Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Itikadi, Uenezi na Mafunzo ndugu Paul Makonda leo tarehe 1 December 2023 amemtembelea na kumshukuru Mufti wa Tanzania Dkt. Abubakary Zuberi bin Ally kwa kumuombea na kuanae katika nyakati zote alizo zipitia makonda kuendelea kupata Baraka zaidi.
Mwenezi Makonda amefanya hivyo ikiwa ni muendelezo wa ushirikiano na Viongozi wa Dini katika kufanya kazi kwani anatambua ndio sehemu kubwa inayochochea uwepo wa Amani katika Taifa kutokana na maombi yao.
Kwa upande wa Mufti Dkt. Abubakary Zuberi Bin Ally amempokea na kumfanyia dua maalum ndugu Paul Makonda na kumuahidi kuendeleza ushirikiano na nakuombea katika kuhakikisha anafanya kazi zake vyema kwa lengo la kumsaidia Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan , kwa manufaa ya Watanzania na Taifa kwa Ujumla.
#Kaziinaendelea.