Mtuhumiwa wa Ubakaji amwambia Mwandishi wa Habari “Afu we Camera man nikimaliza kesi ntakutafuta”

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,591
8,820
Watuhumiwa wanne wa kesi ya Ubakaji na ulawiti ambao ni Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) MT 140105 Clinton Damas maarufu Nyundo, Amini Lema maarufu Kindamba, Nickson Jackson maarufu Machuche na Askari wa Jeshi la Magereza C 1693 Praygod Mushi wakiondolewa mahakamani jioni hii kurudishwa mahabusu mpaka Agosti 28, 2024 ambapo kesi hiyo itaendelea tena.

Nyundo na wenzake wakati wakitoka Mahakamani mmoja wao alisikika akimwambia Cameraman kuwa akifanikiwa kumaliza kesi yao atamtafuta "Wewe cameraman nikimaliza kesi nitakutafuta" Endelea Kufuatilia kurasa Zetu kufahamu Kuhusu kilichojiri Mahakamani kuhusu Kesi hii leo Agosti 23, 2024.

View: https://youtu.be/hLeI2QJ4xJQ?si=LA4rAwG1ap6LfbpR

Kwamba cameraman nae ataomba maji?
 
Ni utovu wa nidhamu wa Hali ya juu sana,kwanza kwa binadamu aliyelelewa ktk maadili mazuri hapo anajua ni kosa kabisa kuingilia kazi ya mtu pia ni wazi Kuna shida katika makuzi ya sasa maana kwa Hali aliyonayo mtuhumiwa angekuwa anajuta. Na pengine kuwa mtu wa sala na toba na pia mtu mtulivu maana ni kwa Nini awe yeye na siyo mtu mwingine,hili Ndo swala la msingi angekuwa anajiuliza.Naisi wazazi wa Leo Kuna sehemu tunakosea,Ina maana akitoka afanye Tena jinai,duh Dunia inapitia pabaya sana.
 
Back
Top Bottom