Akiwa anazungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo August 20 Rais wa TLS amewataka Jeshi la Polisi kutoka mbele na kueleza wamefikia wapi uchunguzi wao kuhusu orodha ilie iliyotolewa kwa watu waliotekwa ama kupotea kwa kuchukuliwa na watu wasiyojulikana. TLS ilitoa orodha ya watu zaidi ya 80 huku BBC wakaenda mbali kuonyesha sura zao na walipokuwa wanaishi na siku walizotekwa na watu hao.
Mwabukusi amesema TLS wanafyatilia suala hili na kama polisi wasipochukua hatua basi TLS hawatasita kuchukua hatua.
Rais huyo ametoa wito kwa Watanzania kwa kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake na kukataa kukamatwa na watu wasiyojitambulisha au wenye utambulisho tata bila kuwepo uongozi wako wa serikali za mtaa unaowafahamu.