matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,469
- 17,990
Mwanzoni mwa mwaka huu niliboresha mifumo yangu ya kijamii kwa kukitoa kipengere cha kumuaga marehemu mara ya mwisho kama ni kitu cha lazima kwangu. Sifanyi hicho kitu tena.
Naamini muda sahihi wa kumuaga mtu mara ya mwisho ni wakati akiwa hai, kama hutapata nafasi basi jitahidi kukumbuka mazuri yake inatosha.
Mtu akifa hajui kitu chochote. Kilio, unyenyekevu na huzuni unayoionyesha kwa maiti haimuhusu chochote muhusika wala haimuathili chochote. Vitu vivyo vinapaswa kufanyika akiwa katika hatua za mwisho.
Katika hili naungana na wayahudi na waislamu katika kutoaga kwa kuangalia sura ya maiti.
Faida ya huu utaratibu mpya kwangu, nimekuwa mwepesi sana kuwaona wagonjwa, watu wanaopitia nyakati ngumu hata kwa kupiga simu maana najua ndio muda wa thamani sana kwao maana ikitokea wamelala sinanafasi hiyo. Hivyo siwezi kuweka picha ya mtu aliyekufa status, au social media au kutembea na tshirt maana kwangu ni njia potofu ya kumkumbuka.
Natambua ni utaratibu mzuri kwa wanaoupenda ila kwa tukio la kupuuza kumuona rafiki yangu na jirani mgonjwa baada ya masaa mawili akafa na sikuwa na sababu ya msingi kutomuona nimeachana na utamaduni wa kuona maiti.
Ni hayo tu.
Mtumishi Matunduizi.