Mtoto wa mama yangu mdogo anapenda kuiba nguo zangu za ndani

Muzine

JF-Expert Member
May 4, 2017
32,366
60,444
Salama wapendwa?

Naombeni ushauri nifanye nn huyu mdogo wangu ni mtoto wa mama mdogo ameolewa na ana mme ila amekuwa akinikera sana na tabia ya kuniibia nguo zangu za ndani kama chupi na taiti hasa zile mpya au nilizovaa mara moja.

Hii tabia ameanza zamani huu ni mwaka wa 8 .
Toka tunasoma Sekondary tulikuwa tukikutana likizo yeye kazi yake kuiba nguo zangu za ndani na kuzificha sku nikirudi ghafla nazikuta nguo zangu kwake akiwa amefua au zimeshavaliwa na kuchakaa lakini zinakuwa kwenye nguo zake.

Kifupi mm nina tabia ya kununua nguo za ndani kwa dozen hivyo nakuwa nazo nyingi zimejaa na zote nazijua sasa yeye akija tu au nikienda kwake au tukutane nyumbani kwa mama mdogo ujue lazima nitarud na nguo za ndani nusu kumbe huwa anaficha.

Jana nimeshangaa sana baada ya kwenda ghafla nyumbani kwa mama mdogo bila kuwapa taarifa nilivyofika nikapitiliza chumba tunachofikiaga watoto wa kike nakutana na nguo zangu za ndani nilizopoteza.

Nakumbuka nilienda siku moja kwa mama mdogo nikawa nimesahau nimesafir na nguo moja ya ndani kumbe zingine niliziacha kitandani nikasahau kuweka kwenye mkoba hivyo nilivyofika huko ikabidi ninunue nusu dozen ya nguo ya ndani kwa elf 20 .Nilikaa kama siku 5 siku narud nyumban kwangu nikakuta nguo zangu za ndani nilizonunua hazipo 3 maana nusu dozen zinakaa 6.

Jana nimeenda ghafla kwa mama angu mdogo nimezikuta kwa mdogo wangu zikiwa zimetumika alafu rangi za chupi zilizopotea ni hizo hizo 3.

Piah nakumbuka kuna siku nilipita mwenge Dar nikanunua kichupi cha netinet yani resi tupu cha rangi ya udhurungi tena kimojaa tu kizur kilikuwa cha elf 10 nilikuwa njiani naenda kwa Mama angu mdogo kuwasalimia.

Mdogo wangu naye akaja mm wala sikukitoa kwenye mkoba baadae nikarudi zangu Tegeta ile nafika tu Tegeta nilikokuwa nakaa kuangalia kwenye pochi nitoe nikifue hakipo.

Maajabu siku moja nimeenda kwenye ubarikio wa wadogo zetu wa kiume eeeh natafuta Wanja nijipodoe kwenye kabati nikakutana na kakyupi kangu kapo kwenye nguo za mdogo wangu nikabaki nashangaa.

Nimfanye nini huyu ndugu yangu nimevumilia nimechoka sasa?
Hii tabia ya kuniibia kyupi zangu ataacha lini?
Au amezaliwa nayoo?

Kifupi huyu mdogo wangu hana tabia kabisa ya kununua vitu vya gharama na vyupi vyake ni vile vya bukubuku kwahiyo akichukua za kwangu huwa najua tu jamani uvumilivu umenishinda nipo njiapanda naombeni ushauri wenu.
 
Mkuu kama umeshajua tabia yake na umegundua anapenda vitu vizuri ila uwezo hana unonaje ukiwa unampelekea zawadi ya vyupi na hizo taiti kuepuka usumbufu?
Pesaa zangu anakula vya kutosha na mme wake ana kazi gani?

Nimeshamsitiri vya kutosha nataka mbinu mnipe za kumwambia kuhusu tabia yakeee
 
Huyo mdogo anataka tu, kuwa katika daraja flani la maisha ambalo kwa sasa halimudu...

Msapoti kidogo, ukinunua hata 10,
Ukampa 2 sio mbaya

Njaa tu, inamsumbua
Mkuu kwanza siyo tu nimsapot nilimsisitiza sana suala la kusoma aachane na wanaume unajua maisha ya mbagala makundi na vigomaa vimemuharibu na nimeshamsaidia mambo mengi sasa kinachonikera ni tabia ya kubeba nguo zangu za ndani.
 
Ujinga mtupu,
Nonsence!

Ni utoto tu ndio unaokusumbua, pamoja na kutokua na kazi ya kufanya,
Jaribu japo kufuga Kuku,huenda nawe akili yako ikaanza kuwaza vitu vya maana kidogo kuliko huu ujinga ujinga.
 
Ujinga mtupu,
Nonsence!

Ni utoto tu ndio unaokusumbua, pamoja na kutokua na kazi ya kufanya,
Jaribu japo kufuga Kuku,huenda nawe akili yako ikaanza kuwaza vitu vya maana kidogo kuliko huu ujinga ujinga.
Ila The list huwa unanikera muda mwingine si uhamie jukwaa la biashara unanikera wewe unajifanyaga mtu mxeeeew
 
Back
Top Bottom