Mtambachuo
JF-Expert Member
- May 6, 2023
- 1,810
- 3,337
Leo Jimbo Katoliki Moshi lilikuwa na Upadrisho wa mashemasi 18 katika Ibada ya misa hiyo ambayo iliiongozwa Askofu Mkuu huyo mstaafu wa wa Jimbo kuu Katoliki la Dar es Salaam.
Mwisho wa Ibada hiyo Askofu wa Jimbo Katoliki Moshi Ludovic Joseph Minde alimpa nafasi Kadinali Pengo kutoa salamu na alisema kuwa Wachagga sio wezi kama inavyosemwa na watu kwani yeye amefanya kazi nao akiwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam na walimsaidia sana kwenye kujenga kanisa na maendeleo yalionekana kwenye nafasi waliozopata katika kulijenga kanisa. Aliongeza kwa kusema kama ni tabia ya udokozi ya mtu sio kwa Wachagga tu pia wapo Wasukuma, Wafipa ma wengine wenye tabia hiyo.
Hivyo nyie mnaopenda kueneza propaganda kuwa Wachagga ni wezi ili wasipate uhalali wa kuongoza acheni hiyo tabia.