Mvomero, Morogoro: Waziri Bashungwa abaini upotevu wa shilingi milioni 231 ujenzi wa miundombinu Sekondari ya Kumbukumbu ya Sokoine

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,085
4,888
Watanzania hawa watendaji wetu sasa wamekuwa ni balaa. Upigaji wa fedha za miradi unatisha. Kila kukicha utasikia halmashauri hii imepiga, wilaya hii imepiga.

Mkandarasi huyu kapiga ilimradi ni vipigo wa fedha za miradi kwa urefu wa kamba. Wakati umefika kwa serikali isiishie kuwasimamisha kazi watendaji wanaokula kwa urefu wa kamba zao, Kinachotakiwa ni kuwafungulia mashtaka mahakamani na kuwafukuza kazi.

Angalia hapa Waziri wa Tamisemi analalamika juu ya upigaji wa fedha Mvomero. Ngoja tusubiri hatua zitakazochukuliwa sana sana ni kuunda tume na kuwahamisha wakale kwingine kwa urefu wa kamba zao.

======

Bashungwa Ubadhirifu milioni 231 Mvomero.jpg

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa amebaini upotevu wa fedha na matumizi yasiyosahihi ya kiasi cha shilingi milioni 231.84 katika ujenzi wa shule ya Sekondari ya kumbukumbu ya Sokoine kwa ajili ya ujenzi wa bwalo la chakula, miundombinu ya jiko na bweni.

Waziri Bashungwa amebaini hayo katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya Mvomero mkoani Morogoro na kumtaka Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Hassan Njama kutoa ufafanuzi wa fedha hizo.

“Nikiwa hapa shule ya Sekondari Sokoine nigependa kuona na kujiridhisha fedha zilizoletwa na Serikali Milioni 700 ambazo zilitakiwa kujenga bwalo la chakula, bweni na jiko kama zimetumika kulingana na mujibu wa BoQ” amaesema Bashungwa

Bashungwa amesema kutokana na tathmini iliyofanywa na Tume maalum ya ukaguzi wa matumizi ya fedha za ukamilishaji wa miundumbinu katika shule ya Sokoine imebaini upotevu, matumizi yasiyo sahihi ya shilingi milioni 231.84

Amefafanua kuwa kulingana na taarifa iliyotolewa gharama halisi ya kazi iliyofanyika ni shilingi milioni 468.15 zikilinganishwa na fedha zilizopokelewa milioni 700 hivyo ilitakiwa kiasi cha shilingi milioni 231. 84 kiwe kimebaki na kutaka kupata maelezo ya kina fedha hiyo nyingine ilipo.

Aidha, Wakati akikagua ujenzi wa jengo la huduma ya dharura katika Hospitali ya wilaya Mvomero hakuridhishwa na kuchelewa kwa kuanza ujenzi huo ambapo Serikali imeshatoa kiasi cha milioni 300 kutekeleza mradi huo na kumuagiza kuanza ujenzi ndani ya siku 7.
Vile vile, Bashungwa alikagua ujenzi wa wodi ya wazazi katika kituo cha afya Mlali ambayo imekamilika lakini haijaanza kutoa huduma na kumuagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI kusaidia upatikanaji wa vifaa, vitendanishi na vifaa tiba kwenye vituo va afya vilivyokamilisha ujenzi.
 
Viongozi wakuu wa Serikali kuanzia Rais, Wabunge na Madiwani walipatikana kwa rushwa.unategemea nani ataweza kusimamia kitu ambacho kimetokana nae.

Ndio maana wengine tulimuona Magufuli kama Muigizaji,sababu nae alikuwa zao la rushwa na mula rushwa,still akawa anakemea wala rushwa-yalikuwa maajabu ya Dunia.

The only way tukitaka kukomesha rushwa tuanze katika upatikanaji wa Viongozi wakubwa kama Rais,tuhakikishe hawapatikani kwa rushwa.
 
Viongozi wakuu wa Serikali kuanzia Rais, Wabunge na Madiwani walipatikana kwa rushwa.unategemea nani ataweza kusimamia kitu ambacho kimetokana nae.

Ndio maana wengine tulimuona Magufuli kama Muigizaji,sababu nae alikuwa zao la rushwa na mula rushwa,still akawa anakemea wala rushwa-yalikuwa maajabu ya Dunia.

The only way tukitaka kukomesha rushwa tuanze katika upatikanaji wa Viongozi wakubwa kama Rais,tuhakikishe hawapatikani kwa rushwa.
Naomba msaada uniambie Magufuli alikula rushwa gani?
 
Huko ndio kwenye pesa, mradi wa halamashauri,bei za vifaa zinaongezwa Cha juu, mkandarasi analipwa fasta, Cha juu kinachukuliwa, na vifaa vinanunuliwa kwenye duka la ofisa wa serikali,
 
Tanzania Bara itazidi kuchakaaa, hakuna maendeleo yoyote ya kiuchumi na vitu yatakayopatikana kwa sasa.

Viongozi wapo Dar hawana habari na yoyote yanayoendelea kuanzia Chalinze kuja huku kwetu mikoani.

Watu ni kushinda kula kwa ushirikiano, ili ilikija bumburuka wanasaidiana.
 
Naomba msaada uniambie Magufuli alikula rushwa gani?
Huyo Jamaa ana chuki sana na JPM, hajui hata kwenye zile 5 bora za mchujo wa Wagombea wa Urais ulimptitisha Magufuli sababu ni yeye ndiye aliyeonekana hana kashfa zaidi za rushwa kuliko wenziye?

Chuki ni laana na zinawatesa sana Watu, yani hadi Mtu kashakuwa Hayati lakini bado tu Watu hai wanateseka naye, usikute kama si vyeti feki, itakuwa alitumbuliwa kazini au kubananishwa kwenye kodi nakati kabla ya JPM alishazoea biashara za magendo.
 
Pesa ya chai hiyo nikajua bil.kadhaa
Pesa si inategemea na gharama ya mradi. Mradi wa mil 500, utakulaje bil kadhaa?

Vyovyote vile Kama pesa imeliwa basi wawajibishwe na Sheria ifate mkondo, hiyo ndio serikali inavyotakjwa na hata mama Samia alilisema hilo
 
Kwanini walipeka kiasi kilichozidi?? kwa hiyo mln 700 ilienda pale bila maelekezo inatakiwa kufanya nini?
 
Pesa si inategemea na gharama ya mradi. Mradi wa mil 500, utakulaje bil kadhaa?

Vyovyote vile Kama pesa imeliwa basi wawajibishwe na Sheria ifate mkondo, hiyo ndio serikali inavyotakjwa na hata mama Samia alilisema hilo
Ndio maana nasema practically haiwezekani pesa nusu ipigwe
 
Back
Top Bottom