Mtikisiko wa kuvujishwa kwa siri za vigogo kuelekea uchaguzi mkuu 2025

The Supreme Conqueror

JF-Expert Member
Feb 13, 2017
438
1,255
SIRI za baadhi ya vigogo Serikalini zilizofichwa kwa muda mrefu sasa zimeanza kuibuka huku kukiwa na taarifa zinazodai kuwa kundi la mahasimu wa kisiasa wa vigogo hao limepanga kutumia siri hizo kama moja ya kete za turufu za kuwaondoa kwenye ulingo wa mnyukano wa uchaguzi mkuu wa mwakani.

Taarifa zilizopatikana zinadai kuwa wapo vigogo serikali wenye dhamana za kutoa maamuzi ambao uraia wao una utata na kwamba vigogo hao wamewekeza vitega uchumi vyenye thamani ya mabilioni ya shilingi kwenye nchi wanakonasibishwa kuwa na asili ya huko.

Kwa upande mwingine taarifa hizo zinazodai kuwa wapo vigogo ambao wamekuwa wakiwashinikiza watendaji wa mashirika na taasisi za umma kuwachotea mabilioni ya fedha kutoka kwenye mafungu ya matumizi ya kawaida yanayotolewa na hazina kila mwezi na hivyo kukwamisha utekelezaji wa mipango ya taasisi na mashirika hayo.

Inadaiwa kigogo mmoja mwandamizi serikalini (jina lake limehifadhiwa kwa sababu hajazungumza) asili ya wazazi wake ni nchi jirani (jina la nchi nalo tumelihifadhi kwa muda) lakini kwa sababu ameishi hapa nchini kwa muda mrefu, amefanikiwa kugombea na kuchaguliwa kwenye nafasi za uongozi wa kisiasa na kisha aliteuliwa kushika nafasi nyeti serikalini.

Inadaiwa kigogo huyo amewekeza vitega uchumi vyake katika nchi mbili za Afrika Mashariki huku ikitajwa zaidi hoteli aliyojenga kwenye moja ya nchi hizo kwa kutumia fedha alizochuma hapa nchini.

Taarifa kutoka kwa watu walio karibu na kigogo huyo zinadai kuwa alianza kujenga hoteli yake hiyo wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano na baadhi ya viongozi wa juu wa wakati huo waliokuwa karibu naye walijua kuhusu ujenzi wa hoteli hiyo pamoja na vitenga uchumi vyake vingine vilivyopo nchi jirani.

Kwamba ujenzi wa hoteli ya kigogo huyo umesimamiwa na mjomba wake ambaye anaishi nchi hiyo jirani na ambaye huwa anafika hapa nchini kukutana naye.

Inadaiwa, fedha za ujenzi wa hoteli hiyo zimekuwa zikichotwa serikalini tangu wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano na kutoroshwa kwa njia za panya kwenda kugharamia pamoja na miradi yake mingine nje ya nchi, mradi wa ujenzi wa hoteli hiyo.

Madai hayo yanakwenda mbali zaidi yakimtaja aliyepata kuwa kiongozi mkubwa hapa nchini, (jina kapuni) wa Serikali ya Awamu ya Tano kuwa alikuwa mbia wake katika ujenzi wa hoteli hiyo na kwamba kiongozi huyo anamfahamu mjomba wa kigogo huyo anayesimamia hoteli hiyo nje ya nchi.

Inadaiwa kiongozi huyo aliufahamu ukoo wa marehemu mama wa kigogo huyo ambao asili yake ni nchi jirani na alipata kukutana na mjomba wa kigogo huyo alipofika nchini kwa ajili ya kuchukua fedha za kwenda kugharamia uwekezaji unaofanywa na kijana wake nje ya nchi.
Haya yanaanza kubainika baada ya tabriban miezi saba sasa tangu Mkuu wa Majeshi, Jenerali Jacob Mkunda aliposema kuna baadhi ya waomba hifadhi na wakimbizi wameajiriwa na kuteuliwa katika nafasi mbalimbali serikalini jambo ambalo ni tishio kwa usalama.

Jenerali Mkunda alitoa kauli hiyo jumatatu, Januari 22, 2024 kwenye mkutano wa saba wa Mkuu wa Majeshi na makamanda uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwepo kwa muda mrefu kwa waomba hifadhi na wakimbizi ni tishio la kiusalama kwa kuwa baadhi yao au familia zao wameajiriwa na wengine wamepewa teuzi serikalini katika nafasi za kutoa maamuzi.

Pia soma: Nabii Sanga: Mgawanyiko mkubwa utaikumba CCM mwaka 2024 na 2025, tuiombee

Pia soma:

Hiyo ipo wazi. Huyo anayeongelewa, kama ndiye huyu tunayemfahamu, wakati akiishikilia wizara, aliwajaza ndugu zake kutoka nchini kwake, kwenye maeneo yenye dhahabu, tena kwa kuwanyang'anya maeneo hayo watanzania asilia. Na mpaka sasa wanatamba kwenye biashara ya madini.

Lakini wajumvi wa mambo wanasema kuwa licha ya kila kitu kufahamika, mbinu yake ya kugawa pesa kwa wanafamilia wa jumba kuu kulimsaidia kuendelea kubakia kwenye uongozi hadi kufikia kuundiwa nafasi ambayo haipo kikatiba.
 
Doto Biteko ameituliza sana wizara ya nishati iliyokuwa imeharibiwa vibaya kwa ufisadi na January Makamba. Foleni za kugombea mafuta hazionekani tena pia upatikanaji wa umeme umeimarika mno.

Kama kuwa na wajomba nje ya nchi ni kosa hata Rais Samia ana wajomba Dubai na amewagawia bandari zote za Tanganyika.
 
Hiyo ipo wazi. Huyo anayeongelewa, kama ndiye huyu tunayemfahamu, wakati akiishikilia wizara, aliwajaza ndugu zake kutoka nchini kwake, kwenye maeneo yenye dhahabu, tena kwa kuwanyang'anya maeneo hayo watanzania asilia. Na mpaka sasa wanatamba kwenye biashara ya madini.

Lakini wajumvi wa mambo wanasema kuwa licha ya kila kitu kufahamika, mbinu yake ya kugawa pesa kwa wanafamilia wa jumba kuu kulimsaidia kuendelea kubakia kwenye uongozi hadi kufikia kuundiwa nafasi ambayo haipo kikatiba.
Mbona kama anayeongelewa ni Dotto Biteko?
 
SIRI za baadhi ya vigogo serikalini zilizofichwa kwa muda mrefu sasa zimeanza kuibuka huku kukiwa na taarifa zinazodai kuwa kundi la mahasimu wa kisiasa wa vigogo hao limepanga kutumia siri hizo kama moja ya kete za turufu za kuwaondoa kwenye ulingo wa mnyukano wa uchaguzi mkuu wa mwakani.

Taarifa zilizopatikana zinadai kuwa wapo vigogo serikali wenye dhamana za kutoa maamuzi ambao uraia wao una utata na kwamba vigogo hao wamewekeza vitega uchumi vyenye thamani ya mabilioni ya shilingi kwenye nchi wanakonasibishwa kuwa na asili ya huko.

Kwa upande mwingine taarifa hizo zinazodai kuwa wapo vigogo ambao wamekuwa wakiwashinikiza watendaji wa mashirika na taasisi za umma kuwachotea mabilioni ya fedha kutoka kwenye mafungu ya matumizi ya kawaida yanayotolewa na hazina kila mwezi na hivyo kukwamisha utekelezaji wa mipango ya taasisi na mashirika hayo.

Inadaiwa kigogo mmoja mwandamizi serikalini (jina lake limehifadhiwa kwa sababu hajazungumza) asili ya wazazi wake ni nchi jirani (jina la nchi nalo tumelihifadhi kwa muda) lakini kwa sababu ameishi hapa nchini kwa muda mrefu, amefanikiwa kugombea na kuchaguliwa kwenye nafasi za uongozi wa kisiasa na kisha aliteuliwa kushika nafasi nyeti serikalini.

Inadaiwa kigogo huyo amewekeza vitega uchumi vyake katika nchi mbili za Afrika Mashariki huku ikitajwa zaidi hoteli aliyojenga kwenye moja ya nchi hizo kwa kutumia fedha alizochuma hapa nchini.

Taarifa kutoka kwa watu walio karibu na kigogo huyo zinadai kuwa alianza kujenga hoteli yake hiyo wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano na baadhi ya viongozi wa juu wa wakati huo waliokuwa karibu naye walijua kuhusu ujenzi wa hoteli hiyo pamoja na vitenga uchumi vyake vingine vilivyopo nchi jirani.

Kwamba ujenzi wa hoteli ya kigogo huyo umesimamiwa na mjomba wake ambaye anaishi nchi hiyo jirani na ambaye huwa anafika hapa nchini kukutana naye.

Inadaiwa, fedha za ujenzi wa hoteli hiyo zimekuwa zikichotwa serikalini tangu wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano na kutoroshwa kwa njia za panya kwenda kugharamia pamoja na miradi yake mingine nje ya nchi, mradi wa ujenzi wa hoteli hiyo.

Madai hayo yanakwenda mbali zaidi yakimtaja aliyepata kuwa kiongozi mkubwa hapa nchini, (jina kapuni) wa Serikali ya Awamu ya Tano kuwa alikuwa mbia wake katika ujenzi wa hoteli hiyo na kwamba kiongozi huyo anamfahamu mjomba wa kigogo huyo anayesimamia hoteli hiyo nje ya nchi.

Inadaiwa kiongozi huyo aliufahamu ukoo wa marehemu mama wa kigogo huyo ambao asili yake ni nchi jirani na alipata kukutana na mjomba wa kigogo huyo alipofika nchini kwa ajili ya kuchukua fedha za kwenda kugharamia uwekezaji unaofanywa na kijana wake nje ya nchi.
Haya yanaanza kubainika baada ya tabriban miezi saba sasa tangu Mkuu wa Majeshi, Jenerali Jacob Mkunda aliposema kuna baadhi ya waomba hifadhi na wakimbizi wameajiriwa na kuteuliwa katika nafasi mbalimbali serikalini jambo ambalo ni tishio kwa usalama.

Jenerali Mkunda alitoa kauli hiyo jumatatu, Januari 22, 2024 kwenye mkutano wa saba wa Mkuu wa Majeshi na makamanda uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwepo kwa muda mrefu kwa waomba hifadhi na wakimbizi ni tishio la kiusalama kwa kuwa baadhi yao au familia zao wameajiriwa na wengine wamepewa teuzi serikalini katika nafasi za kutoa maamuzi.

Pia soma: Nabii Sanga: Mgawanyiko mkubwa utaikumba CCM mwaka 2024 na 2025, tuiombee
2025 Rais ni mmoja tu Mama Samia
 
Sikio la kufa halisikii dawa. Namba 2 na namba 4 uraia wao unamashaka. Japo namba 2 ni mwadilifu sana.

Namba moja uzalendo wake unamashaka vilevile, anajiona wa uarabuni.

Mzalendo pekee ni namba tatu, naye anapigwa vita kwa sababu ya uadilifu wake. Si hatari hiyo?
 
Mmh!
Ukiwa mwanasiasa unatakiwa kuwa mvumilivu sana
 
Kama umeamua kuficha jina la muhusika ungeweka wazi nchi anayohusishwa nayo.
Vnginevyo katika siku hizi za kuelekea uchaguzi serikali kupitia vyombo vyake itangze hadharani watanzania wenye uraia wa mashaka ili wajiweke mbali na nafasi za kuchaguliwa.
 
Hiyo ipo wazi. Huyo anayeongelewa, kama ndiye huyu tunayemfahamu, wakati akiishikilia wizara, aliwajaza ndugu zake kutoka nchini kwake, kwenye maeneo yenye dhahabu, tena kwa kuwanyang'anya maeneo hayo watanzania asilia. Na mpaka sasa wanatamba kwenye biashara ya madini.

Lakini wajumvi wa mambo wanasema kuwa licha ya kila kitu kufahamika, mbinu yake ya kugawa pesa kwa wanafamilia wa jumba kuu kulimsaidia kuendelea kubakia kwenye uongozi hadi kufikia kuundiwa nafasi ambayo haipo kikatiba.
Unajihangaisha bure.
 
SIRI za baadhi ya vigogo Serikalini zilizofichwa kwa muda mrefu sasa zimeanza kuibuka huku kukiwa na taarifa zinazodai kuwa kundi la mahasimu wa kisiasa wa vigogo hao limepanga kutumia siri hizo kama moja ya kete za turufu za kuwaondoa kwenye ulingo wa mnyukano wa uchaguzi mkuu wa mwakani.

Taarifa zilizopatikana zinadai kuwa wapo vigogo serikali wenye dhamana za kutoa maamuzi ambao uraia wao una utata na kwamba vigogo hao wamewekeza vitega uchumi vyenye thamani ya mabilioni ya shilingi kwenye nchi wanakonasibishwa kuwa na asili ya huko.

Kwa upande mwingine taarifa hizo zinazodai kuwa wapo vigogo ambao wamekuwa wakiwashinikiza watendaji wa mashirika na taasisi za umma kuwachotea mabilioni ya fedha kutoka kwenye mafungu ya matumizi ya kawaida yanayotolewa na hazina kila mwezi na hivyo kukwamisha utekelezaji wa mipango ya taasisi na mashirika hayo.

Inadaiwa kigogo mmoja mwandamizi serikalini (jina lake limehifadhiwa kwa sababu hajazungumza) asili ya wazazi wake ni nchi jirani (jina la nchi nalo tumelihifadhi kwa muda) lakini kwa sababu ameishi hapa nchini kwa muda mrefu, amefanikiwa kugombea na kuchaguliwa kwenye nafasi za uongozi wa kisiasa na kisha aliteuliwa kushika nafasi nyeti serikalini.

Inadaiwa kigogo huyo amewekeza vitega uchumi vyake katika nchi mbili za Afrika Mashariki huku ikitajwa zaidi hoteli aliyojenga kwenye moja ya nchi hizo kwa kutumia fedha alizochuma hapa nchini.

Taarifa kutoka kwa watu walio karibu na kigogo huyo zinadai kuwa alianza kujenga hoteli yake hiyo wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano na baadhi ya viongozi wa juu wa wakati huo waliokuwa karibu naye walijua kuhusu ujenzi wa hoteli hiyo pamoja na vitenga uchumi vyake vingine vilivyopo nchi jirani.

Kwamba ujenzi wa hoteli ya kigogo huyo umesimamiwa na mjomba wake ambaye anaishi nchi hiyo jirani na ambaye huwa anafika hapa nchini kukutana naye.

Inadaiwa, fedha za ujenzi wa hoteli hiyo zimekuwa zikichotwa serikalini tangu wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Tano na kutoroshwa kwa njia za panya kwenda kugharamia pamoja na miradi yake mingine nje ya nchi, mradi wa ujenzi wa hoteli hiyo.

Madai hayo yanakwenda mbali zaidi yakimtaja aliyepata kuwa kiongozi mkubwa hapa nchini, (jina kapuni) wa Serikali ya Awamu ya Tano kuwa alikuwa mbia wake katika ujenzi wa hoteli hiyo na kwamba kiongozi huyo anamfahamu mjomba wa kigogo huyo anayesimamia hoteli hiyo nje ya nchi.

Inadaiwa kiongozi huyo aliufahamu ukoo wa marehemu mama wa kigogo huyo ambao asili yake ni nchi jirani na alipata kukutana na mjomba wa kigogo huyo alipofika nchini kwa ajili ya kuchukua fedha za kwenda kugharamia uwekezaji unaofanywa na kijana wake nje ya nchi.
Haya yanaanza kubainika baada ya tabriban miezi saba sasa tangu Mkuu wa Majeshi, Jenerali Jacob Mkunda aliposema kuna baadhi ya waomba hifadhi na wakimbizi wameajiriwa na kuteuliwa katika nafasi mbalimbali serikalini jambo ambalo ni tishio kwa usalama.

Jenerali Mkunda alitoa kauli hiyo jumatatu, Januari 22, 2024 kwenye mkutano wa saba wa Mkuu wa Majeshi na makamanda uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Alisema kuwepo kwa muda mrefu kwa waomba hifadhi na wakimbizi ni tishio la kiusalama kwa kuwa baadhi yao au familia zao wameajiriwa na wengine wamepewa teuzi serikalini katika nafasi za kutoa maamuzi.

Pia soma: Nabii Sanga: Mgawanyiko mkubwa utaikumba CCM mwaka 2024 na 2025, tuiombee
Hao mnawasingizia tu.
MHARIFU NAMBA MOJA HAPA TANGANYIKA NI ccm.
 
Back
Top Bottom