TANZIA Mungu ailaze roho ya Janken John Njunde mahali pema peponi

DOKEZO

JF-Expert Member
Jan 17, 2014
322
496
Ni siku yako ya kwanza leo umelala katika udongo wa ardhi toka jana zoezi la kukuhifadhi katika makaburi ya Ununio likamilike. Janken umekwenda kaka tuna imani Mungu amekupokea kwa furaha baada ya kutimiza malengo aliyokupa hapa duniani.

Tunaamini umefika salama kwa mungu baba hakika kama binadamu tutazidi kukuombea heri uko ulipo. Umeweza kuishi kusudi la maisha yako na wote uliogusa maisha yao wanaomboleza na kukuombea hakika pengo lako kwetu sote ni kubwa sana. Tutakukumbuka daima kwa kadri ya urefu wa maisha yetu sisi uliotuacha hapa duniani.

Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi JANKEN JOHN NJUNDE.

Screenshots_2024-01-30-09-55-31.png
 
Huyu Jamaa nilikuwa naona nae miaka 4 iliyopita NBC tawi Kariakoo, Mcheshi sana .Nimemsave Junken Manager Nbc. Aisee poleni sana Familia
 
Back
Top Bottom