kidemokrasia kwa kiwango cha wakati huo. Nyakati zake, hakuna mgombea ambaye alitumia polisi, wasiojulikana, au kununua kura. Mfumo ule ulikuwa wa wazi kuliko hata mfumo wa vyama vingi tulio nao leo. Leo hii, wabunge waliopo Bungeni, robo tatu hawakupitishwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM(waliteuliwa tu kakikundi ka watu). Kilichofanyika kwenye uvhaguzi 2020 ni uchafu usiostahili hata kutamkwa. Ule msisitizo wa mwalimu kuwa maamuzi yatokane na vikao, umepotea jumla. Hata mabadiliko ya ndani ya CCM, yalikuwa ni mashinikizo ya kakikundi ka watu. Waliotaka kuhoji, polisi walitumika kuwazima (udikteta, kwa kadiri ya tafsiri ya Mwalimu).

5) Mwalimu alikuwa maskini wa roho. Angetaka angeweza kuwa tajiri kupindukia kutokana na mazingira ya wakati huo, lakini aliwatazama zaidi Watanzania kuliko kujitazama yeye na familia yake. Niliwahi kushiriki chakula cha jioni pamoja na Mwalimu nyumbani kwake Butiama, akiwa amestaafu, hakika kuanzia mazingira, mpaka chakula chenyewe, killikuwa cha kawaida sana ambacho mwanakijiji wa kawaida anamudu kukipata. Mwalimu hakuwahi kujiona bora kuliko wanadamu wengine. Kaunda suti zake zilikuwa zikishonwa na fundi cherahani pale Kariakoo. Hakuna Rais hata mmoja, baada yake aliyeamua kuishi kama wananchi wake wanavyoishi. Wote waliofuatia, kwa kiasi fulani, nafasi ya Urais ilionekana ni nafasi ya kuwaingiza familia zao, ndugu zao, marafiki na wanafiki wa kusifia, kwenye nafasi za uongozi.

6) Mwalimu alikuwa mwanafalsafa. Alikuwa na itikadi yake kama kiongozi, na akaushawishi umma umfuate katika anachokiamini. Aliitetea falsafa yake. Aliandika vitabu mbalimbali ambavyo ukivisoma, unakubali kuwa ni fikra za mwandishi mwenye akili kubwa. Hakuna Rais hata mmoja aliyeandika vitabu kufikia hata 50% ya vile vya Mwalimu.

7} Mwalimu alikuwa na uwezo wa kuyaona mambo kabla ya kutokea. Na hiyo ni dalili kubwa ya mtu ambaye ni super intelligent. Mwalimu aliwaona viongozi watakaotumia vibaya katiba kabla hawajatokea. Na akaonya kuwa katiba ni mbaya. Wakitokea madikteta wataitumia vibaya. Baadaye imekuja kudhihirika. Alieleza ishara za udikteta, na sasa tunashuhudia yale aliyowahi kuyanena.

Mwalimu aliishi, anaishi na ataendelea kuishi, japo mwili wake upo ardhini. Viongozi wengine waliishi na kisha wakafariki mwili, roho na fikra.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,tunakukumbuka sana, kwa sababu ya uadilifu, ukweli kwa nafsi yako, upendo wako wa kweli kwa Taifa lako.

Kama walivyo wanadamu wote, pamoja na mengi mazuri uliyoyatenda, yawezekana kuna mahali ulipungukiwa, la wewe mwenyewe ulivyowahi kunena

"Tulifanya mazuri lakini tulifajya makosa pia. Tusifanye makosa, sisi ni malaika?"

Mungu wetu, uliye tajiri wa msamaha, pale mtumishi wako alipopujgukiwa, umjalie msamaha kamili ili naye awe miongoni mwa watakatifu wako, wanaoizunguka meza yako, wakikusujudia na kukusifu usiku na mchana, na sala zake zikalete baraka kwa Taifa la Tanzania alilolipenda bila hila bali kwa moyo uliokamili usio na unafiki. Tunaomba uliepusha Taifa lako dhidi ya viongozi wanafiki na walaghai wanotaka waliongoze Taifa lako kwa hila, uwongo, vitisho na ulaghai. Huo uovu waufanyao, ukawe adhabu yao ya Duniani na Mbinguni.
 
Pamoja na sifa zote hizo kwa nini alifahamu vizuri katiba yetu ilikuwa na mapungufu makubwa na ingeweza kutumika vibaya ila hakufanya jambo lolote kuirekebisha na kutuachia katiba bora?
 
Ni miongoni mwa mapungufu yake. Hata yeye aliliona hilo.
 
Pamoja na sifa zote hizo kwa nini alifahamu vizuri katiba yetu ilikuwa na mapungufu makubwa na ingeweza kutumika vibaya ila hakufanya jambo lolote kuirekebisha na kutuachia katiba bora?
Unaweza kuorodhesha "mapungufu makubwa" matatu ya katiba yetu kwa kututajia vifungu vyake?
 
41.- (7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake.

46.-(1) Wakati wote Rais atakapokuwa bado ameshika madaraka yake kwa mujibu wa Katiba hii, itakuwa ni marufuku kumshitaki au kuendesha mashataka ya aina yoyote juu yake mahakamani kwa ajili ya kosa lolote la jinai.

90.-(2)Rais hatakuwa na uwezo wa kulivunja Bunge wakati wowote, isipokuwa tu-

77.-(3)Wagombea uchaguzi katika jimbo la uchaguzi watatakiwa watimize masharti yafuatayo- (a) wawe wamependekezwa mmoja mmoja, na chama cha siasa kinachoshiriki uchaguzi katika jimbo hilo;

74.-(1) Kutakuwa na Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao watakaoteuliwa na Rais:
 
Hayo mengine upo sawa, hilo la 46(1) umewahi kusikia Rais yeyote popote duniani kashtakiwa akiwa madarakani?
 
Bahati mbaya vijana wengi humu JF hawakuwahi kumwona wala kumwelewa Mwalimu Nyerere. Mimi nilibahatika nyakati hizo nikiwa shule ya msingi, kiongozi wa chipukizi, nilipeana mkono naye kara moja. Na mara ya pili na ya tatu l, akiwa amestaafu.

Nilipata kuvisoma vitabu vyake vichache, na wakati fulani kuyarudia maneno kwenye matukio mbalimbali rasmi ya kiserikali. Nukuu hizi zilitoka kwenye vitabu vyake alivyoviandika kwa lugha ya Kiingereza. Baadhi ya sifa zake zisizobishaniwa, ni pamoja na:

1) Mwalimu alikuwa super intelligent kwa kiwango ambacho hatujawahi kubahatika kumpata Rais wa kiwango hicho. Na hilo lilithibitika na hata historia yake katika kumudu masomo yake. Mwalimu alikuwa miongoni mwa watanzania watatu wa mwanzo kuwa na kiwango cha elimu ya chuo kikuu.

2) Mwalimu alikuwa na karama ya uongozi. Hilo linadhirika tangu akiwa shuleni. Kila ngazi, wanafunzi wenzake walimchagua kuwa kiongozi. Nafasi zake zote za uongozi zilitokana na ushawishi na siyo nguvu ya dola. Ikumbukwe Mwalimu hakuanzisha TAA, lakini alipojiunga TAA, viongozi wa wakati huo kwa hiari yao waliamua kumwachia Mwalimu awaongoze. Viongpzi wetu wa leo, wanatumia hila mbalimbali ikiwemo kuiba kura, kutoa rushwa na wakati fulani kuwaengua wapinzani wao kwa hila. Ni kwa sababu hawana ushawishi. Uwezo wa Mwalimu wa kushawishi, hakuna Rais hata mmoja aliwahi kuufikia hata kwa 50%. Ushawishi wa Mwalimu uliweza hata kuwafanya wakoloni waipe Tanganyika uhuru bila ya kumwaga damu. Viongozi wetu wa leo, wanategemea zaidi vipigo toka polisi, utekaji wa wasiojulikana ili kubakia kwenye nafasi zao.

3) Mwalimu Nyerere alikuwa na upeo mkubwa kuzidi Rais yeyote aliyefuatia. Mwalimu Nyerere alitambua kuwa nchi haiwezi kupata maendeleo bila ya kuwa na taasisi za utafiti ambako unatarajia upate ukweli wa mambo mbalimbali. Alianzisha vituo vya utafiti wa magonjwa, utafiti wa zana za kilimo, vituo vya utafiti wa samaki, vituo vya utafiti wa kilimo, n.k. Waliofuatia waliviua vituo hivyo na wala hawakuweza kuanzisha vituo vingine vipya. Taasisi mbalimbali zilizoanzishwa na Mwalimu Nyerere, hata majengobyake tu, huwezi kulinganisha na ya sasa. Kwa mfano, angalia UDSM, linganisha na UDOM. Itazame hosputali ya rufaa ya Muhimbili wakati huo, linganisha na hospitali za rufaa utitiri zilizopo leo.

4) Mwalimu, ndani ya mfumo wa chama kimoja, alijenga mifumo imara ya kidemokrasia kwa kiwango cha wakati huo. Nyakati zake, hakuna mgombea ambaye alitumia polisi, wasiojulikana, au kununua kura. Mfumo ule ulikuwa wa wazi kuliko hata mfumo wa vyama vingi tulio nao leo. Leo hii, wabunge waliopo Bungeni, robo tatu hawakupitishwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM(waliteuliwa tu kakikundi ka watu). Kilichofanyika kwenye uvhaguzi 2020 ni uchafu usiostahili hata kutamkwa. Ule msisitizo wa mwalimu kuwa maamuzi yatokane na vikao, umepotea jumla. Hata mabadiliko ya ndani ya CCM, yalikuwa ni mashinikizo ya kakikundi ka watu. Waliotaka kuhoji, polisi walitumika kuwazima (udikteta, kwa kadiri ya tafsiri ya Mwalimu).

5) Mwalimu alikuwa maskini wa roho. Angetaka angeweza kuwa tajiri kupindukia kutokana na mazingira ya wakati huo, lakini aliwatazama zaidi Watanzania kuliko kujitazama yeye na familia yake. Niliwahi kushiriki chakula cha jioni pamoja na Mwalimu nyumbani kwake Butiama, akiwa amestaafu, hakika kuanzia mazingira, mpaka chakula chenyewe, killikuwa cha kawaida sana ambacho mwanakijiji wa kawaida anamudu kukipata. Mwalimu hakuwahi kujiona bora kuliko wanadamu wengine. Kaunda suti zake zilikuwa zikishonwa na fundi cherahani pale Kariakoo. Hakuna Rais hata mmoja, baada yake aliyeamua kuishi kama wananchi wake wanavyoishi. Wote waliofuatia, kwa kiasi fulani, nafasi ya Urais ilionekana ni nafasi ya kuwaingiza familia zao, ndugu zao, marafiki na wanafiki wa kusifia, kwenye nafasi za uongozi.

6) Mwalimu alikuwa mwanafalsafa. Alikuwa na itikadi yake kama kiongozi, na akaushawishi umma umfuate katika anachokiamini. Aliitetea falsafa yake. Aliandika vitabu mbalimbali ambavyo ukivisoma, unakubali kuwa ni fikra za mwandishi mwenye akili kubwa. Hakuna Rais hata mmoja aliyeandika vitabu kufikia hata 50% ya vile vya Mwalimu.

7} Mwalimu alikuwa na uwezo wa kuyaona mambo kabla ya kutokea. Na hiyo ni dalili kubwa ya mtu ambaye ni super intelligent. Mwalimu aliwaona viongozi watakaotumia vibaya katiba kabla hawajatokea. Na akaonya kuwa katiba ni mbaya. Wakitokea madikteta wataitumia vibaya. Baadaye imekuja kudhihirika. Alieleza ishara za udikteta, na sasa tunashuhudia yale aliyowahi kuyanena.

Mwalimu aliishi, anaishi na ataendelea kuishi, japo mwili wake upo ardhini. Viongozi wengine waliishi na kisha wakafariki mwili, roho na fikra.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,tunakukumbuka sana, kwa sababu ya uadilifu, ukweli kwa nafsi yako, upendo wako wa kweli kwa Taifa lako.

Kama walivyo wanadamu wote, pamoja na mengi mazuri uliyoyatenda, yawezekana kuna mahali ulipungukiwa, la wewe mwenyewe ulivyowahi kunena

"Tulifanya mazuri lakini tulifajya makosa pia. Tusifanye makosa, sisi ni malaika?"

Mungu wetu, uliye tajiri wa msamaha, pale mtumishi wako alipopujgukiwa, umjalie msamaha kamili ili naye awe miongoni mwa watakatifu wako, wanaoizunguka meza yako, wakikusujudia na kukusifu usiku na mchana, na sala zake zikalete baraka kwa Taifa la Tanzania alilolipenda bila hila bali kwa moyo uliokamili usio na unafiki. Tunaomba uliepusha Taifa lako dhidi ya viongozi wanafiki na walaghai wanotaka waliongoze Taifa lako kwa hila, uwongo, vitisho na ulaghai. Huo uovu waufanyao, ukawe adhabu yao ya Duniani na Mbinguni.
JKN and undisputed profile.
 
Hayo mengine upo sawa, hilo la 46(1) umewahi kusikia Rais yeyote popote duniani kashtakiwa akiwa madarakani?
Lakini sio kwa kujiwekea mipaka. Ukishaweka kwenye maandishi maana yake unakusudiwa kuvunja haki za Raia wako kwa kupanga.
 
Pamoja na sifa zote hizo kwa nini alifahamu vizuri katiba yetu ilikuwa na mapungufu makubwa na ingeweza kutumika vibaya ila hakufanya jambo lolote kuirekebisha na kutuachia katiba bora?
Mwl alijua pia kuwa ukiwa na katiba yenye demokrasia pana utashindwa kuwa govern raia wako ambao wengi mpaka leo hawana critical thinking, wana poverty kubwa ambayo inawasababisha ku compromize mambo mengi wakishawishiwa na cash au inventives fulani....Mwl kama JPM makosa yao yalikuwa kwa dhamira njema kabisa...Ili kujilinda wao na kulinda maslahi ya nchi tofauti na wengine wetu ambao tunajifikiria kwanza hata kwa gharama ya taifa zima.
 
Kwakifupi mwalim angekuwepo tanzania ingekua isha dominate east africa na ukanda wote wa maziwa makuu.Hiv vikina paul kagame na museven vingekua vi watu vya kutufanya tukose utulivu
 
Alikaa madarakani miaka 26 akiongoza nchi iliyokuwa na utulivu mkubwa kwa muda mrefu ila Tanzania haikuipita Kenya iliyokuwa ina mapambano makali ya kidemokrasia.
Kwakifupi mwalim angekuwepo tanzania ingekua isha dominate east africa na ukanda wote wa maziwa makuu.Hiv vikina paul kagame na museven vingekua vi watu vya kutufanya tukose utulivu
 
Raia wa chini hawali rushwa wala hawashawishiwi na mabeberu. Viongozi walio katika nafasi za juu ndio wana compromise, wanafanya ufisadi kwa kushirikiana na mabeberu. Unapokuwa na katiba isiyoweka demokrasia pana hali inakuwa mbaya zaidi kwa sababu hao viongozi wafujaji hawatawezwa kuwajibishwa na umma mpana.
Mwl alijua pia kuwa ukiwa na katiba yenye demokrasia pana utashindwa kuwa govern raia wako ambao wengi mpaka leo hawana critical thinking, wana poverty kubwa ambayo inawasababisha ku compromize mambo mengi wakishawishiwa na cash au inventives fulani....Mwl kama JPM makosa yao yalikuwa kwa dhamira njema kabisa...Ili kujilinda wao na kulinda maslahi ya nchi tofauti na wengine wetu ambao tunajifikiria kwanza hata kwa gharama ya taifa zima.
 
Trump amefunguliwa kesi nyingi akiwa madarakani.
Hajawahi kufunguliwa kesi ya jinai akiwa madarakani, sidhani pia kama kuna kesi yeyote ile imewahi kufunguliwa akiwa madarakani! Ila uchunguzi mbalimbali juu ya mienendo yake umewahi kufanyika, not kupandishwa kizimbani
 
Lakini sio kwa kujiwekea mipaka. Ukishaweka kwenye maandishi maana yake unakusudiwa kuvunja haki za Raia wako kwa kupanga.
Isipokuwa kwenye katiba sasa ndiyo italeta mkanganyiko na mitafaruku! Ni kama Sirro juzi aliposema definition ya kikao cha ndani/nje haijawekwa wazi kwenye sheria ya vyama vya siasa, hiyo inaleta mkanganyiko kwao
 
Back
Top Bottom