- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu kumekuwa na hii dhana miongoni mwa watu wengi kuwa mtu akinywa vidonge mfano Panado kisha akaenda kupima UKIMWI atakuwa negative hata kama anao.
Je, ni kweli?
Je, ni kweli?
- Tunachokijua
- Kumekuwepo na madai yanayosambaa Mtandaoni yakibainisha kuwa watu wenye maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) wakimeza dawa za kupunguza maumivu kama panadol, au dawa za antibayotiki muda mfupi kabla ya kuchukua vipimo hupata majibu hasi (negative), yaani huonekana hawana maambukizi.
Mathalani, madai ya Mtumiaji wa Mtandao wa TikTok anayefahamika kama Kanda ya Nduthi ya Februari 2, 2023 yanadokeza kuwa baadhi ya watu hasa wenye VVU hutumia njia hii kuhadaa wengine huku wakijua hali zao kuwa wameambukizwa, hivyo njia sahihi ya kuwakamata ni kutokuwapa kabla taarifa za uchukuaji wa vipimo ili wasimeze dawa hizo.
Mtumiaji mwingine wa Mtandao wa X aliwahi kutoa madai haya Septemba 29, 2022. Tazama hapa.
Ukweli upoje?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini madai haya hayana ukweli. Kwa mujibu wa tume ya Kudhibiti VVU Uganda, madai haya ni miongoni mwa dhana nyingi potoshi zinazozungumzwa na watu kuhusu VVU.
Dawa aina ya panadol, antibayotiki au hata dawa zingine kali kuzidi hizi hazina uwezo wa kufanya kipimo cha VVU kisiweze kutambua uwepo wa kinga mwili (Antibodies). Njia pekee inayoweza kumfanya mwathirika wa VVU afikie hatua ya kuwa nakala chache zisizoweza kuonekana kwenye vipimo ni kupitia matumizi ya dawa za kufubaza virusi, yaani ARV.
Madai haya yaliwahi kukanushwa pia na baadhi ya taasisi za uhakiki ikiwemo Africa Check mwaka 2023.