Muda mwingine uhalisia tunaouona sio kweli sana, hata vitu vingi vinavyotuvutia hatujui sababu hasa kwanini vimetuvutia

NadeOj

JF-Expert Member
Mar 25, 2024
457
863
Umewahi kujiuliza je?

Mfano wewe ni mpenzi wa yanga au simba, ni kwanini unapenda na ni vigumu kubadilishwa mtizamo wako kiasi kwamba hata wazingue kwa kiasi kikubwa bado utazidi kutafuta namna ya kutetea ili uendelee kuipenda.

Kuna case mbili fikiria alafu useme katika case ipi utabadili timu.

Case I.
Ikitokea wachezaji wote wa yanga pamoja na kocha na viongozi waende kuajiriwa simba, Kisha wa simba waende yanga, lakini majina ya timu yabaki hivyo hivyo.

Je, utaendelea kuwa katika timu hiyo Kwasababu bado inaitwa Simba au Yanga?

Case II.
Ikitokea timu imebaki kama ilivyo, ila imebadilishwa jina na jezi. Mfano simba sasa iitwe yanga na wavae jezi za njano. na yanga iitwe simba na wavae jezi nyekundu.

Je, sasa utahama timu kufata jina na jezi?

Kipi hasa kinakufanya uipende timu hiyo?

Je, katika case hizo mbili ipi itakufanya ubadili timu?

Kuna paradox moja ina question uhalisia wa kitu inaongelea kuhusu meli Fulani.

Mfano kuna meli mimi nitaiita "MV NADE". Hii meli imekua ikibadilishwa vifaa kila baada ya muda.

Tuseme mwaka huu imebadilishwa engine, mwakani ikabadilishwa siti n.k

Ikafika kipindi vifaa vyote vilivyokua kwenye MV NADE mwanzo vimebadilishwa.

Je, hiyo meli bado itakua MV NADE?

Na je, vile vifaa vilivyobadilishwa kutoka kwenye MV NADE, vikitumika kuunda meli.

Kati ya meli hii iliyo undwa saivi na ile ya mwanzo ipi ni MV NADE?

Kwahiyo uhalisia wa kitu unatokana na jinsi wewe unavyoki-define.
 
Aisee... Mkuu umeongea kitu cha kufikirisha sana... In case of simba na yanga naweza sema mm nimependa jina "SIMBA" ikiwa ni moja ya mnyama mwenye sifa nyingi za kishujaa mwituni na muonekano wake mzuri kwa ujumla.


Pia nmependa rangi "NYEKUNDU" coz hii pia inatafsiri nyingi tofauti tofauti za kishujaa.

Hivyo team ya Yanga ikibadili jina na kuwa SIMBA, nahama ushabiki
 
Kupenda kitu/ mtu huanzia rohoni na Wala sio kwa macho tu
hata dini uliyopo nadhani ulijikuta kwanza huko kwaajili ya wazazi mazingira n.k
ndo ikaingia rohoni ukaipenda.

ukizaliwa na ukakulia kwenye ukristo utaona ndo upo upande sahihi zaidi na ni ngumu kuhama,

ukizaliwa na ukakulia kwenye uislam utaona pia ndo upo upande sahihi zaidi na ni ngumu kuhama.

kama wewe ni mkristo amini kwamba ungezaliwa kwenye familia ya uislam,

una zaidi ya asilimia 90 kwamba nawe ungekua nawe kwenye uislam na ungeupenda sana tu na ingekua ngumu kubadilishwa,

vilevile kama wew ni muislam amini kwamba ungezaliwa kwenye familia ya ki kristo saivi pia unaasilimia kubwa kwamba nawe ungekua mkristo safi tuu na pia ingekua ngumu kubadilishwa.

kwaiyo mimi naona kitu hakianzii tuu rohoni ila kikiingia rohoni ndo kinakua na mkazo zaidi,
kinakua kimeshafungamana na wewe unaweza kutumia hata kuji define nacho... mimi mkristo, mimi muislam, mimi simba, mimi yanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…