Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,870
- 5,045
Wakuu
Mnakumbuka sakata la CCM Rufiji kumpitisha Mchengerwa mgombea pekee?
Mapya yaibuka huko, panga limepita kwenye Chama
==
Katika Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani, kumekuwa na sintofahamu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo baadhi ya viongozi wa matawi na kata wamedai kusimamishwa kuendelea na nafasi zao kwa kile kinachodaiwa ni kutomuunga mkono Mbunge wa sasa wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa katika jimbo hilo ambalo limeonekana kuwavutia wanasiasa wengine.
Soma: CCM Rufiji kumpitisha Mchengerwa mgombea pekee
Akizungumza na Jambo TV, Ramadhan Kassim, aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Mkongo, ambaye ni miongoni mwa waliodai kusimamishwa, amesema kuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Rufiji alimsimamisha kutoka kwenye nafasi hiyo katika Mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Kata ya Mkongo.
Ramadhan ameeleza kuwa hatua hiyo haikufuata taratibu za chama na ametoa wito kwa viongozi wa juu wa CCM kufika wilayani Rufiji ili kuchunguza suala hilo na kuhakikisha haki inatendeka kwa wote waliokumbwa na hali hiyo.
Sakata hili linatokea wakati joto la uchaguzi wa mwaka 2025 wa Urais, Ubunge na Udiwani likianza kuongezeka, ambapo wanasiasa mbalimbali wamekuwa wakionekana kupalilia njia kuelekea kuteuliwa na vyama vyao kugombea nafasi hizo wakati utakapofika.