Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,832
- 13,588
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 13, Kikao cha 2, leo Novemba 1, 2023 ambapo Muswada wa sheria ya Bima ya Afya kwa wote wa Mwaka 2023 unasomwa.
====
MAELEZO YA MHESHIMIWA UMMY ALLY MWALIMU (MB), WAZIRI WA AFYA AKIWASILISHA MUSWADA WA KUTUNGA SHERIA YA BIMA YA AFYA KWA WOTE NA.8 WA MWAKA 2022
KATIKA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAREHE 01 NOVEMBA 2023
MAELEZO YA MHESHIMIWA UMMY ALLY MWALIMU (MB), WAZIRI WA AFYA AKIWASILISHA MUSWADA WA KUTUNGA SHERIA YA BIMA YA AFYA KWA WOTE NA.8 WA MWAKA 2022
KATIKA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA TAREHE 01 NOVEMBA 2023
Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naomba nianze kwa kumshukuruMwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kuniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha maelezo kuhusu Muswada wa kutunga Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote (Na.8) wa Mwaka 2022.
Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekee naomba uniruhusu nitoeshukrani zangu za dhati kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais waJamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wake mahiri na shupavukwa nchi yetu katika Nyanja zote. Sisi katika sekta ya Afya tunajivuniamageuzi makubwa anayofanya katika kuhakikisha huduma za afyazinapatikana kwa watanzania wote bila vikwazo vyovyote. Vilevile,ameendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika kuboresha huduma za afyanchini hususani katika ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya kutoleahuduma za afya, ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa vya uchunguzi na kutibumagonjwa, kuongeza bajeti kwa ajili ya ununuzi wa dawa na bidhaa nyingineza afya na kuimarisha upatikanaji wa wataalam wa afya katika ngazi zote.Hakika jitihada za Rais Samia zinaonekana katika maeneo mbalimbali ya nchiyetu. Kipekee tunampongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihadazake alizozianzisha mwaka 2018 ambazo zimewezesha nchi yetu kupunguzaVifo vya Watoto wa umri chini na miaka mitano kwa asilimia 35 kutoka vifo 67kwa kila vizazi hai 1,000 mwaka 2016 hadi vifo 43 kwa kila vizazi hai 1,000mwaka 2022. Aidha, Vifo vitokanavyo na uzazi vimepungua kwa asilimia 80kutoka vifo 530 katika kila vizazi hadi 100,000 mwaka 2016 hadi vifo 104katika kila vizazi hai 100,000 mwaka 2022. Hakika hii ni rekodi ya kutukukakwa nchi yetu. Vilevile, nawapongeza Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. KassimMajaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniakwa kumsaidia vyema Mheshimiwa Rais katika kuwaletea maendeleowananchi wa Tanzania. Aidha, nichukue fursa hii kumpongeza Mhe. Dkt.Dotto Mashaka Biteko (Mb) kwa kuaminiwa na kuteuliwa kuwa Naibu WaziriMkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati.
Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza wewe binafsi,kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa 31 wa Mabunge Duniani (InterParliamentary Union) na Rais wa kwanza mwanamke kutoka Bara laAfrika kushika wadhifa huo. Hii ni fahari na heshima kubwa kwa nchi yetukwani inaonesha ukuaji wa diplomasia na kielelezo cha imani kubwa ambayomataifa mengi Duniani wanayo juu ya nchi yetu na wewe mwenyewe.
Mheshimiwa Spika, niendelee kukupongeza kwa kuongoza vyema Bungeletu na kusimamia vikao na mijadala ndani ya Bunge letu kwa umahiri na kwakuzingatia Sheria na Kanuni zinazoliongoza Bunge hili. Aidha, nawapongezaMheshimiwa Naibu Spika na Waheshimiwa Wenyeviti wa Bunge kwakukusaidia vyema katika kuliendesha Bunge letu. Vilevile, ninawapongezaWaheshimiwa Wabunge wote kwa kuendelea kutekeleza ipasavyo wajibu waowa Kikatiba wa kutunga Sheria pamoja na kuisimamia Serikali.
Mheshimiwa Spika, nimalizie shukrani zangu kwa kuishukuru sana Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI inayoongozwa na Mhe.Stanslaus Haroon Nyongo - Mwenyekiti wa Kamati, na Mhe. Dkt. FaustineEngelbert Ndungulile - Makamu Mwenyekiti, kwa ushirikiano na ushaurimzuri waliotupatia wakati wa kupitia Muswada huu mbele ya Kamati hiyo.Kamati hii ilifanya kazi kubwa ya kuchambua Muswada huu kwa makini,weledi na umahiri mkubwa na kusikiliza na kuchambua maoniyaliyowasilishwa na wadau mbalimbali walioitwa mbele ya Kamati hiyo nakuishauri Serikali kuboresha Muswada huu.
Mheshimiwa Spika, kabla ya kuanza kuwasilisha Muswada wa Sheria yaBima ya Afya kwa Wote, naomba kutoa Chimbuko la kuandaliwa kwaMuswada huu wa Bima ya Afya kwa Wote kuwa ni kutimiza wajibu wa Serikaliwa Kikatiba wa kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora za afyabila vikwazo. Aidha, kuwasilishwa kwa Muswada huu ni Utekelezaji waMaelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi, Ibara ya 83 (e)inayotaka kuimarishwa kwa mfumo wa Bima ya Afya nchini ili kufikia lengo lakuwa na bima ya afya kwa wananchi wote.
Mheshimiwa Spika, Bima ya Afya kwa Wote ni sehemu ya kufikia malengoya Huduma za Afya kwa Wote (Universal Health Coverage). Dhana yahuduma za afya kwa wote imejengeka katika Tamko la Haki za Binadamu laUmoja wa Mataifa la mwaka 1948; Katiba ya Shirika la Afya Duniani (WHO)ya mwaka 1948; na kuwekewa viwango vya Kimataifa katika Mkataba waShirika la Kazi Duniani (ILO) Na. 102 wa mwaka 1952 pamoja na pendekezoNa. 202 kuhusu hifadhi ya jamii la mwaka 2012. Pia, Azimio la Alma Ata lamwaka 1978 (Alma- Ata Declaration of 1978) ambalo limeeleza wazi kwamba,upatikanaji wa huduma za afya ya msingi na yenye ubora ni haki ya kila mtu.Dhana ya Huduma za Afya kwa Wote imejengeka katika nguzo kuu tatuambazo ni; uwezo wa kuwafikishia wananchi huduma za afya, upatikanaji wahuduma bora za afya na mfumo madhubuti wa ugharamiaji wa huduma zaafya bila kikwazo cha fedha.
Mheshimiwa Spika, Tangu uhuru Serikali za awamu zote sita zimewekezakatika sekta ya afya kwa kiasi kikubwa ili kuwezesha wananchi wengi kuzifikiahuduma za afya ambapo kwa sasa huduma zinapatikana kuanzia ngazi yaZahanati, Vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya/Halmashauri, Hospital za Rufaaza Mikoa, Hospital za Rufaa za Kanda, Hospital Maalum na Hospitali ya Taifa.Kutokana na uwekezaji huo, upatikanaji wa huduma za afya nchiniumeendelea kumeimarika kuanzia ngazi ya msingi, kati na huduma zakibingwa na ubingwa bobezi pamoja na kuchochea tiba utalii.
Mheshimiwa Spika, Mfumo wa ugharamiaji huduma za afya ulianza na Seraya Serikali ya huduma bila malipo mwaka 1960 hadi mwaka 1990 ambapoutaratibu wa wananchi kuchangia huduma za afya ulianza kutumika. Utaratibuhuu ulikua na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na wananchi wengikukosa huduma za afya kutokana na kukosa fedha za kugharamia matibabupapo kwa papo. Aidha utaratibu huu unawaingiza wananchi wengi hususaniwasio na uwezo katika umaskini kutokana na gharama kubwa za matibabu.Kutokana na changamoto hizo, kuanzia mwaka 2000 Serikali ilianzishautaratibu wa bima ya afya kwa Mifuko ya bima ya afya ya Umma na Kampunibinafsi za bima ya afya. Hata hivyo, bado wananchi wengi takribani asilimia85 wapo nje ya utaratibu huo kutokana na uhiari wa kujiunga na Bima za afya.Takwimu zinaonyesha kuwa hadi kufikia Septemba 2023 ni asilimia 15.3 tu yawananchi wote ndio wapo katika mfumo wa bima ya afya (NHIF 8%; CHF 6%,NSSF-SHIB 0.3% na Bima Binafsi 1%). Hivyo, Muswada ninaouwasilishaunalenga kuimarisha mfumo wa ugharamiaji huduma za afya kupitia bima yaafya kwa wote ili kufikia lengo la huduma bora za afya kwa wote.
Mheshimiwa Spika, sasa naomba kuwasilisha mbele ya Bunge lako TukufuMuswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote wa Mwaka 2022. Lengo lakutungwa kwa Sheria inayopendekezwa ni kuhakikisha upatikanaji wahuduma bora za afya kwa wote kupitia mfumo wa bima ya afya na kuwekamfumo wa ushiriki katika skimu za bima ya afya kwa raia na wakazi wote.Utaratibu unaopendekezwa utawezesha mwananchi kupata huduma za afyabila kikwazo cha fedha pindi anapohitaji huduma hizo na kumwezeshakushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo na hivyo kumuepushamwananchi kuingia katika janga la umaskini.
Mheshimiwa Spika, Muswada huu umegawanyika katika Sehemu Tisa.Sehemu ya Kwanza inahusu masharti ya utangulizi ambapo Kifungu chaKwanza kinahusu Jina na kuanza kutumika kwa Sheria. Kifungu hiki kimempaWaziri Mamlaka ya kubainisha tarehe za kuanza kutumika kwa Vifungumbalimbali vya Sheria ili kutekeleza mfumo wa Bima ya Afya kwa wote.Kifungu cha Pili kinaainisha mipaka ya matumizi ya Sheria hii.
Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 3 kinaweka masharti kuhusu tafsiri yamisamiati mbalimbali iliyotumika katika Sheria kwa lengo la kuweka maanailiyokusudiwa na kuondoa utata wa tafsiri unaoweza kujitokeza katikautekelezaji wa Sheria hii. Aidha, Serikali inapendekeza kifungu hichokifanyiwe marekebisho kwa kuondoa na kuongeza misamiati kamainavyobainishwa katika Aya C ya Jedwali la Marekebisho. Kifungu cha 4kimeainisha Malengo ya Sheria hii ambayo ni kuhakikisha upatikanaji wahuduma bora za afya kwa wote. Lengo la kifungu hiki ni kuweka misingi yakuzingatiwa wakati wa usimamizi na utekelezaji wa Sheria hii.
Mheshimiwa Spika, Sehemu ya Pili inaweka masharti kuhusu Mfumo wa Bima ya Afya kwa Wote. Kifungu cha 5 kinaweka wajibu wa ushiriki wa kila mtu katika Mfumo wa Bima ya Afya. Aidha, Serikali inapendekeza kufanyamarekebisho katika kifungu hiki kwa lengo la kuweka ulazima wa kila mtukujiunga na Bima ya Afya kama inavyoainishwa katika Aya D ya Jedwali laMarekebisho. Kifungu cha 6 kinapendekeza kuanzisha Mfumo wa Bima yaAfya kwa Wote ambapo makundi mbalimbali yatajumuishwa na kushirikikatika Skimu za Bima ya Afya. Makundi hayo ni pamoja na Waajiri, Watumishiwa Umma, Wafanyakazi walioajiriwa katika sekta binafsi, waliojiajiri wenyewekatika sekta isiyo rasmi na wananchi wasio na uwezo. Washiriki wenginekatika mfumo wa bima ya afya ni skimu za bima ya afya, vituo vya kutoleahuduma za afya na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TanzaniaInsurance Regulatory Agency - TIRA).
Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 7 kinaainisha majukumu ya Mamlaka yaUsimamizi wa Bima Tanzania (Tanzania Insurance Regulatory Authority-TIRA) katika kudhibiti na kusimamia mfumo wa bima ya afya nchini. Kwamujibu wa kifungu hiki, Mamlaka hiyo, pamoja na mambo mengine, itakuwana wajibu wa kusajili na kudhibiti skimu za bima ya afya; kuhakikisha kuwakila skimu ya bima ya afya inatoa kitita cha mafao ya huduma muhimu(Standard Benefit Package) kwa mujibu wa Sheria hii; na kutoa miongozokuhusiana na uendeshaji wenye tija na ufanisi wa shughuli za skimu za bimaya afya. Lengo la usimamizi na udhibiti wa bima ya afya ni kuhakikisha
ufanisi wa utoaji wa huduma za bima ya afya. Serikali inapendekezamarekebisho katika kifungu hiki kama ilivyoainishwa katika Aya E ya Jedwali la Marekebisho.
Mheshimiwa Spika, Sehemu ya Tatu inaweka masharti kuhusiana na skimu za bima ya afya. Kifungu cha 8 kinatambua uwepo wa Mfuko wa Taifa waBima ya Afya kama skimu ya bima ya afya ya umma. Aidha, kifungu hikikimempa mamlaka Waziri kuboresha skimu ya bima ya afya ya umma. Lengola kifungu hiki ni kuendelea kuboresha huduma za bima ya afya katika skimuya bima ya afya ya Umma kwa kuzingatia matokeo ya tafiti na tathminimbalimbali.
Mheshimiwa Spika, kifungu cha 9 kinaweka utaratibu wa kampuni binafsikusajiliwa kama skimu za bima ya afya binafsi baada ya kutimiza vigezo namasharti yatakayoainishwa katika Kanuni zitakazotungwa chini ya Sheriainayopendekezwa. Dhumuni la kifungu hiki ni kuwawezesha wananchi kuwana uhuru wa kuchagua aina ya Skimu ambazo watapenda ziwahudumie nakupanua wigo wa uwepo wa skimu za bima ya afya ili kuongeza fursa yaushiriki kwa lengo la kukuza ushindani na kuongeza ufanisi wa utoaji wahuduma za Bima ya Afya nchini.
Mheshimiwa Spika, Serikali inapendekeza kufutwa kwa kifungu cha 10kama inavyoonekana katika Aya F ya jedwali la marekebisho.
Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 11 kinaweka katazo la uendeshaji waskimu za bima ya afya bila kusajiliwa. Lengo ni kuhakikisha kuwa skimu zoteza bima ya afya za umma na binafsi nchini zinasajiliwa na kuendeshwa kwamujibu wa Sheria inayopendekezwa. Kifungu cha 12 kinaipa Mamlaka yaUsimamizi wa Bima jukumu la kutunza Rejesta ya Skimu za Bima ya Afyazilizosajiliwa chini ya Sheria inayopendekezwa ili kuwezesha uratibu nausimamizi wa Skimu hizo.
Aidha, Kifungu cha 13 kinaweka utaratibu ambao Mamlaka ya Usimamizi wa Bima itaufuata ikiwa inataka kufuta usajili wa skimu ya bima ya afya na hatuazitakazochukuliwa iwapo skimu ya bima ya afya itataka kujiondoa katika utoajiwa huduma za bima ya afya. Dhumuni la kifungu hiki ni kuhakikisha kuwawatoa huduma za bima ya afya wanafuata utaratibu wa kujiondoa aukuondolewa katika shughuli ya utoaji wa huduma za bima ya afya ili kulindahaki na maslahi ya wanachama na watoa huduma za afya. Aidha, Serikalikatika Aya G ya Jedwali la Marekebisho inapendekeza kufanya marekebishokatika kifungu hiki kwa kuongeza utaratibu wa kuzingatiwa kabla ya skimu yabima ya afya kufutiwa usajili kwa lengo la kulinda maslahi ya wanachama nawatoa huduma za afya.
Mheshimiwa Spika, Sehemu ya Nne inaweka masharti kuhusu vitita vyamafao. Kifungu cha 14 kinaweka ulazima kwa skimu za bima ya afya kutoakitita cha mafao ya huduma muhimu (Standard Benefit Package) kwawanufaika. Aidha, kifungu hiki kinatoa fursa kwa wanachama kupata kitita chamafao ya ziada kinachojumuisha huduma zaidi ya zilizomo katika kitita chamafao ya huduma muhimu. Lengo la kifungu hiki ni kuhakikisha kuwa kilamwanachama anapata huduma za kitita cha mafao ya huduma muhimu kwausawa, na kutoa fursa ya upatikanaji wa huduma za ziada pale ambapomwanachama atahitaji. Serikali inapendekeza kufanya marekebisho katikakifungu hiki kama inavyobainishwa katika Aya I ya Jedwali la Marekebisho.
Mheshimiwa Spika, Kama ilivyoainishwa katika Aya J ya Jedwali lamarekebisho, Kifungu cha 15 kimefutwa na kuandikwa upya kwa kuainishahuduma za afya zilizojumuishwa katika kitita cha mafao ya huduma muhimu.Vilevile, kifungu hiki kinampa Waziri mamlaka ya kufanya marekebisho yakitita hicho kwa kuzingatia matokeo ya tathmini na uendelevu wa Skimu zabima ya afya. Dhumuni la kifungu hiki ni kuhakikisha upatikanaji wa hudumamuhimu za afya kwa wanachama wote.
Mheshimiwa Spika, katika kufikia lengo la Bima ya Afya kwa Woe na kwa kutambua uzoefu na uwekezaji uliofanywa na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF),Serikali inapendekeza kufanya marekebisho kama inavyobainishwa katikaAya K ya Jedwali la marekebisho kwa kuanzisha kitita cha bima ya afyacha jamii (Community Health Insurance Package – CHIP) ikiwa ni mpangombadala wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambapo Sheria iliyoanzishaMfuko huo inapendekezwa kufutwa na kuianzisha upya chini ya sheria hii.Lengo la kuanzishwa kwa kitita hicho ni kuhakikisha wananchi wotewanajumuishwa katika utaratibu wa bima ya afya ili kupata huduma bora zaafya pasipo vikwazo wanavyokutana navyo sasa. Vikwazo hivyo ni pamojana: (i) Wananchi kutopata huduma za afya wanapokuwa nje ya maeneowaliyojiandikisha na hivyo kulazimu kulipia huduma za afya kwa utaratibu wapapo kwa papo hali inayoathiri shughuli za kijamii na kiuchumi; (ii) Wigomdogo wa kuchangiana kati ya Mikoa na Halmashauri zenye uchumi mkubwana mdogo, wananchi wenye kipato kikubwa na kidogo na wagonjwa na wasiowagonjwa kutokana na kusimamiwa katika ngazi za Mamlaka za Serikali zaMitaa; (iii) Ufinyu wa huduma katika kitita cha mafao kinachotolewa na hivyokukosekana kwa huduma muhimu mathalani huduma za afya ya kinywa nameno, kutojumuishwa kwa baadhi ya dawa na hivyo kumlazimu mwanachamakulipia (iv) Muundo wa CHF kutokidhi misingi na kanuni za uendeshaji wabima ya afya mathalani kutotenganisha kwa majukumu kati ya mnunuzi namtoa huduma za afya; na (v) Uhiari wa wananchi kujiunga unaosababishawananchi kujiunga wakiwa wagonjwa.
Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 16 kinaweka utaratibu wa utoaji wa kitita cha mafao ya ziada kama itakavyoidhinishwa na Mamlaka ya Usimamizi waBima kwa kuzingatia uhitaji. Serikali inapendekeza kufanya marekebishokupitia Aya M ya Jedwali la marekebisho kwa kufuta Kifungu cha 17 namaudhui ya kifungu hicho kuwekwa katika kifungu kipya kamainavyobainishwa katika Aya N ya Jedwali la marekebisho. Lengo la kifunguhiki ni kutoa wigo wa upatikanaji wa huduma za afya kwa vituo vyote vyakutolea huduma za afya vilivyoingia mkataba na skimu za bima ya afya kwalengo la kuhakikisha wanufaika wanapata huduma kwa utaratibuutakaowekwa.
Mheshimiwa Spika, Sehemu ya Tano inaweka masharti kuhusu uanachamana uchangiaji katika skimu za bima ya afya. Kifungu cha 18 kinaainisha watuwanaopaswa kujiunga na skimu za bima ya afya na kuweka wajibu wa kilamtu kujiunga. Kifungu cha 19 kinabainisha aina na idadi ya watu wanaowezakujumuishwa katika skimu za bima ya afya kama wategemezi wamwanachama mchangiaji. Kifungu cha 20 kinaweka utaratibu wa usajili wawanachama ambapo waajiri katika sekta za umma na binafsi watatakiwakuwasajili waajiriwa wao ndani ya siku 30 toka kuanza kwa mkataba wa ajira.Aidha, kila mtu katika sekta rasmi na isiyo rasmi atatakiwa kujiunga na skimuya bima ya afya kwa utaratibu utakaoainishwa katika kanuni.
Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 21 kinaweka viwango vya uchangiaji kwawanachama kutoka sekta ya umma, sekta rasmi binafsi na sekta isiyo rasmi.Serikali inapendekeza kufanya marekebisho katika Kifungu hiki kwakubainisha kuwa mchango wa asilimia sita wa mshahara utakuwa kwa ajili yamwajiri wa sekta ya umma na mwajiri wa sekta rasmi binafsi atakayechaguakuwasajili waajiriwa wake katika skimu ya bima ya afya ya umma kamailivyoainishwa katika mapendekezo ya mabadiliko katika Aya O ya Jedwali lamarekebisho. Kwa muktadha wa Sheria hii mshahara wa sekta ya Ummana sekta rasmi binafsi, umetafsiriwa kwa maana sawa na ile inayotumikana mifuko ya hifadhi ya jamii kwa sekta zote mbili mtawalia. Dhumuni lakifungu hiki ni kuwa na maana zinazofanana na kuhakikisha uwepo wauwiano katika uchangiaji wa Kitita cha mafao ya Huduma Muhimu. Vilevile,Serikali inapendekeza kufanya marekebisho katika kifungu hiki kwa kutoauhuru kwa waajiri wa sekta rasmi binafsi kuchagua skimu ya bima ya afya yaumma au binafsi kuwasajili waajiriwa wao.
Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 22 kinaweka utaratibu wa utambuzi nausajili wa kundi la watu wasio na uwezo kwa lengo la kuhakikisha wanapatahuduma za afya bila kikwazo cha fedha kwa utaratibu utakaowekwa naSerikali, ambapo kundi hili litajumuishwa chini ya skimu ya bima ya afya yaUmma kwa namna itakavyoainishwa kwenye kanuni. Aidha, Serikaliinapendekeza kufanya marekebisho ya kifungu hiki kama inavyobainishwakatika Aya P ya Jedwali la marekebisho. Ili kuhakikisha upatikanaji wahuduma za afya kwa kundi hilo, Serikali inapendekeza kuanzishwa Mfuko wenye lengo la kugharamia bima ya afya kwa watu wasio na uwezo. Aidha,Mfuko utaweza kutumika kugharamia huduma za matibabu kwa magonjwasugu na ya muda mrefu kama vile saratani na magonjwa ya figo na hudumaza dharura zitokanazo na ajali kama inavyobainishwa katika Aya Q.
Vyanzovya Mfuko huo ni pamoja na sehemu ya mapato yatokanayo na ushuru wabidhaa kwenye vinywaji vyenye kaboni (carbonated drinks), Vinywaji vikali(Liqour), bidhaa za vipodozi (Cosmetic Products), Kodi ya michezo yakubahatisha, Ada ya bima za vyombo vya moto na mapato yatokanayo naushuru wa miamala ya kielektroniki (Eletronic Transaction Levy) kwa kadriitakavyopendekezwa na Waziri mwenye dhamana na masuala ya fedha,fedha zitakazotengwa na Bunge, mapato yatokanayo na uwekezaji wa mfuko;na zawadi na misaada kutoka kwa wadau mbalimbali.
Kipekee nitumie fursa hii kumshukuru na kumpongeza kwa dhati Rais waJamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwauwamuzi wake wa kuhakikisha kuwa watu wasio na uwezo wanapata hudumabora za afya bila kikwazo chochote, hakika historia ya Tanzania na Dunia itamkumbuka.
Mheshimiwa Spika, Kipekee tunaishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge yaAfya na masuala ya UKIMWI, kwa kuweka msisitizo wa umuhimu wa kuwa naMfuko kwa ajili ya kugharamia bima ya afya kwa watu wasio na uwezo. Hilitutalisimamia kikamilifu kwa kuwa ni wajibu wa Serikali kuhakikisha wananchiwasio na uwezo wanapata huduma bora za afya. Katika kuwatambua watuwasio na uwezo mapendekezo ya Serikali ni kuboresha mifumo ya utambuziwa watu kwa kutumia Mamlaka zilizopo. Takwimu za Utafiti wa Mapato naMatumizi ya Kaya Binafsi (Household Budget Survey – HBS) wa mwaka2017/18 zinaonyesha kuwa asilimia 26.4 ya watu wote Tanzania Bara niwananchi wasio na uwezo. Kwa kuzingatia utafiti huo asilimia 26.4 ya takwimuza Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 (59,851,347) idadi wawananchi wasio na uwezo ni 15,800,756 sawa na kaya 3,637,121. Aidhawananchi wasio na uwezo na ambao wanaishi katika umaskini uliokithiri ni4,044,843 ambao ni asiliia 8 sawa na kaya 1,113,513.
Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 23 kinaweka sharti kwa skimu za bima yaafya kuweka na kutunza amana katika Benki Kuu ya Tanzania ambayoitatumika kwa ajili ya kuhakikisha kuwa wanachama waliosajiliwa chini yaskimu husika hawaathiriki endapo skimu hizo zitashindwa kuendelea kutoahuduma kwa wanufaika wake kutokana na sababu mbalimbali. Aidha, Serikaliinawasilisha mapendekezo yaliyoainishwa katika Aya R ya Jedwali laMarekebisho yanayobainisha jukumu hili kutekelezwa kupitia Sheria ya Bima,Sura ya 394. Kifungu cha 24 kinaweka utaratibu wa utambuzi wawanachama na wanufaika kwa lengo la kupata taarifa zitakazowezeshauhakiki wa wanachama na kudhibiti udanganyifu. Kifungu cha 25 kinawekamasharti kuhusiana na ukomo wa uanachama ambapo uanachama utafikiaukomo iwapo mwanachama atafariki au ataacha kuchangia katika skimu yabima ya afya. Hata hivyo, kifungu kinabainisha kuwa wategemezi wamwanachama aliyefariki, wataendelea kupata huduma kwa kipindikitakachobainishwa na Waziri mwenye dhamana katika Kanuni. Dhumuni lakifungu hiki ni kulinda haki za wategemezi wa mwanachama. Vilevile, Serikaliinapendekeza kuongeza sababu za ukomo wa uanachama kamailivyoainishwa katika Aya S ya Jedwali la Marekebisho.
Mheshimiwa Spika, Sehemu ya Sita inaweka masharti kuhusu udhibitiubora wa huduma zitolewazo na vituo vya kutolea huduma za afya na skimuza bima ya afya. Kifungu cha 26 kina lengo la kuhakikisha skimu za bima yaafya zinazingatia ubora katika utoaji wa huduma za bima ya afya kulingana namiongozo ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima. Kifungu cha 27 kinaipaWizara jukumu la kuhakikisha kuwa vituo vya kutolea huduma za afyavilivyoingia mikataba na skimu za bima ya afya za umma na binafsi vinatoahuduma bora za afya kwa wanufaika kwa kuzingatia viwango vya uboravilivyotolewa na Wizara kama inavyopendekezwa katika Aya T ya Jedwali lamarekebisho. Dhumuni la kifungu hiki ni kuhakikisha vituo vinatoa hudumabora za afya kwa wananchi kupitia mfumo wa Bima ya Afya.
Mheshimiwa Spika, Sehemu ya Saba inaweka masharti mengineyo ambayokwa namna moja au nyingine yatahusika katika utekelezaji wa masharti yaSheria hii. Kwa kuwa uendeshaji wa skimu utazingatia kanuni za uendeshajiwa bima za afya, Kifungu cha 28 kinaitaka kila skimu ya bima ya afya yaumma na binafsi kufanya tathmini ya uhai na uendelevu wake kila baada yamiaka mitatu au wakati wowote itakavyoelekezwa na Mamlaka ya Usimamiziwa Bima na taarifa ya tathmini kuwasilishwa kwa Mamlaka hiyo pamoja naWaziri. Kifungu hiki kinaipa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima uwezo wakuchukua hatua dhidi ya skimu kutokana na upungufu utakaobainishwa nataarifa ya tathmini ya uhai na uendelevu. Dhumuni la kifungu hiki nikuhakikisha skimu za bima ya afya zinakuwa na ukwasi na uendelevu wakutoa huduma kwa wanufaika.
Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 29 kinaruhusu skimu za bima ya afya zaumma na binafsi kufanya uwekezaji kwa lengo la kukuza mtaji na hivyokuimarisha uhai na uendelevu wake. Aidha, Kifungu cha 30 kinaipa Mamlakaya Usimamizi wa Bima jukumu la kutoa miongozo kuhusiana na ukomo wagharama za uendeshaji wa skimu za bima ya afya ili kuhakikisha skimu hizozinakuwa na uwezo wa kujiendesha na kusimamia utekelezaji wa majukumuyake bila kuathiri utoaji wa huduma za bima ya afya kwa wanachama wake.
Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa haki za wanufaika na watoahuduma katika mfumo wa bima ya afya zinalindwa, Kifungu cha 31 kinawekautaratibu wa namna ambavyo Mamlaka ya Usimamizi wa Bimaitakavyoshughulikia malalamiko.
Mheshimiwa Spika, Kufuatia maoni na ushauri wa wadau mbalimbali pamojana Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI, Serikali,kupitia Aya W ya Jedwali la Marekebisho, inapendekeza kukifuta kifungucha 32 kilichokuwa kimefungamanisha huduma mbalimbali za kijamii nabima ya afya. Huduma zilizokuwa zimefungamanishwa ni pamoja na leseniya udereva, bima za vyombo vya moto, viza ya kuingilia nchini, utambulishowa mlipa kodi, Usajili wa Laini za Simu, hati ya kusafiria, uandikishaji wawanafunzi kidato cha tano na cha sita na utoaji wa kitambulisho cha Taifa.
Mheshimiwa Spika, Hata hivyo ni lengo ya Serikali kuwa kila mtu nchini awena bima ya afya ili kuwa na uhakika wa matibabu kabla ya kuugua. Baada yaSheria hii kupitishwa, Serikali itaendelea kutoa elimu na hamasa kwawananchi kuhusu dhana na umuhimu wa bima ya afya lengo likiwa nikuwaepusha wananchi kuingia katika umaskini. Tunayo mifano iliyo hai yawananchi ambao walilazimika kuuza mali zao ikiwemo mashamba, mifugo,vyombo vya usafiri, vifaa vya ndani na kuweka rehani mali zao ili kugharamiamatibabu yao au ya wapendwa wao. Aidha Seerikali itaendelea kuboreshahuduma za afya katika ngazi zote ili kuwezesha wananchi kupata hudumabora za afya.
Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 33 kinampa Waziri mamlaka ya kutungaKanuni kwa masuala mbalimbali kwa lengo la kutekeleza sheriainayopendekezwa kwa ufanisi. Aidha Kifungu cha 34 kinaweka katazo kwawanufaika, vituo vya kutolea huduma za afya na skimu za bima ya afya namtu yeyote kutoa taarifa za uongo na kuweka adhabu iwapo watathibitikakufanya hivyo. Dhumuni la kifungu hiki ni kulinda uhai na uendelevu wa skimuza bima ya afya kwa kuzuia masuala ya udanganyifu na ubadhirifu wa pesaza wanachama ili kuhakikisha huduma za bima ya afya zinazotolewa zinakidhivigezo na ni endelevu. Aidha, Serikali inapendekeza kufanya marekebishokatika kifungu hicho kwa kutenganisha adhabu ya Skimu ya Bima ya afya navituo vya kutolea huduma za afya, kuongeza kiwango cha kulipa faini,kuongeza sharti la ulipaji wa fidia kwa hasara iliyosababishwa na kuwekaadhabu kwa wataalam, kama inavyobainishwa katika Aya Y ya Jedwali laMarekebisho.
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia maoni ya kutokufungamanisha hudumaza kijamii na bima ya afya na katika kuhakikisha ulazima wa kuwa na bima yaafya unatekelezwa, Serikali katika Aya Z ya Jedwali la marekebishoinapendekeza kufanya marekebisho kwa kuweka adhabu ya asilimia 10 yamchango wa kila mwaka kwa mtu yeyote ambaye hatajiunga na bima ya afyakwa kipindi cha miaka mitatu tangu kuanza kutekelezwa kwa Sheriainayopendekezwa. Hata hivyo, Waziri amepewa mamlaka ya kutoa msamahawa ulipaji wa adhabu ya asilimia 10 kwa kuzingatia maslahi ya umma ausababu nyingine yoyote.
Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 35 kinaweka utaratibu wa kushughulikiamadai ya skimu za bima ya afya ambapo mahakama ina uwezo wa kuamuruulipwaji wa fidia iwapo kosa litathibitika kutendwa na mwanachama au mtuyoyote. Vilevile, Kifungu cha 36 kinatoa adhabu ya jumla kwa makosaambayo adhabu mahsusi haijatolewa chini ya Sheria inayopendekezwa.Dhumuni la kifungu hiki ni kuweka utaratibu wa kushughulikia makosa yoteambayo hayajawekewa adhabu mahsusi katika Sheria. Serikali inapendekezakufanya marekebisho ya kutenganisha adhabu kati ya mtu binafsi na taasisikama inavyobainishwa katika Aya AA ya Jedwali la Marekebisho.
Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 37 kinaweka utaratibu wa uwajibishwaji wachombo hodhi pamoja na watendaji kwa makosa yatakayofanywa chini yaSheria inayopendekezwa kwa lengo la kuweka utii wa Sheria. Kifungu cha38 kinaweka ukuu wa Sheria inayopendekezwa na sheria nyingine katikamasuala yanayohusu uendeshaji na usimamizi wa mfumo wa bima ya afyanchini. Lengo la kifungu hiki ni kuondoa ukinzani wa sheria baina ya Sheria hiina sheria nyingine yoyote inayohusiana na masuala ya bima ya afya.
Mheshimiwa Spika, Sehemu ya Nane inaainisha masharti kuhusu Sheria yaMfuko wa Afya ya Jamii, masharti ya mpito na masharti yanayoendelea.Kifungu cha 39 kinafuta Sheria ya Mfuko wa Afya ya Jamii na wanufaikawataendelea kupata huduma kupitia kitita cha bima ya afya cha Jamii(Community Health Insurance Package – CHIP) kama inavyobainishwakatika Aya BB ya Jedwali la Marekebisho. Kifungu hiki pia kinabainishamasharti yatakayoendelea kutekelezwa baada ya kufutwa kwa Sheria yaMfuko wa Afya ya Jamii ili kulinda haki za wanufaika wake.
Mheshimiwa Spika, sababu kubwa ya kuchukua hatua hii ni Muundo waMfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kutokidhi misingi na kanuni za uendeshaji wabima ya afya mathalani, Mfuko wa Afya ya Jamii una wigo mdogo wakuchangiana kati ya Mikoa na Halmashauri zenye uchumi mkubwa na mdogo,wananchi wenye kipato kikubwa na kidogo na wagonjwa na wasio wagonjwakutokana na kusimamiwa katika ngazi za Mamlaka za Serikali za Mitaa,wanufaika kutoweza kupata huduma za afya nchi nzima isipokuwa katikaHalmashauri walizojiandikisha tu.
Mheshimiwa Spika, sababu nyingine ni ufinyu wa huduma katika kitita chamafao kinachotolewa na hivyo kukosekana kwa huduma muhimu mathalanihuduma za afya ya kinywa na meno, kutojumuishwa kwa baadhi ya dawa nahivyo kumlazimu mwanachama kulipia. Vilevile, wananchi kutopata hudumaza afya wanapokuwa nje ya maeneo waliyojiandikisha na hivyo kulazimukulipia huduma za afya kwa utaratibu wa papo kwa papo hali inayoathirishughuli za kijamii na kiuchumi.
Mheshimiwa Spika, Kifungu cha 40 kinaweka masharti kuhusiana na kipindicha mpito kisichozidi miezi kumi na miwili tangu kuanza kutumika kwa Sheriainayopendekezwa ambapo wadau wote watapaswa kutekeleza masharti yaSheria hiyo. Vilevile, Kifungu hicho kinampa Waziri mamlaka ya kuongezakipindi cha ziada cha mpito kisichozidi miezi sita baada ya kipindi cha awalicha mwaka mmoja kupita. Lengo la kifungu hiki ni kuhakikisha uendelevu wahuduma kwa wanachama walio kwenye skimu mbalimbali na kuwawezeshawadau mbalimbali kufanya maandalizi na kukamilisha taratibu za utekelezajiwa Sheria inayopendekezwa.
Mheshimiwa Spika, Sehemu ya Tisa inabainisha Sheria mbalimbalizitakazofanyiwa marekebisho baada ya Muswada huu kupita. Sheria hizo niSheria ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Sura ya 395; Sheria ya Hifadhi yaJamii, Sura ya 135; Sheria ya Bima, Sura ya 394; Sheria ya Mtoto, Sura ya13; Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini, Sura ya 366; Sheria ya Udhibiti waHospitali Binafsi, Sura ya 151; na Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi yaJamii, Sura ya 50.
Mheshimiwa Spika, naomba kutumia fursa hii kutoa ufafanuzi kuhususababu za kufanya marekebisho ya Sheria ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi yaJamii Sura ya 50. Marekebisho haya yanalenga kuendelea kutoa fao lamatibabu kwa wanufaika wake kama fao la afya na sio bima ya afya.
Mheshimiwa Spika, Katika kuhakikisha Sheria inayopendekezwainatekelezwa kwa ufanisi Serikali imejipanga kutoa elimu kwa umma kuhusudhana na umuhimu wa bima ya afya. Utoaji wa elimu kwa umma utatekelezwakupitia Mkakati wa Utoaji wa Elimu kwa Umma unaobainisha jumbe mahususi
zinazotakiwa kutolewa, ushirikishaji wa wadau mbalimbali hususan viongoziwa kisiasa, viongozi wa dini, pamoja na viongozi katika ngazi ya Taifa, Mikoana Mamlaka za Serikali za Mitaa. Elimu kwa umma itatolewa kabla na wakatiwa utekelezaji wa Sheria hiyo.
Mheshimiwa Spika, tunatambua pia kuwa utekelezaji wa Sheriainayopendekezwa na utayari wa wananchi kujiunga na Skimu za Bima ya afyaunategemea kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa huduma bora za afyazinazotolewa kwa wananchi wenye bima ya afya. Hivyo huduma za afyazikiwa bora zitawavutia wananchi wengi kujiunga na skimu za bima ya afya.Katika kutambua hilo, Serikali itahakikisha huduma bora za afya zinapatikanakatika ngazi zote. Kwa mfano katika kipindi cha takriban miaka mitatu vituovya kutolea huduma za afya vimeongezeka kutoka vituo 8,449 mwaka (2019)hadi kufikia vituo 11,630 mwezi Septemba, 2023, sawa na ongezeko laVituo 3,181. Vilevile, upatikanaji wa dawa katika vituo vya kutolea hudumaza afya umeimarika kutoka asilimia 62 mwezi Agosti, 2022 hadi kufikiaasilimia 73 (mwezi Agosti, 2023).
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha awamu ya sita chini ya MheshimiwaDkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniaumefanyika uwekezaji mkubwa katika vifaatiba vya kisasa vya uchunguzi wamagonjwa na matibabu ikiwemo X-rays (199), CT-Scan (30), MRI (4) ikiwa nipamoja na Ujenzi wa Idara ya Wagonjwa wa Dharura (EMD) (111) na Wodiza Wagonjwa Muhtuti (ICU) (73) hadi katika ngazi ya Hospitali zaHalmashauri. Uwepo wa hatua hii katika vituo vya kutolea huduma za afyakumesogeza huduma za kiuchunguzi karibu zaidi na wananchi nakuwapunguzia gharama waliyokuwa wakitumia kufuata huduma hizo katikaHospitali za Taifa.
Mheshimiwa Spika, Serikali pia imeendelea kuongeza rasilimali watu katikasekta ya Afya, ambapo Mwaka 2020/2021 iliajiri watumishi wa afya 3,347,Mwaka 2021/2022 watumishi 10,285 na mwaka 202/23 watumishi 8,8277waliajiriwa. Vilevile, katika mwaka wa fedha 2023/2024 kiasi cha Shilingibilioni tisa (9) zimetengwa kwa ajili ya ufadhili wa mafunzo ya Ubingwa na
Ubingwa Bobezi kwa watumishi wa Afya wa Serikali. Aidha, tutaendelezajitihada za kuhakikisha watumishi wa afya wanatoa huduma kwa kuzingatiaWeledi na Maadili.
Mheshimiwa Spika, katika kuwezesha utoaji wa huduma bora za bima yaafya kwa wananchi, Serikali pia itaendelea kuimarisha matumizi ya TEHAMA.Ili kuwezesha utekelezaji wa Sheria hii, tutazitaka skimu za bima ya afyakuimarisha matumizi ya TEHAMA katika utoaji wa huduma za bima ya afyaikiwemo usajili na utambuzi wa wanachama na vituo vya kutolea huduma zaafya na utekelezaji wa majukumu ya skimu hizo. Hatua hii pia itasaidiakudhibiti udanganyifu na vitendo vya ubadhirifu ambapo fedha nyingi hupoteana hivyo kuzifanya skimu za bima ya afya kutokuwa endelevu. Serikaliitahakikisha kwamba mfumo wa bima ya afya unasimamiwa ipasavyo, kupitiaMamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA) ambayo itahakikisha haki nawajibu wa mwanachama, mtoa huduma na skimu za bima ya afyazinatekelezwa kwa mujibu wa Sheria.
Mheshimiwa Spika, kabla ya kuhitimisha maelezo yangu kuhusu Muswadahuu, naomba kutoa kwa ufupi manufaa ya kutungwa kwa sheria hii ambayo nipamoja na; Kundi kubwa la wananchi kuwa na uhakika wa kupata hudumaza matibabu bila kikwazo cha fedha; kuimarisha Uboreshaji wa hudumakatika Vituo vya kutolea huduma za afya vya Umma na binafsi, ikiwa nipamoja na kuimarika kwa upatikanaji wa dawa, vifaa na vifaa tiba; kuimarikakwa Uhimilivu na ustahimilivu wa Skimu za bima ya afya kutoa hudumakwa kuwa wananchi watapaswa kujiunga na Skimu za Bima ya Afya kabla yakuwa ni wagonjwa; Kuimarika kwa usimamizi na udhibiti katika utoaji wahuduma za Bima ya Afya zitolewazo na Mifuko na Kampuni Binafsi za Bimaya Afya; Kuboreshwa kwa vitita vya mafao vinavyotolewa na skimu za bimaya afya na Kuimarisha hali ya kipato kwa wananchi.
Mheshimiwa Spika, athari zitakazoendelea kujitokeza endapo Sheria hiihaitatungwa ni pamoja na; Wananchi kujiunga kwa hiari na wakiwa tayari niwagonjwa na hivyo kuondoa dhana ya kuchangiana gharama za matibabu;Kudhoofisha uhai na uendelevu wa skimu za bima ya afya zilizopo; Kundi
kubwa la wananchi kuwa nje ya mfumo wa bima ya afya (asilimia 85) hivyokuwa katika hatari ya umaskini; Wananchi kushindwa kumudu gharama zamatibabu kutokana na kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambukizwa (NCDs);Kukosekana kwa Udhibiti Madhubuti wa utoaji wa huduma katika soko la bimaya afya na Serikali kushindwa kufikia lengo la Afya Bora kwa Wote.
Mheshimiwa Spika, mwisho lakini sio kwa umuhimu, naomba nisisitize kuwa,Bima ya Afya ndio mfumo bora, rahisi na endelevu ambao umethibitika katikanchi mbalimbali duniani kuwawezesha wananchi wengi hususani wa kipatocha chini kupata huduma bora za afya pindi wanapozihitaji. Wengitunafahamu kuwa pale familia inapokuwa na mgonjwa basi huuza mali zao ilikupata fedha za kulipia gharama za matibabu. Nitumie fursa hii kutoa witokwa wananchi wote kujiunga na Bima ya Afya ili kuwa na uhakika wamatibabu kabla ya kuugua.
SHUKRANI
Mheshimiwa Spika, naomba kutumia fursa hii kumshukuru sana Mhe. Dkt.Godwin Mollel (Mb.), Naibu Waziri wa Afya kwa ushirikiano anaoendeleakunipa wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yangu hasa katika kipindicha maandalizi ya Muswada huu. Aidha, ninawapongeza watumishi wote waWizara ya Afya wakiongozwa na Dkt. John A.K. Jingu, Katibu Mkuu, Dkt.Grace E. Magembe, Naibu Katibu Mkuu na Prof. Tumaini J. Nagu, MgangaMkuu wa Serikali. Kwa mara nyingine tena nimshukuru Mhe. KassimMajaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano waTanzania kwa kutuongoza vyema katika mchakato huu, Mhe. Jenista J.Mhagama (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge naUratibu) kwa uratibu na ushirikiano wake katika maandalizi ya Muswada huu.Kipekee nitambue mchango wa Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba(Mb.), Waziri wa Fedha, kwa ushirikiano wake katika kipindi chote chamaandalizi ya muswada huu hususan katika kuwezesha upatikanaji wavyanzo vya fedha kwa ajili ya kugharamia bima ya afya kwa watu wasio nauwezo. Kwa namna ya pekee pia ninamshukuru Mhe. Jaji Dkt. Eliezer MbukiFeleshi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ndugu Onorius Njole, MwandishiMkuu wa Sheria na watumishi wote wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali kwa ushirikiano walioutoa wakati wa Maandalizi ya Muswada huu.Vilevile, niwashukuru wataalam kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI na Wadauwote wa sekta ya afya waliotoa ushauri, maoni na mapendekezoyaliyowezesha maandalizi ya Muswada huu.
Mwisho na si kwa umuhimu nitambue taasisi zifuatazo:- TASAF, APHTA,TEA, Kampuni binafasi za Bima ya Afya, TIRA, NHIF, NBS na NSSF.
Mheshimiwa Spika, naomba nirudie tena kuishukuru Kamati ya Kudumu yaBunge ya Afya na masuala ya UKIMWI. Nimalizie kwa kukushukuru weweMheshimiwa Spika, kwa kunipa fursa ya kuwasilisha Muswada huu nanichukue nafasi hii kuliomba Bunge lako Tukufu liujadili Muswada huu waSheria ya Bima ya Afya kwa Wote (Na.8) wa Mwaka 2022 na kuupitishakatika hatua ya Kusomwa kwa Mara ya Tatu na hatimaye Sheriainayopendekezwa kuwa sehemu ya Sheria za Nchi.
Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.