Mwabukusi atoa pole kufuatia kifo cha Papa Fransisko

deblabant

JF-Expert Member
Oct 7, 2022
2,709
4,124
SALAMU ZA POLE KUFUATIA KIFO CHA BABA MTAKATIFU PAPA FRANCIS

Kwa heshima kuu na huzuni isiyo kifani, napenda kutoa salamu zangu za pole kwa Kanisa Katoliki Tanzania, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), na waumini wote wa Kanisa Katoliki ndani na nje ya mipaka ya taifa letu, kufuatia taarifa za msiba mzito wa kifo cha Baba Mtakatifu PAPA FRANCIS.

Baba Mtakatifu Francis alikuwa kiongozi wa kipekee aliyesimama kidete kwa ajili ya amani, huruma, haki za binadamu, maskini, na mazingira ya dunia. Aliongoza Kanisa la Kristo kwa unyenyekevu wa hali ya juu, busara, na maono ya kiroho yaliyogusa mamilioni ya watu duniani kote, bila kujali imani au mataifa yao.

Katika kipindi chake cha utume, Papa Francis alijitokeza kama sauti ya wanyonge na daraja la maridhiano kati ya mataifa, dini na watu wenye tofauti mbalimbali. Kwa wito wake wa “Kanisa linalotoka na kwenda kwa watu,” alirejesha nguvu ya Injili ya upendo katika maisha ya kila siku ya watu wa Mungu.

Kwa msiba huu, dunia imepoteza kiongozi mashuhuri wa kiroho, mzalendo wa imani, na baba wa kweli kwa familia ya kibinadamu.

Naungana na familia ya Kanisa Katoliki Tanzania na Duniani kote kuomboleza msiba huu, huku nikimuomba Mungu wa rehema ampokee Papa Francis katika raha ya milele, alikostahili kwa kazi njema alizozitenda.

“Amepigana vita vilivyo vizuri, amemaliza mwendo, ameilinda imani.”
(2 Timotheo 4:7)

Bwana alibariki Kanisa Lake.
Amina.
 
Back
Top Bottom