Mwaka 2023, wakenya milioni 12 walisafiri kwa ndege ilhali watanzania milioni 3.8. Je, sisi watanzania shida ni umaskini au tunaogopa kusafiri?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
61,773
72,209
Kwa mujibu wa takwimu za usafiri zilizotolewa na mamlaka ya anga ya Nchi zote inaonesha wakenya wakitumia usafiri wa ndege mara 3 zaidi ya Watanzania ambapo takribani watu Milioni 12.3 walisafiri kwa Ndege huko Kenya wakiwemo wageni zaidi ya mil. 5 na raia zaidi ya mil. 6.

1721731079075.png

Kwa upande wa Tanzania ,mwaka huo huo takribani watu Mil.3.8 wakitumia usafiri wa ndege ambapo kati ya hao zaidi ya mil.2 ni wageni na raia ni chini ya mil.2.

Kwa takwimu hizi ,hivi ni kwamba Watanzania sisi ni maskini kiasi hicho au Kuna sababu zingine zinazofanya hatusafi Kwa Ndege?

Unaweza Kuta 90% ya Watanzania hawajawahi kuona tiketi ya ndege. Naomba kuwasilisha 👇👇

The Citizen Tanzania The Tanzania Airport Authority (TAA) has recorded a 13% increase in passe...png
 
Umasikini unaambatana na lack of knowledge, na hiyo inazaa watu wenye low IQ , madhara yake wanawekeana vikwazo kwa kwenda nje or hawaoni opportunity za kwenda nje

Na wakishindwa wanaenda kuwaponda wanao enda huko. And that say something kwa jamii ya kitanzania
 
Wakenya wengi ni manesi nchi za ulaya na marekani

Wakenya wengi ni ma house girl uarabuni.

Hivyo wanasafiri sana kwa ndege kwenda majuu makazini kwao na kurudi kenya likizo ama kuhudhuria misiba ya wazazi wao.

Tofauti na wabongo wengi wanafanya kazi hapa hapa bongo. Na wachache ni ma house girl uarabuni.. ambao hawana tabia ya kurudi bongo mara kwa mara
 
Hizi takwimu zinajumuisha ndege za kienyeji? Maana nimeongea na waha na wa sumbawanga wamepata mshituko mkubwa.

Halafu hao ni wakenya kwa uraia, au umehesabu na watalii? Maana watanzania wakiona kitu kibaya basi ni cha kwao, kizuri cha jirani. Ukute mtanzania anasifia mnyarwanda, mkenya, yaani tumeumbwa kujidharau
 
Kusafiri kwa ndege kwa baadhi ya nchi ni lazima wala sio anasa kutokana na ubovu wa miundombinu na usalama. Wakongo wanapanda sana ndege kutokana na ubovu wa barabara zao na usalama mdogo. Hivyo hauwezi kusema wakongo ni matajiri sana kuliko watanzania kisa wanapanda ndege.
Sawa lakini Haina maana ya kwamba watanzania hatupandi sana ndege kwa ubora na usalama wa Barbara, I think 🤔 sababu ni Individual financial capability
Kipato kinafanya tuone kupanda ndege ni ANASA🦹
 
Passport ni anasa bongo utataja hadi jina la jirani wa nyanya ako aliyefariki 1947.

Wabongo wengi hawana exposure. Wamejazwa ujinga bongo ni mbinguni kila mtu anatuonea wivu kwa mali zetu, mali zenyewe hamna. So wengi wamerundikana bongo kama nyanya.

And of course umaskini. GDP ya Kenya almost doubles ile ya Tanzagiza.
 
Watanzania wengi hutumia usafiri wa mabasi ndani ya mipaka ya nchi kwa upande wa ndege ni swala la muda tu...na sisi tuta wapita wakenya ili tuwe namba afu wao wawe nyuma yetu😎😎😎
 
Passport ni anasa bongo utataja hadi jina la jirani wa nyanya ako aliyefariki 1947.

Wabongo wengi hawana exposure. Wamejazwa ujinga bongo ni mbinguni kila mtu anatuonea wivu kwa mali zetu, mali zenyewe hamna. So wengi wamerudhikana kana tu bongo kama nyanya.

And of course umaskini. GDP ya Kenya almost doubles ile ya Tanzagiza.
Umeanza kwa pumba then ukamaliza kwa points 3
I think GDP ndo sababu kubwa,,
Individual financial capability kwetu bado ni disaster, so lazima tuone kupanda ndege ni ANASA✌️
 
Umeanza kwa pumba then ukamaliza kwa points 3
I think GDP ndo sababu kubwa,,
Individual financial capability kwetu bado ni disaster, so lazima tuone kupanda ndege ni ANASA✌️

Pumba gani?

Hujui wabongo wengi bado washamba? Hawa ndugu zako hawajui lolote duniani, hawajui vitu vidogo tu kama tofauti ya L na R; a na ha nk. Utawapelekea wapi dunia ya leo? Angalia reasoning yao mitandaoni. Tatizo namba moja TZ sio katiba wala CCM ni ujinga.

Na wewe unaaamini ujinga wa kwamba bongo inaonewa wivu duniani wakati in reality duniani bongo haifahamiki hadi useme ipo karibu na Kenya? Mali za bongo za kawaida sana, mmejazwa ujinga tu and y'all fell for it.
 
Kwa Mujibu wa takwimu za usafiri zilizotolewa na mamlaka ya anga ya Nchi zote ,inaonesha WaKenya wakitumia usafiri wa ndege mara 3 zaidi ya Watanzania ambapo takribani watu Milioni 12.3 Walisafiri Kwa Ndege huko Kenya wakowemo wageni zaidi ya mil.5 na raia zaidi ya mil.6.
View attachment 3050756

Kwa upande wa Tanzania ,mwaka huo huo takribani watu Mil.3.8 wakitumia usafiri wa ndege ambapo kati ya hao zaidi ya mil.2 ni wageni na raia ni chini ya mil.2.

Kwa takwimu hizi ,hivi ni kwamba Watanzania sisi ni maskini kiasi hicho au Kuna sababu zingine zinazofanya hatusafi Kwa Ndege?

Unaweza Kuta 90% ya Watanzania hawajawahi kuona tiketi ya ndege.Naomba kuwasilishwa 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C9wu0Z2ou6d/?igsh=OHgzcnVyZXZjcmFk

Kenya Kuna ufukara wa kutisha,hata kula shida,kwa nini wasikimbie kwao!?
 
Back
Top Bottom