DOKEZO Mtendaji wa Mtaa Halmashauri ya Mji Njombe analazimisha Mgao wa Pesa za Mikopo ya Asilimia 10 ya vikundi vya Wanawake,Vijana na Walemavu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Habari Mimi ni kijana nipo Njombe Mjini, Hivi Karibuni Halmashauri ya Mji wa Njombe ilitoa Mikopo Kwa vikundi vya wanawake,Vijana na watu wenye ulemavu zaidi ya Billion 1.8, Kikundi chetu Cha vijana tulipokea zaidi ya Milioni 30

Mchakato wa kupata mkopo wa Halmashauri huwa unapitia kwa mtendaji wa mtaa Ili apitishe na kututambua kama vijana tunaofanya shughuli za Ujasiliamali kwenye mtaa wake.

Lakini Cha kushanganza hadi naandika hapa ni kwamba Mmoja wa Watendaji wa mtaa hapa Njombe analazimisha tumpatie Milioni 10 kama Posho ya kutusaidia kupitisha mkopo Wetu. Amekuwa akiwatukana na kuwatishia viongozi wa kikundi ili wakati mwingine tusipate tena.

Kwa idadi yetu hata kama tungegawana hatuwezi kupata hata Milioni 3 kila mmoja , na hizi pesa tuliandikia mradi wa kikundi.

Sasa amesababisha Kikundi tupo Njipanda hatujui tufanye nini anatishia hadi kuturoga,tumeamua kukaa kimya na Pesa bado zipo banki na hatujua tuende kulalamika kwa nani.

Nashauri Mkurugenzi afanye uchunguzi kwa hawa watendaji wa mitaa na vijiji kwasababu wanakwamisha ndoto za vijana

Mwisho wa siku marejesho tunatakiwa kufanya sisi, tukimpatia hiyo Milioni 10 manakae hatuwezi kufanyia shughuli yoyote na hii pesa itapotea bila kufanya kazi.

Mhusika ni Mtendaji wa Mtaa mmoja upo Njombe Mjini,Naomba unisaidie kupaza Sauti ,Nimeficha jina lake Ili ujumbe huu ukimfikia aache hiyo tabia mara moja mana anahatarisha na Kazi yake.
 

Attachments

  • Screenshot_20250208-102253_Instagram.jpg
    297.4 KB · Views: 2
Hivi Pesa za moto hawatoi sikuizi Takukuru.!!
Mnasubiri nini Hamna Takukuru Njombe?
 
Taja huo mtaa na jina kabisa la huyo mtendaji

Mkurugenzi hawezi poteza muda kuangalia mitaa yotee

Wewe mumbeya tu unashindwa nini kuanika wazi taarifa? Zipeleke hata kwa Mkurugenzi kama ushahidi unao

Wewe utakuwa na kikundi hewa wewe
 
Huko hakuna ofisi ya TAKuKURU?
 
umaskini umetufanya hata tunashindwa fikiri vyema, mtendaji mmoja anawashinda vijana zaidi ya 20

bado anawatishia kuwaroga mnamwangalia tu
 
Warasimu, wabadhirifu, wabaguzi, wala rushwa, wanao tumia madaraka yao vibaya.
Wote hawa ndio waimbaji wa kuu wa mama kafanya hivi mama kafanya vile.
Kwenye kila sentensi lazima jina la smaia liwepo, ANGALIA MATENDO YAO SASA!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…