BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,804
Takwimu za Maambukizi mapya ya VVU zimeonesha Wasichana wenye miaka 15-24 walioambukizwa VVU kila wiki walikuwa 212, sawa na wastani wa Maambukizi mapya 30 kila siku.
Kwa mujibu wa WHO, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2021 kulikuwa na watu milioni 38.4 wanaoishi na VVU Duniani kote, ambapo waathirika milioni 25.6 walikuwa barani Afrika.
=====================
TAKRIBANI asilimia 70 ya kundi la vijana kati ya miaka 15-24 wanaopata maambuziki ya mapya ya VVU ni wasichana.
Taarifa iloyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, na Uratibu) George Simbachawene, leo Novemba 30 imeeleza.
Amesema katika mwaka wa 2021 kulikuwa na maambuziki mapya 212 kila wiki kwa kundi la wasichana wa miaka 15-24, huku kukiwa na maambuziki mapya 30 kila siku kwa kundi hilo la wasichana
Simbachawene ametoa taarifa hiyo katika kilele cha shughuli za vijana Mkoani Lindi kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani kesho Disemba Mosi.
Kufuatia taarifa hiyo, Waziri huyo ametoa rai kwa vijana wote nchini kushiriki katika huduma za upimaji wa Virusi vya Ukimwi (VVU) kwa hiari ili waweze kutambua Afya zao na kuchukua hatua stahiki za kujizua na maambuziki ya VVU.
Aidha, Simbachawene amewataka wasichana kuzingatia maudhui ya kampeni mbalimbali ili kujikinga na maambuziki ya VVU.
‘Wale mlio mashuleni na vyuoni hakikisheni mnaweka mkazo katika Elimu na kujiepusha na tabia zote hatarishi zinazopeleka kupata maambuziki ya VVU,” amesema
HABARI LEO