Mungu hakumaliza uumbaji

Michael Mlay

Member
Aug 24, 2022
57
84
Habari zenu wana JF,

Tusipoteze muda twende kwenye point, ukiangalia duniani sasa hivi kuna vitu vingi sana vya ajabu. Mfano kuna meli ambazo zina uwezo wa kubeba matani ya mizigo pasipo kuzama majini,kuna ndege ambazo ni kubwa sana zinapaa pasina shida yoyote, kuna simu ambazo unaweza wasiliana na mtu yoyote yule duniani, kuna taa, umeme, magari, treni, robots na vingine vingi sana lakini ukifatilia vitu hivi Mungu hakuviumba kabisa huku duniani, je nini maana yake?

Mungu alivyoumba vitu natural kama jua, anga, ardhi nk, akaamua kumuumba mwanadamu ili akaendeleze UUMBAJI wake hapa duniani ndo maana unaona kuna vitu vingi sana ambavyo wakati Mungu anaumba Dunia havikuwepo kabisa but now vimezagaa Duniani kote na bado vinakuja kwa kasi zaidi kutokana na advancement of technology.

Mungu hakutaka kuumba kila kitu, alitaka kushirikiana na wanadamu kwenye kuendeleza uumbaji wake hapa Duniani, hivyo kila mwanadamu ana nguvu ya uumbaji ndani yake kwaajili ya kuendeleza uumbaji wa Mungu Duniani.

Swali ni je, mbona hivo vitu vimetengenezwa na watu wachache sana ambao mpaka leo wameacha historia kwenye Dunia hii? Watu kama akina Izaak newton, Thomas Edison, Robert NK. Sababu kubwa ni watu kutojua uwezo ambao umo ndani yao ambao Mungu aliuweka wakati anatuumba wanadamu tuje tutawale Dunia. So ukianza kujua wewe ni nani utaanza KUENDELEZA UUMBAJI WA MUNGU DUNIANI, "Idea rules the world."
 
Habari zenu wanajf
Tusipoteze muda twende kwenye point,ukiangalia duniani sas Kuna vitu vingi sana vya ajabu mfano Kuna Meri ambazo zina uwezo wa kubeba matani ya mizigo pasipo kuzama majini,Kuna ndege ambazo ni kubwa sana zinapaa pasina shida

Kuna utofauti kati ya kuumba na kuunda. Huwezi kutengeneza gari ukasema umeumba gari
 
Kuendeleza uumbaji, uko sahihi mkuu.

Alipoumba chuma na aluminium na miti yenye rubber bas ni kazi yetu kuendeleza Kwa kuunda magari na matajiri nk...

KUENDELEZA...!
 
Back
Top Bottom