NadeOj
JF-Expert Member
- Mar 25, 2024
- 457
- 863
Umewahi kujiuliza je?
Mfano wewe ni mpenzi wa yanga au simba, ni kwanini unapenda na ni vigumu kubadilishwa mtizamo wako kiasi kwamba hata wazingue kwa kiasi kikubwa bado utazidi kutafuta namna ya kutetea ili uendelee kuipenda.
Kuna case mbili fikiria alafu useme katika case ipi utabadili timu.
Case I.
Ikitokea wachezaji wote wa yanga pamoja na kocha na viongozi waende kuajiriwa simba, Kisha wa simba waende yanga, lakini majina ya timu yabaki hivyo hivyo.
Je, utaendelea kuwa katika timu hiyo Kwasababu bado inaitwa Simba au Yanga?
Case II.
Ikitokea timu imebaki kama ilivyo, ila imebadilishwa jina na jezi. Mfano simba sasa iitwe yanga na wavae jezi za njano. na yanga iitwe simba na wavae jezi nyekundu.
Je, sasa utahama timu kufata jina na jezi?
Kipi hasa kinakufanya uipende timu hiyo?
Je, katika case hizo mbili ipi itakufanya ubadili timu?
Kuna paradox moja ina question uhalisia wa kitu inaongelea kuhusu meli Fulani.
Mfano kuna meli mimi nitaiita "MV NADE". Hii meli imekua ikibadilishwa vifaa kila baada ya muda.
Tuseme mwaka huu imebadilishwa engine, mwakani ikabadilishwa siti n.k
Ikafika kipindi vifaa vyote vilivyokua kwenye MV NADE mwanzo vimebadilishwa.
Je, hiyo meli bado itakua MV NADE?
Na je, vile vifaa vilivyobadilishwa kutoka kwenye MV NADE, vikitumika kuunda meli.
Kati ya meli hii iliyo undwa saivi na ile ya mwanzo ipi ni MV NADE?
Kwahiyo uhalisia wa kitu unatokana na jinsi wewe unavyoki-define.