Muda wa matumizi ya ving'amuzi vya TV kwanini usihesabiwe kwa siku halisi za kutazama?

Mkoba wa Mama

JF-Expert Member
May 5, 2021
218
99
Kwa mfumo wa sasa wa malipo ya ving’amuzi vya TV, kifurushi cha mwezi hukatika baada ya siku 30, bila kujali kama mtumiaji ametazama TV kila siku au la. Hii inamaanisha kuwa hata ikiwa mtu hajaangalia TV kwa muda mrefu ndani ya mwezi huo au hata mwezi mzima, bado atalazimika kulipia kifurushi kipya baada ya muda kuisha.

Je, si haki zaidi kama siku za matumizi zikihesabiwa kulingana na muda halisi ambao mtumiaji ametumia king’amuzi chake (siku alizotazama TV)? Mfumo huu ungemwezesha mtumiaji kupata thamani halisi ya pesa zake kwa kutumia kifurushi chake kwa siku 30 halisi badala ya siku 30 mfululizo bila kujali matumizi yake.

Mfumo huu utawasaidia zaidi wateja, hasa wale wasioweza kutazama TV kila siku, na pia ungeongeza usawa katika matumizi ya huduma hizi.

Wataalamu wa mambo mlitazame hili.
 
Back
Top Bottom