george aloyce
JF-Expert Member
- Aug 22, 2017
- 1,302
- 2,021
Nimeolewa lakini sifurahii ndoa yangu kabisa, nilichokitegemea kwenye ndoa si ninachokipata. Mimi ni binti wa miaka 24, nimeolewa na mume wangu ni askari, yeye ni polisi wa kata hivyo tuko huku Songea ni kijijini sana. Huyu kaka wakati nakutana naye tulikuwa Arusha ila akaja kuhamishwa huku kipindi ndiyo tuko kwenye mchakato wa ndoa.
Sikuona shida kwani niliamini kwa kuwa ni kazi ya serikali basi atapata uhamisho. Baada ya ndoa ndiyo nikaja huku, mimi ndiyo nimeamaliza chuo hivyo sina kazi najaribu kuomba lakini sijapata.
Hali ya huku ni ya shida kweli siwezi kuishi maisha haya, umeme upo lakini ni ile sehemu ambayo ukiingia ndani ni umeingia, hakuna cha kusema utokea uongee na majirani kila mmoja yuko shambani sijui ana mambo yake. Kwanza nyumba zenyewe ni za mbali mbali, na kupata nyumba ya maana ni changamoto sana kama unavyojua vijijini
Nikimuambia mwanaume kuhusu kuhama ananiambia ndiyo kwanza kahamishwa hawezi kupata tena uhamisho. Nimejikuta nimekuwa mtu wa hasira, yaani kila siku tunagombana, mume wangu anajitahidi kunisawazisha lakini siwezi, namkasirikia tu bila sababu kitu ambacho sikipendi.
Nimemuambia mimi angalau anitafutie nyumba mjini awe anakuja lakini hataki kwa sababu ni mbali sana, kutoka alipo mpaka mjini ni siku nzima na usafiri ni wa shida, ndoa ina miezi 8 mwanamume anataka mtoto lakini siko tayari kuzaa kwenye mazingira haya, ni bora kuachana lakini sijui namuachaje mwanamume ambaye hajawahi kunikosea!