MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 12,430
- 27,986
Mimi sio mtu wa mchezo wa masumbwi ila nimelazimika kufuatilia huu mzozo kati ya Mwakinyo na mapromota na kujikuta nimejua mambo kadhaa kuhusu mchezo huo. Na baada ya wengi wenu kunisihi nitoe maoni yangu kuhusu hili sakata nimeona acha nitumie haki yangu ya kikatiba ya uhuru wa kutoa maoni. Na haya maoni yangu ndo yatakuwa msimamo wa JF.
1. Mwakinyo kusema kuwa kakataa kupigana kwasababu ya kubadilishiwa bondia dakika za mwisho ni uongo mtupu. Bondia anayetajwa kubadilishiwa alilipiwa kila kitu na Mwakinyo. Ina maana yeye ndo aliamua kujiletea mpinzani wake. Haya ni maajabu kwenye boxing ya Tanzania. Huyo bondia angepigwa tu atake asitake. Yaani kila kitu nimekulipia mimi bado unipige?
2. Kwenye huu mzozo promota Karigo kajitahidi sana kuwa professional ila kasoro yake kubwa ni kutokuwa na pesa. Ni promota njaa. Kwa melezo ya Karigo na Mwakinyo ni kuwa kuna baadhi ya gharama zililipwa na bondia Mwakinyo baada ya kuwa Promota kashindwa. Kwa mfano Karigo anasema mpinzani wa Mwakinyo aligharamiwa na Mwakinyo mwenyewe. Sasa kama mpinzani alilipiwa na Mwakinyo ina maana tayari kungekuwa na mgongano mkubwa wa kimaslahi. Kwangu mimi ni kama Mwakinyo alinunua ushindi.
3. Bado Mwakinyo ana akili ndogo sana za kibiashara na ana uswahili wa kipuuzi. Mwakinyo mwenyewe alikiri kuwa sababu nyingine iliyosababisha akakataa kupigana ni kuhusishwa kwa kampuni ya Mafia Promotions kwenye pambano lake. Kama nilivyosema mwanzoni ni kuwa promota Karigo hana pesa za kutosha ikabidi atafute kampuni nyingine washirikiane ndo akawapata hao Mafia. Mwakinyo akawakataa Mafia kwa kudai hao jamaa ana ugomvi wao binafsi. Hii ni sababu ya kipuuzi kwenye professionalism. Yaani uwe na ugomvi binafsi na watu wa kampuni ndo uichukie kampuni? Na hata baada ya Mafia kuamua kujiondoa bado Mwakinyo akataka mabondia wote walio chini ya kampuni ya Mafia waliotarajiwa kupigana mapambano ya ufunguzi waondolewe. HUU ULIKUWA NI UWENDAWAZIMU WA MWAKINYO.
4. Kitendo cha promota kutufichulia siri kuwa Mwakinyo huwa anajichagulia mabondia wa kupigana nao kimemvua nguo Mwakinyo na kuonekana huwa anashinda kimagumashi. Inatajwa kuwa Mwakinyo amekuwa akijichagulia mabondoa wadhaifu kwa maslahi yake binafsi.
5. Shirikisho la ngumi za kulipwa nalo haliwezi kuepuka lawama kwa kutochukua hatua kwa mambo mengi ya kijinga yanayochafua boxing.
Ninamshauri Mwakinyo aache janja janja na kufuata utaratibu. Anachofanya ni kujidanganya. Msimamo anaodai kuwa nao ni wa kijinga na hauwezi kumsaidia.