Muigizaji Cherel (Michelle Botes) wa Isidingo afariki dunia

Muga_Thachamp

Member
Dec 11, 2024
38
110
Michelle Botes, aliyetamba sana kupitia series ya Isidingo the Need miaka ya 2000, amefariki dunia.

Michelle Botes, alijulikana kwa kucheza vyema nafasi ya mwanamke muuaji aliyeitwa Cherel De Villiers, na baadaye kuwa Cherel Haines baada ya kuolewa na tajiri Barker Haines,

Ambapo katika series hiyo ya Isidingo, Cherel Haines alimuua mtoto wa kiume wa Barker Haines aliyeitwa Duncan Haines kwa kumpiga risasi kisa ni baada ya mtoto huyo kujua kuwa mamake wa kambo alimuua mume wake wa mwanzo pia na mama wa mume huyo wa mwanzo

Kifo cha mtoto wa Barker Haines ndio moja ya stori zilizofanya watu wapende kufuatilia Isidingo, maana Cherel alifanikiwa kwa muda mrefu kuficha mwili wa Duncan kwa kuuviringisha zulia la sebuleni, na kuutupa kwenye moja ya mashimo ya machimbo ya dhahabu ambayo yalimilikiwa na Barker Haines.

Barker Haines alimpenda Cherel hivi kwamba hakuamini kuwa mkewe huyo aliweza kumuulia mwanae hadi akagombana sana na binti yake aliyeitwa Lee Haines, Lee Haines alikuwa hampendi mamake wa kufikia sababu alijua vifo vya utata vilivyoongozana kwenye familia ya awali ya mamake wa kufikia, aliona mama huyo ana nuksi na hafai kwenye familia yao.

Ila baadae Barker alikubali kuwa Cherel alimuua mwanae baada ya mwili wa Duncan kupatikana.

Ila Cherel hakuweza kufungwa sababu hakukuwa na ushahidi wa dhamira ya kumuua (hakuna aliyejua kuwa siku moja kabla ya kifo chake, Duncan alijua kwa uhakika, na ushahidi, siri za mauji aliyofanya mamake wa kambo) na hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja kuwa Cherel alimuua Duncan pia.

Barker aliishia kumtaliki Cherel na kuishi kwa uchungu, huku akiipa hoteli yake jina la mwanae Duncan, hoteli ikaitwa The Duncan.

Kwa wapenzi wa Isidingo wa mwishoni mwishoni hiyo hoteli ya The Duncan baadae ilikuja kununuliwa na familia ya Matabane na kuitwa Bokamoso.

Kila nafsi itaonja umauti, Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

R.I.P Michelle Botes, maarufu kama Cherel De Villier Haines wa Isidingo
 
Attachments

  • Screenshot_20241223-100934.jpg
    Screenshot_20241223-100934.jpg
    302.8 KB · Views: 8
🎼Tiliri tii rii!!, yehi yeih la!, la!, lah!! 🎼
Nikiona neno ISIDINGO kinakuja icho kimziki kichwani 😂.

Anyway R.I.P Cherel
 
Michelle Botes ameacha watoto wawili, wanaoitwa Cara Roberts na Daniel Roberts, pamoja na mtalaka anayeitwa Ian Roberts

Amefariki jana tarehe 21 December 2024

Chanzo cha kifo chake ni kansa ya damu
 
Michelle Botes, aliyetamba sana kupitia series ya Isidingo the Need miaka ya 2000, amefariki dunia.

Michelle Botes, alijulikana kwa kucheza vyema nafasi ya mwanamke muuaji aliyeitwa Cherel De Villiers, na baadaye kuwa Cherel Haines baada ya kuolewa na tajiri Barker Haines,

Ambapo katika series hiyo ya Isidingo, Cherel Haines alimuua mtoto wa kiume wa Barker Haines aliyeitwa Duncan Haines kwa kumpiga risasi kisa ni baada ya mtoto huyo kujua kuwa mamake wa kambo alimuua mume wake wa mwanzo pia na mama wa mume huyo wa mwanzo

Kifo cha mtoto wa Barker Haines ndio moja ya stori zilizofanya watu wapende kufuatilia Isidingo, maana Cherel alifanikiwa kwa muda mrefu kuficha mwili wa Duncan kwa kuuviringisha zulia la sebuleni, na kuutupa kwenye moja ya mashimo ya machimbo ya dhahabu ambayo yalimilikiwa na Barker Haines.

Barker Haines alimpenda Cherel hivi kwamba hakuamini kuwa mkewe huyo aliweza kumuulia mwanae hadi akagombana sana na binti yake aliyeitwa Lee Haines, Lee Haines alikuwa hampendi mamake wa kufikia sababu alijua vifo vya utata vilivyoongozana kwenye familia ya awali ya mamake wa kufikia, aliona mama huyo ana nuksi na hafai kwenye familia yao.

Ila baadae Barker alikubali kuwa Cherel alimuua mwanae baada ya mwili wa Duncan kupatikana.

Ila Cherel hakuweza kufungwa sababu hakukuwa na ushahidi wa dhamira ya kumuua (hakuna aliyejua kuwa siku moja kabla ya kifo chake, Duncan alijua kwa uhakika, na ushahidi, siri za mauji aliyofanya mamake wa kambo) na hakukuwa na ushahidi wa moja kwa moja kuwa Cherel alimuua Duncan pia.

Barker aliishia kumtaliki Cherel na kuishi kwa uchungu, huku akiipa hoteli yake jina la mwanae Duncan, hoteli ikaitwa The Duncan.

Kwa wapenzi wa Isidingo wa mwishoni mwishoni hiyo hoteli ya The Duncan baadae ilikuja kununuliwa na familia ya Matabane na kuitwa Bokamoso.

Kila nafsi itaonja umauti, Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe

R.I.P Michelle Botes, maarufu kama Cherel De Villier Haines wa Isidingo
Dah kweli tumezeeka na sisi
 
Back
Top Bottom