Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,717
- 13,467
Mufti Zubeir awataka Masheikh wa Mikoa, Wilaya, Kata na Maimamu wakemee mmomonyoko wa Maadili
Akizungumza katika tukio la Kumbukumbu ya Miaka 8 ya Mufti Dkt. Abubakar Zubeir, leo Juni 22, 2023 katika Ukumbi wa Mfalme Mohammed Vi, kiongozi huyo amesema Sikukuu ya Eid Kitaifa inatarajiwa kufanyika.
Amesema itafanyika Jijini Dar es Salaam katika msikiti Mkuu Mohammed VI uliopo Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) mnamo Juni 29, 2023 baada ya mikoa mingine kutotuma maombi.
Amesema “Suala la maadili tulipe nafasi kubwa. Tuelimishe watu wetu, tukemee momonyoko kwa nguvu zote. Masheikh wa mikoa, wilaya, kata na maimamu wakemee momonyoko na kupinga vikali itikadi na utamaduni kinyume na dini na desturi yetu.”
Mgeni rasmi siku hiyo ya Eid anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye atafika katika shughuli hiyo baada ya kuagizwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye awali ndiye aliyeombwa kuwa mgeni rasmi.
Aidha, ametaja mafanikio ambayo yamepatikana chini ya uongozi wake ndani ya kipinchi cha miaka 8 ikiwemo; Uwepo wa Jengo kubwa la ofisi ambalo limefikia hatua nzuri, uwepo wa washauri kwa mujibu wa katiba yao, kuwepo kwa JUWAKITA Na JUVIKIBA kwenye katiba yao ambapo zimefika mpaka misikitini.
Mengine ni kujenga zahanati 120 zilizo katika hatua mbalimbali pamoja na vituo vya afya, kuanzisha kitengo cha habari ofisi ya Mufti na kuongeza ushirikiano na vyombo vya habari vyote nchini,
Sasa tumeanza kuanzisha vituo vya uwekezaji mkubwa, mfano kituo cha Biashara cha BAKWATA kinachojengwa Bukoba kwa Bilioni tano.
Kuanzisha BAKWATA Online Academy, kufundisha na kuwapa vyeti viongozi zaidi ya elfu sita na waliosoma kupitia mtandao ni zaidi ya laki moja na elfu sitini Kozi 14 zimefundishwa.