Lethergo
JF-Expert Member
- Aug 7, 2023
- 6,502
- 11,400
Wakuu,
Awali ya yote nitakachokiandika hapa naomba kieleweke kwa Jicho la tatu sio Jicho la kawaida.
Mwaka 2025 ndio mwaka ambao wanaume wengi hususani vijana watakatisha uhai wao kwa wingi sana.
Wanaume wengi wanaishi na mambo mazito mioyoni mwao na hawana pa kusemea ila wanaishi ilimradi tu kuishi huku ndani kwa ndani vitu vikiwatafuna kidogo kidogo.
Wanaume wengi wanaendeshwa na Wanawake waliowaoa au wanaoishi nao kinyumba au wanaokaa nao kwenye mazingira yao, tafadhari sana elewa namaanisha kuendeshwa.
Wanaume wengi wanapitia hali ngumu za kimaisha kwa sasa ila hawana pa kusemea na wengi wao wanaoishia kukaa kimya maana wakisema wanaonekana sio wanaume.
Vifo vya Wanaume kwa Mwaka huu 2025 vitakua ni vingi sana hususani vijana wasio na ajira ambao wengi wao wamejiingiza kwenye uraibu wa pombe, wanawake na kamari.
Vijana na wanaume watakatisha sana uhai wao kwa mwaka 2025 kwa sababu tofauti tofauti.
Vijana wasio na ajira ambao wanapitia kipindi cha ukata wa kifedha, uchumi mbovu na msongo wa mawazo hasa hasa vijana wa kiume ambao wao hawana option nyingi km ilivyo kwa vijana wa kike.
Vijana wa kike wana option nyingi za upendeleo tofauti na ilivyo kwa vijana wa kiume. Option moja wapo ambayo wengi wao inawabeba vijana wa kike ni kuolewa na kua mama wa nyumbani km hawana kazi au ajira rasmi. Hio option kijana wa kiume ambae hana ajira au hajajipata haipo hakuna atakae kuoa wewe kijana wa kiume na kukufanya uwe mama wa nyumbani.
Nini kifanyike?
Serikali na wadau mbalimbali waangalie namna ya kuwakomboa hawa vijana wa kiume waliokata tamaa ya kuishi ambao wengi wanaangamia huku mtaani bila hivyo kwa huu mwaka idadi ya vijana wanaojiua kila siku itakua ni kubwa sana.
Familia, ndugu, marafiki na jamaa wa karibu pamoja na wana jamii wengine wawaangalie hawa vijana waliokata tamaa ya kuishi kwa namna tofauti jinsi na namna ya kuwasaidia na sio kuwatenga na kuwasema vibaya. Oh umesoma sasa kiko wapi huna kazi huna ajira upo upo tu mtaani hueleweki huna chochote unachokifanya cha kimaendeleo na umri unakwenda.
Wanawake wengi wenye midomo michafu inayoongea maneno machafu machafu kuwaongelea vibaya kuhusu hawa vijana wa kiume ambao wanapitia hali ya kukata tamaa ya kuishi wapunguze hio hali ya kuongea vibaya na kuwaongelea mbovu maana inawasononesha sana na kuwatia simanzi wengi hufikia hatua ya kuona hakuna maana ya kuishi na kuishi kujiua.
Vijana walio wengi huku mitaani nyuso zao zimejaa simanzi nzito sana wengi wanaishi na sonona na kukata tamaa ya kuishi wanaishi tu basi watafanyaje ila inafika hatua ya kuchoka ndio wanachukua uamuzi wa kujiondoa duniani. Misiba ni mingi na mingine itatokea mwaka huu.
Majuzi kumetokea misiba mingi ya vijana wa kiume wanaojiua kwa namna mbalimbali bila watu kujua kua hawa wamejiua, kisa cha kwanza kilikua cha ajali ila ukiangalia kwa makini sio ajali km ajali bali wamejiua, kisa kingine amejiua ndani kwake usiku majuzi ila watu hawakujua km amejiua.
Mwingine amejiua tena ndani kwake majuzi hio hio baada ya kumaliza msiba wa rafiki yake aliemzika na yeye akaenda kujiua km alivyojiua mwenzake na hakuna aliehisi wala kudhani km amejiua ila kiundani ukiangalia unagundua amejiua.
Mwingine tena imetokea huko Mbeya Jana hii ndio imeenda viral mpaka kwenye vyombo vya habari imetangazwa na kuandikwa maana baada ya kujiua aliacha ujumbe bila hivyo hakuna ambae angeelewa na kujua km amejiua. Anasema amejiua baada ya kuliwa elfu 90 kwenye mchezo wa kamari almaarufu km dubwi yeye ni dereva wa Bajaj.
Uzi ubaki hapa tusuburie mwaka uishe mtasema nilisema.
Nimemaliza.