Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,069
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais IKULU, Zuhura Yunus, leo ameita waandishi wa habari kuwapatia taarifa mbalimbali kuhusiana na ziara za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan za nje ya nchi za hivi karibuni na tija zake. Tukio linarushwa MUBASHARA na waandishi kutoka vyombo vikubwa na vya kati nchini wamealikwa.
Tumezoea kuona utaratibu huu ukifanyika kwa mataifa yaliyoendelea na hasa nchini Marekani ambapo Press Secretary amekuwa akiita waandishi kwa ajili ya kuwapa taarifa, kujibu maswali na kufafanua masuala mbalimbali yanayomhusu Rais na Serikali.
Kama tunafuatilia kwa umakini, tutaona hii ni hatua ya pili ya mapinduzi katika Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu tangu Zuhura ateuliwe, ambapo hatua ya kwanza tuliona akibadili namna ya kutoa taarifa kwa umma kwa kuweka angle na kuzitoa kwa lugha mbili; Kiingereza na Kiswahili, kitu ambacho hakikuwahi kuwepo kabla yake.
Nashauri tutumie uzi huu kushauri wapi pa kuboresha na wapi pa kupunguza ili aendelee kuboresha.
Natanguliza ushauri: Awe anawaalika waandishi wa habari kutoka media zote na wale binafsi wanaotambulika kama kina Paschal Mayala, pia awaruhusu waulize maswali ya papo kwa papo na kupatiwa ufafanuzi wa haraka.