Mtoto (6) mwingine aliyepotea juzi, amekutwa kafariki kwenye jumba bovu. Je, ni kwanini Rais asitangaze hali ya hatari (State of emegency)

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
37,998
44,022
Mtoto Ashfaki Abimu (5) mkazi wa Mbagala Kizuiani jijini Dar es Salaam, amekutwa amefariki dunia katika eneo ya Mbagala Kibonde Maji ndani ya jumba bovu, baada ya kupotea kwa takribani siku tatu akiwa anacheza nje ya nyumba yao ambapo mwili wake umekutwa ukiwa umefanyiwa kitendo cha kikatili.

Akizungumza kwa uchungu, mama wa mtoto huyo ameiomba serikali ibadilishe sheria ya Jeshi la Polisi kuanza kumtafuta mtu aliyepotea baada ya saa 24, kwani anaamini kuwa angewahi kutafutwa mapema basi mwanaye angeweza kuwa hai.

Soma Pia: RC Chalamila: Matukio ya Mauaji na Utekaji Watoto yapo lakini siyo kama yanavyoripitiwa, mengi siyo ya kweli
 
Uwepo wa hizi taarifa tu ni hali ya hatari tosha wazazi waongeze umakini kulinda watoto tatizo suala la ulinzi wa watoto imekua siyo kipaumbele tena kila mtu yuko mbio kutafuta pesa.

Polisi ambao hawafiki hata 50,000 ukiwajumlisha wote na IGP wao hawawezi kulinda kila mtoto sasa we endelea kujenga hoja kwa kusema mbona kukamata wapinzani wanaweza wakati jukumu la ulinzi wa mtoto ni lako mzazi.

Hao polisi hata wakija kumpata mtuhumiwa wala haiwezi kuwa mafanikio ikiwa tayari mtoto wako ameshafanyiwa ukatili au kuuwawa kabisa
 
Natamani siku atekwe mtoto wa waziri au Mbunge yeyote ili wajue maumivu makali wanayopitia wazazi wa hawa watoto.

Hivi hii nchi tuna Usalama wa taifa kweli? Ina maana hadi leo hawajamtambua ni Mganga yupi wa jadi anayeagiza watu wakalete viungo vya watoto? Au nyie wenyewe ndio mnafanya?!

Video ina habari kamili


View: https://www.instagram.com/reel/C-spLwQi9Qz/?igsh=NTc4MTIwNjQ2YQ==

Tatizo kubwa liko kwa wazazi kuacha watoto kuzagaa mitaani bila uangalizi yaani ni kama kuku wa kienyeji
 
Natamani siku atekwe mtoto wa waziri au Mbunge yeyote ili wajue maumivu makali wanayopitia wazazi wa hawa watoto.

Hivi hii nchi tuna Usalama wa taifa kweli? Ina maana hadi leo hawajamtambua ni Mganga yupi wa jadi anayeagiza watu wakalete viungo vya watoto? Au nyie wenyewe ndio mnafanya?!

Video ina habari kamili


View: https://www.instagram.com/reel/C-spLwQi9Qz/?igsh=NTc4MTIwNjQ2YQ==

Hutosikia mtoto wa waziri au kiongozi yoyte katekwa,hizo zinatokea Kwa sisi walala hoi mkuu.
 
Una uhakika mkuu? Nakuombea uzima ili ushuhudie mengi
Tusiombeane hayo bali tuone/tutafakari kwa kina kama hakuna mahali wazazi walizembea. Tusiende na kauli ya eti mtoto alikuwa anacheza nje...Nje wapi? (i.e.Umbali gani kutoka nyumbani alipokuwa anaishi) Matukio ya utekwaji wa watoto yameanza muda mrefu. Je, wazazi hawakujali kuona ipo haja ya kuchukua Tahadhari za makusudi juu ya Usalama wa mtoto wao 6yrs kipindi hiki cha vurumai?
Sheria ya Polisi ni kweli ina udhaifu mkubwa sana kwani anayetakiwa atafutwe baada ya 24hrs nadhani ni kwa mtu mzima na sio kwa mtoto mdogo(Sina uhakika). Lakini hata Polisi nao inafaa watumie akili za kujiongeza/ubinadamu. Kwani wakianza kutafuta kabla ya hizo 24hrs ni kosa?
 
Mbona matukio mabaya kuhusu watoto yanatokea sana na hatusikii tamko?
Aliepita alidhibiti majambazi na yaliuwawa na mengine yakaikimbia nchi
Sasa kama hawa wauwaji na wachawi hawalazwi msitegemee unyama huu kuisha
Natamani waziri wa mambo ya Ndani awe mkali na aitishe press atie neno
 
Tatizo kubwa liko kwa wazazi kuacha watoto kuzagaa mitaani bila uangalizi yaani ni kama kuku wa kienyeji
Kuna mtoto alipotea shuleni Oyester Bay au Masaki.
Shule ya gharama kwa bahati akapatikana Mikumi Morogoro sababu mganga alimkataa hafai kwa mambo yao.
 
Huku ni dereva boda aseee,,jana tu katoka kuzikwa kaokotwa porini huko😢shida tupu
 
Back
Top Bottom