Nifah
JF-Expert Member
- Feb 12, 2014
- 33,220
- 74,902
Kama mnakumbuka vyema, Novemba ya mwaka jana niliwaletea hapa taarifa kuhusiana na aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi Maisha Magic Bongo, Barbara Kambogi kusimamishwa kazi kwa tuhuma zilizowasilishwa makao makuu ya DSTV Afrika ya Kusini na mtayarishaji wa tamthilia za Kiswahili Bwana Isike Samwel.
Baada ya tuhuma hizo zenye ushahidi usio na shaka, DSTV walimsimamisha kazi Barbara Kambogi na msaidizi wake kupisha uchunguzi na hivi sasa umefanyika uteuzi wa Mkurugenzi mpya, Bibie Mwangaza Mollel.
CV yake huko DSTV imeshiba kwelikweli!
Kwa taarifa za kiutendaji imefahamika kwamba uteuzi huu ni makini. Mwangaza amefanya kazi DSTV kwa kipindi kisichopungua miaka 10!
Alianza kufanya kazi kitengo cha huduma kwa wateja kuanzia mwaka 2014 alikohudumu kwa miaka 7, kisha akahamishiwa kitengo cha masoko na baadaye akawa mwendeshaji wa ofisi ya DSTV hadi alipoukwaa Ukurugenzi wa kitengo cha tamthilia za Kiswahili hivi karibuni.
Ni mchapakazi hodari!
Mwangaza anafahamika kwa uchapaji kazi wake usio na mashaka. Hilo linadhihirika kwa tuzo aliyopokea mwaka juzi kwenye kitengo hichohicho cha tamthilia za Kiswahili.
Hongera Mwangaza, matumaini yetu tulio wengi ni juu yako kuona ukifanya tofauti na wenzio Barbara pamoja na msaidizi wake waliogeuka Miungu watu katika kitengo hichohicho ulichoteuliwa.
Kila la kheri
Mwangaza Evarest Mollel pichani…
Hii ni taarifa mpya, DSTV watatangaza kuhusu uteuzi huo hivi karibuni.
Chanzo changu nyeti, nami ndiye
Nifah.