Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,106
- 10,178
Mwaka 2018, MIC Tanzania Limited (Tigo) iliamriwa na Kamati ya Malalamiko ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kumlipa Ogada Ogweno Tsh. 1,000,000 kama fidia ya usumbufu. Pia walitakiwa kumrudishia Tsh 450 waliyoikata kimakosa kwa huduma ambayo hakujiunga
Hali ilikuwa hivi, Ogweno alitaka kujiunga na University offer cha Tsh 500 katika miezi Fulani 2017. Ambapo hela yake ilikatwa lakini kifurushi hakupata. Baadae akawa anakatwa Tsh. 150 kila siku. Aliwasiliana na Tigo na wakamwambia kuwa amejiunga na huduma ya Tigo Hadith ambao wanakata fedha hiyo. Ogweno alikataa kuwa aliwahi kujiunga na huduma hiyo.
Alipeleka malalamiko yake TCRA ambapo alisema kushindwa kupewa kifurushi kumefanya asiwasiliane na baba yake ambayo alikuwa anaugua. Na amepata usumbufu mkubwa. Baada ya Kamati ya Malalamiko ya TCRA kusikiza pande zote wakafikia uamuzi kuwa Ogweno apewe Tsh. 1,000,000 kama fidia ya usumbufu. Pia arudishiwe Tsh 450 ambayo alikatwa kwa huduma ambayo hakujiunga.
Hata wewe unaweza kwena kudai hela kwa huduma usizojiunga