Mtoto aliyekuwa akiugua ugonjwa wa kubugia mafuta na kilo ya kila siku sukari atibiwa Muhimbili

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059
Mama wa mtoto huyo anadai aliambiwa na madktari kuwa nyama za ndani za mtoto huyo zimekua ngumu sana, na ili kulainisha nyama hizo mtoto huyo ilibidi anywe mafuta mabichi na sukari robo tatu


Asipopata vitu hivyo basi alikuwa anabadilika rangi na kuwa mweupe na njano, alihangaika naye Msumbiji na Malawi lakini hakupata tiba ndipo alionyeshwa kwenye vyombo vya habari na kwenda kutibiwa baada ya kuonekana

Daktari bingwa wa masuala ya Damu aliyemtibu mgonjwa huyo anasema alikuwa na tatizo la seli mundu (sickle cell) amabalo hushambulia chembechembe za damu mwlini na kuharibu bandama na kutengeneza nyongo nyingi mwilini, seli mundu ni gonjwa la kurithi
 
Reactions: SDG
Mungu amfanyie wepesi apone haraka pia waandishi wa habari pamoja na wanaomiliki smart phone wakibahatika kuwaona watu wengine wenye matatizo kama haya washare wenye mitandao ya kijamii ili wenye huruma watoe walichonacho kusaidia
 
Aisee hujafa hujaumbika. Namuombea kwa Mola ampe wepesi
katika matibabu yake.
 
Reactions: SDG
Afadhali kama ugonjwa umegundulika mm nilihisi ni mambo ya Sayansi ya asili
 
Reactions: SDG

Madaktari wetu!!! Big up Muhimbili and Dr Stella Rwezaura.
 
Reactions: SDG
Waafrica wanaweza kuwa wajinga kuliko mnyama yeyote duniani , sasa huyu siku zote alikuwa anatumia mizizi akitegemea nini ?
 
Reactions: SDG
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…