mcubic
JF-Expert Member
- Mar 3, 2011
- 10,307
- 6,514
Wimbo Muziki wa Darassa umekuwa mkubwa sana kwa sasa. Kila kona unaimbwa, unapigwa, unaburudisha. Unakonga nyoyo za wengi.
Katika soko la muziki Tanzania, Muziki ndiyo band wagon, maana ni wimbo unaovuta mkumbo wa wengi. Watu wanaupenda tu. Wanaupenda sana.
Muziki ni wimbo ambao unaburudisha sana. Mapigo yake ya muziki, Darassa ameichezea beat vizuri, ufundi wa Ben Pol umeonekana. Ni wimbo wenye ladha kwa asilimia 100.
Hata hivyo, Muziki ni wimbo wa msimu. Huwezi kutaraji kuwa baada ya kuchokwa sasa, utaendelea kupendwa nyakati zijazo. Nyimbo za msimu hutikisa kwa wakati wake, zikishachokwa hukosa mvuto kabisa.
Nyimbo za msimu kama ulivyo Muziki, hufanana na Big G. Mwanzoni unakuwa mtamu sana. Ila ule utamu ukishaisha ile ladha yote ya Big G hutoweka, mtu anaweza kubaki anaitafuna tu kuchangamsha meno lakini huwa haina mvuto wowote mdomoni.
Muziki wa msimu ukishachokwa, hata kama baadaye utapigwa itakuwa kujifurahisha tu lakini huwa hauna nguvu kama uliokuwa nao mwanzoni.
Kuna vitu vinne husababisha wimbo uishi kwa muda mrefu. Vitu hivyo ni mapigo ya muziki, mvuto wake una upekee wa kiasi gani? Sauti ya uimbaji (melody), inavuta kiasi gani? Ubunifu wa maneno na kitu cha nne ni ujumbe wake, je, unaigusa jamii kwa kiasi gani?
Ufanyie tathmini Muziki
Muziki wa Darassa ukiachana na mdundo wake, ubunifu wa maneno kusema kuwa kuna upekee ambao unaweza ukaufanya wimbo huo kuishi kwa muda mrefu ni upi? Maneno ya wimbo Muziki ni ya kawaida sana.
Melody ni ya kawaida, mtindo wake wa kutambaa kwenye beat ni mwepesi. Kiitikio kipo kawaida. Mapigo ya muziki yanaubeba wimbo kwa sehemu kubwa. Kama Darassa angeimba Muziki nje ya mdundo wake, watu wasingetarajia ungekuwa wimbo mkubwa kama unavyobamba kwa sasa.
Ukienda kwenye point ya ujumbe hapo ndiyo hakuna kitu kabisa. Darassa alichofanya ni kucheza na maneno, kulazimisha vina, kiasi kwamba kutoka mstari mmoja mpaka mwingine anachoimba vinatofautiana kabisa, ingawa anachoimba kinaeleweka.
Hakuna ubunifu katika ujumbe ndani ya Muziki wa Darassa. Ukifananisha nyimbo, wimbo Too Much wa Darassa ni mkubwa kuliko Muziki. Huwezi kuuchoka kuusikiliza na utaendelea kuishi kwa muda mrefu ujao.
Ndani ya Too Much mdundo mzuri, mtindo aliotumia kuteleza kwenye beat upo sawasawa na ujumbe upo murua. Too Much ni zaidi ya Muziki kwa sababu ndani yake kuna ujumbe na ladha. Katika Muziki ni ladha kwa kwenda mbele.
Too Much ni wimbo ambao unaweza kumwamsha mtu mwenye kusakamwa na watu kwa sababu unafikisha ujumbe ndani ya fikra zake. Too Much majungu, longolongo, maadui na marafiki hawaeleweki, mapichapicha mengi tu.
Mvua jua vyote watu hawataki yaani ni Too Much. Unashindwa kuelewa watu wanataka nini. Mtu mpaka unashindwa kunywa maji. Washakaji ukigeuka ndiyo wauaji. Ujumbe wa Too Much umenyooka na utaendelea kuishi kwa watu wa jamii zote. Wakulima, wafanyabiashara, matajiri na maskini, Too Much za Darssa zinawagusa.
Hata Kama Utanipenda wa Darassa ambao ameimba kwa kumshirikisha Rich Mavoko ni wimbo ambao utakuwa na maisha marefu. Ndiyo maana hata baada ya kuachia nyimbo nyingine, bado Too Much na Kama Utanipenda bado zinapata nafasi ya kupenya kwenye frequency.
Naweza kutabiri; Siku Darassa atatoa wimbo mzuri, itakuwa rahisi kuuzika Muziki jumla na Wabongo pamoja na kwingineko ambako wimbo huo umepenya, hawatakuwa na kipya cha kuwakumbusha zaidi ya maneno kuwa Muziki uliwahi kutamba.
Jambo la kueleweka
Muziki siyo wimbo mbaya, ni mzuri sana kwa biashara ya msimu. Unabamba na kila eno ukisikika unawakuna watu. Kumbi za starehe watu wanaburudishwa na Muziki, redio na televisheni zinavuna watazamaji wengi kwa sababu ya Muziki, katika vyombo vya usafiri, Muziki unapunguza uchovu wa safari.
Haishangazi hata sasa Darassa kuvuna watazamaji wengi YouTube na kuuza sana wimbo kupitia miito ya simu (Ring Back Tunes-RBT) kupitia Muziki. Acha atengeneze pesa kupitia maonesho ya muziki.
Jambo ambalo Darassa anapaswa kufanya ni kujiandaa mapema. Anapaswa kuandaa wimbo mkubwa ambao atapaswa kuuachia mara tu Muziki utakapoanza kuchokwa, maana ukishachokwa hautahitajika kabisa kutokana na sababu ambazo nimeshazieleza.
Angalizo ambalo anapaswa kuwa nalo ni wakati wa kuachia wimbo mpya. Kipindi hiki ambacho Muziki bado upo kwenye reli yake na hauonekani wimbo wa kuutoa sokoni, akithubutu kutoa wimbo mwingine anaweza kuuharibu, maana utafichwa na Muziki utaendelea kutamba.
Hiyo ndiyo changamoto ya kuwa na wimbo mkubwa ambao nguvu yake kubwa inabebwa na upepo wa msimu. Anapaswa kutulia kweli na kuchungulia soko kabla hajaachia mzigo mwingine, vinginevyo anaweza kujimaliza kibiashara wakati sasa ndiyo yupo kwenye kipindi kizuri cha kufaidi uvumilivu wake muda mrefu kwenye soko la muziki wa Kibongo.
Asichopaswa kusahau
Dume Suruali wa FA ni mkubwa na utaishi kwa miaka mingi ijayo kutokana na ujumbe wake pamoja na vigezo vingine vinavyofanya muziki uishi ambavyo nilishavieleza hapo kabla.
Kajiandae wa Ali Kiba na Ommy Dimpoz upo sawasawa na una maisha marefu. Kokoro wa Rich Mavoko aliomshirikisha Diamond Platnumz ni kubwa pia lakini zinapepesuka kila zikikutanishwa na Muziki. Hiyo ni kazi ya msimu.
Zipo nyimbo nyingi tu ambazo zinapepesuka kila zikilinganishwa na Muziki. Usije kushangaa hata Marry You ya Diamond Platnumz aliomshirikisha Ne-Yo ukapwaya mbele ya Muziki, wakati Marry You ni wimbo mzuri na wenye viwango vya kimataifa.
CHANZO: MAANDISHI GENIUS