Muogope mtu ambaye ni maskini ila anaishi kitajiri, kimahusiano atakufilisi

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Feb 4, 2024
291
772
Muogope sana mtu ambaye bajeti zake za kuishi tu ni kubwa zaidi ya uwezo wake kujimudu yaani yupo radhi aishi kwa madeni ili nje aonekane tajiri.

Muogope sana mtu ambaye yuko tayari kumiliki simu ya laki tano ila kipato chake kinamruhusu amiliki ya laki moja, mtu huyu ambaye ana simu ya laki tano ili aonekane tajiri na bado anategemea chanzo kimoja tu cha kipato jua hayuko sawa ki akili muogope sana.

Muogope sana mtu ambaye kwao kula milo mitatu tu shida ila akiwa nawe anajinadi kula mlo wa laki moja kwa siku tena usipomtimizia anakutangaza wewe ni maskini usiyemfaa na kusahau kuwa wazazi wake ndio maskini zaidi kumudu hiyo milo mitatu.

Muogope sana mtu ambaye ukiingia kwake unakuta vitu vya thamani kubwa zaidi ya kipato chake ila hana biashara wala hata kiwanja na yupo kazini takribani mwaka wa tano sasa.

UKIHUSIANA NA MTU HUYO JUA AMA UTAFILISIKA AU MTAISHIA KUISHI KUPENDEZA WATU HUKU MKIANGAMIA KIUCHUMI.

Jiandaye kufilisika ikiwa unahusiana na mtu ambaye hayuko tayari kuishi kulingana na urefu wa kamba yake na kama sio kufilisika basi jiandaeni kuishi maisha ya kuwapendeza watu huku ndani mkiangamia kiuchumi, yaani mtaonekana matajiri kwa vitu vya mkopo au kwa maisha ambayo yanawafanya mjichimbie shimo la umaskini.

Usikubali kuhusiana na mtu ambaye kaona kwako kuna ajira hivyo kutumia ndio msingi mkubwa kwake lakini hakushauei wala kukupa mbinu za kukukua kiuchumi

Mtu ambaye hataki kuishi kulingana na kipato chake muogope sana.

#Mwanasayansi Saul kalivubha.
#fikia ndoto zako.
 
Wanajifanya kufungua viduka vya nguo ili kuficha chaka lao la udangaji.
 
Wapo wengi zaidi ya waliobarikiwa kuwa navyo.Changamoto iliyopo ni namna ya kuishi nao kisanii.Kuliwa lazima uliwe tu(akutumie kwa manufaa yake kiuchumi)lakini ni vema ukawa makini na umtangulie kiakili.
 
Usiiangamize nafsi yako kwa kuishi maisha yaliyo juu ya uwezo wako
 
Back
Top Bottom