Mvua za kutengeneza (mvua za Lowassa)

Ngamanya Kitangalala

JF-Expert Member
Sep 24, 2012
501
1,214
Mwaka 2006, nchi yetu ilikubwa na ukame, nakumbuka waziri mkuu wa wakati huo Edward Lowassa, alikwenda nchini Thailand, kujaribu kufanya mazungumzo na serikali ya Thailand, ili walete wataalamu wao waje kuleta utaalamu wa KUTENGENEZA MVUA ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na ukame kwa wakati ule.

Nadhani ni wakati muafaka sasa, kwa serikali yetu hii ya awamu ya sita, pia kujaribu kulifanyia kazi wazo lile, hasa walati huu nchi yetu ikiwa inakabiliwa na upungufu wa mvua, ili waweze kuokoa wakulima ambao kimsingi wengi wao wanatengemea kilimo cha mvua.
 
Nakumbuka enzi za mh wazir mkuu PINDA alienda nchi za bara Asia huko kununua teknolojia ya kuzalisha mvua ile teknolojia imeishia wapi?

Maana wakati kama huu ingetufaa Sana kutokana na Hali ya ukame unaoendelea

Mh alitumia Kodi zetu kuifuata hii teknolojia tuna haki ya kumuuliza hii teknolojia imeishia wapi?
 
Naona mnataka kuchokoza nyuki waliotulia kwenye mzinga wao bila bughuza yoyote!
 
Daaah kwa kufukuliwa makabuli hivi Baba wa taifa anaweza fufuka kuja kuwatia bakora hao waliopiga hela
 
Back
Top Bottom