Mwabukusi, uchaguzi umekwisha sasa jielekeze kwenye majukumu ya TLS

Huihui2

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
6,829
11,099
Ushauri kwa Mwabukusi. Usicheze na jukwaa jikite katika MALENGO YA KUANZISHWA KWA TLS

Kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha Sheria ya TLS sura ya 307 malengo ya kuanzishwa TLS ni:

(a)Kulinda na kukuza viwango vya taaluma ya sheria na mwenendo wa wanasheria nchini Tanzania;

(b) Kuwezesha upatikanaji wa maarifa ya kisheria kwa wanachama wake na watu wengine;

(c) Kuisaidia serikali na mahakama katika mambo yote yanayohusu sheria, utawala wa sheria na utekelezaji wa sheria;

(d) Kulinda na kuusaidia umma wa watanzania yanayohusu au kuendana au kutokana na sheria;

(e) Kumiliki mali na kuziendeleza kwa faida ya kutimiza malengo yake kwa mujibu wa sheria;6

(f) Kuchangisha au kukopa fedha kwaajili ya uendeshaji wa shughuli zake;

(g) Kujihusisha na uwekezaji wa fedha au rasimali nyingine kama TLS itakavyoona inafaa;

(h) Kufanya kitu kingine chochote kila kinachoendana au kuwezesha kutekeleza malengo yake.
 
Umesahau KAZI mojawapo ya TLS ni uanaharakati wa kuhakikisha Serikali haivunji Katiba.

Tutegemee maandamano ya wanasheria kuhakikisha HAKI inapatikana katika nyanja mbalimbali.

Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote ni sasa.
 
Mtu aliyefeli form six eti ndio watu wanaweka matumaini kwake, na digrii yake ya sheria ya kuokoteza
 
Mbona msukuma bungeni sometimes huwa ana point kuliko "kutulia" . Kuongoza ni busara ziiongoze Elimu yako. Siyo Elimu iongoze busara zako.
 
Ww nani unamshauri mwabukusi cha kufanya?
Ushauri kwa Mwabukusi. Usicheze na jukwaa jikite katika MALENGO YA KUANZISHWA KWA TLS

Kwa mujibu wa kifungu cha 4 cha Sheria ya TLS sura ya 307 malengo ya kuanzishwa TLS ni:

(a)Kulinda na kukuza viwango vya taaluma ya sheria na mwenendo wa wanasheria nchini Tanzania;

(b) Kuwezesha upatikanaji wa maarifa ya kisheria kwa wanachama wake na watu wengine;

(c) Kuisaidia serikali na mahakama katika mambo yote yanayohusu sheria, utawala wa sheria na utekelezaji wa sheria;

(d) Kulinda na kuusaidia umma wa watanzania yanayohusu au kuendana au kutokana na sheria;

(e) Kumiliki mali na kuziendeleza kwa faida ya kutimiza malengo yake kwa mujibu wa sheria;6

(f) Kuchangisha au kukopa fedha kwaajili ya uendeshaji wa shughuli zake;

(g) Kujihusisha na uwekezaji wa fedha au rasimali nyingine kama TLS itakavyoona inafaa;

(h) Kufanya kitu kingine chochote kila kinachoendana au kuwezesha kutekeleza malengo
 
Umesahau KAZI mojawapo ya TLS ni uanaharakati wa kuhakikisha Serikali haivunji Katiba.

Tutegemee maandamano ya wanasheria kuhakikisha HAKI inapatikana katika nyanja mbalimbali.

Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote ni sasa.
Hiyo ndiyo itakayomponza Mwabukusi, akiingia kwq namna hiyo atakwamq
 
Back
Top Bottom