Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,581
- 1,189
MWAKIBETE AONGOZA HARAMBEE NDOGO BUSOKELO GIRLS SEC, ATOA MILIONI 15
Mbunge wa Jimbo la Busokelo Atupele Fredy Mwakibete ameongoza harambee ndogo ya wazazi na walimu katika mahafali ya Tano ya shule ya Sekondari ya Wasichana Busokelo.
Akiwa kama Mgeni Rasmi katika Mahafali ya Kidato cha Nne shule ya wasichana Busokelo,Mwakibete ametumia hadhara hiyo kuwaomba wazazi kushiriki kwa kichache ili kutatua baadhi ya Changamoto ikiwemo Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu ambapo wananchi wa Kandete wameanza michango hadi sasa.
Katika Changizo hilo wazazi wamechanga zaidi ya Taslimu Laki Nane na kumfanya Mbunge kujazia na kufanya michango ya wazazi kufika Shilingi Milioni Moja,huku Mgeni Rasmi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Busokelo Atupele Mwakibete Kutoa Shilingi Milioni Kumi na Tano kwa ajili ya Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu.
Pia kuhusu Motisha kwa Wanafunzi na Walimu Mwakibete amesema kuwa kama alivyoahidi Busokelo Boys vivyo hivyo kwa Mwanafunzi atakaepata Daraja la Kwanza (Div 1.7) atapata shilingi Milioni Moja na kwa Mwalimu atakaefaulisha kwa Wastani wa Alama A atapata shilingi Laki Moja kwa kila somo.
Aidha kuhusu changamoto nyingine ikiwemo ujenzi wa Uzio ulioahidiwa na Waziri wa Fedha Dkt Mwigulu Nchemba,mwakibete amesema kuwa Tayari amewasiliana na Waziri na amesema robo ijayo fedha hizo zitafika shuleni hapo ili kujenga uzio na kazi yake itakua ni kufuatilia.
Aidha ametumia Hadhara hiyo kuwaomba wazazi na walezi kuhakikisha gharama walizotumia kuwekeza katika elimu kwa watoto wao wanaendeleza vyema baada ya kuhitimu kwani shule hizi Mbili ni kioo cha Elimu kwani zinashika nafasi za kwanza Kiwilaya na Kimkoa.