Muliro: Clip ya anayedaiwa kuiba mtoto eneo la Goba ni ya Julai, 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,710
13,462
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam tarehe 25 Julai, 2024, Saa 3:20 asubuhi ilipata taarifa kuwa eno la Goba Matosa, Kinondoni kulikuwa na tukio la mauaji yaliyotokana na ugomvi kati ya watu wanaodaiwa kuwa ni wapenzi

Polisi baada ya kufika eneo la tukio walibaini kuwepo kwa mwili wa mtu ambaye alishapoteza maisha aliyefahamika kwa jina la Lucy Stevin Haule (29) mfanyakazi wa kiwanda cha pombe kali iitwayo nguvu banana wine. Uchunguzi wa awali umeonesha marehemu aliuawa na mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la Musa Sasi (32) anayefanya kazi ya kibarua katika kiwanda cha pombe ya banana, na Mkazi wa Goba Matosa.

Baada ya kumuua mpenzi wake, mtuhumiwa naye alijaribu kujiua kwa kutumia kisu, kwa kujichoma shingoni. Mtuhumiwa huyo amekamatwa na hali yake ni mbaya na yupo Hospitali ya rufaa ya Mwananyamala. Chanzo halisi cha ugomvi uliopelekea mauji hayo bado kinachunguzwa.
WhatsApp Image 2024-07-25 at 17.07.26_0276a04a.jpg
Jeshi la Polisi linatoa wito pindi watu wanapokuwa na migogoro au matatizo ya kijamii wazishirikishe taasisi mbalimbali za kisheria, za kiserikali na zisizo za kiserikali lakini pia taasisi za kidini ili zisaidie kutatua matatizo ya wahusika.

Pia, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya dola na wananchi wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali za kuzuia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na watu wengine

kwa ujumla. Vitendo vya ukatili ni pamoja na vya kubaka, kulawiti, kunajisi, mauaji, na ukiukwaji mwingine wowote wa sheria unaohusisha haki za watoto.

Tarehe 24 Julai, 2024 kupitia mitandao ya kijamii kumekuwa na taarifa zilizojaa sintofahamu kuhusu kipande cha picha ya video ikionesha kijana mmoja wa kiume kutoka eneo la Ilala Bungoni akihojiwa na wananchi kusiana jaribio la wizi wa mtoto.

Baada ya kupata taarifa hizo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilizifuatilia taarifa hizo na kubaini kwamba tukio la kipande hicho cha video sio mwaka huu au mwaka jana bali lilitokea Julai, 2022 eneo la Ilala Sharifu Shamba na kuripotiwa kituo cha Polisi Ilala/Pangani kwa madai ya mama moja kumtuhumu Frank Moi Chacha (18) mkazi wa Vingunguti kutaka kuiba mtoto wake. Baadae shauri hilo lilifikishwa Mahakamani kwa CC.165/2022.

Imetolewa na;
Muliro J. MULIRO - SACP
Kamanda Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom