Papaa Muu
JF-Expert Member
- Nov 6, 2018
- 243
- 292
*Utangulizi.*
Serikali ya Tanzania imesitisha mkataba wa mradi wa Ukanda Maalumu wa Kiuchumi wa Bagamoyo wenye thamani ya Dola Billioni 10.
Mradi huu umesitishwa kwa sababu Serikali ya Tanzania imeona kuwa baadhi ya masharti hayana maslahi kwa Taifa. Masharti hayo ni mwekezaji kupanga tozo wenyewe na kwamba serikali isikaribishe mwekezaji mwingine kuwekeza kuanzia upwa wa Tanga hadi Bagamoyo. Majadiliano hayo yalifanywa na kampuni ya China Merchant Holding Inter. ya China na State General ya Oman.
Tuchukue fursa hii kuipongeza sana Serikali ya Tanzania chini ya Dkt John P Magufuli kwa kuweka mbele maslahi ya Taifa. Ni hakika kuwa maslahi kama haya yangewekwa huko nyuma basi Tanzania ingenufaika na sekta nyingi za Kiuchumi kama vile Madini, Utalii na Bandari.
Historia ya mahusiano ya China na Afrika inachagizwa zaidi na Mkutano wa Bandung wa mwaka 1955 ambao unahesabiwa kama mkutano uliokuza mahusiano ya China na Afrika ambapo China ilikua ikitoa msaada wa kimaendeleo katika juhudi za kupambana na ukoloni mkongwe na ukoloni mambo-leo. Bodomo, A (2009).
Hata hivyo, mwanzoni mwa miaka ya 2000 China ilianza mahusiano ya biashara na Africa kwa kiwango kikubwa tofauti na miaka ya 1980.
Mwaka 1980 biashara ya China na Afrika ilikua Dola Billioni 1. Mwaka 2012 ilikua Dola Billioni 163.9. Kufikia mwaka 2017 hadi sasa biashara kati ya China na Africa inakua kwa asilimia 17% kila mwaka. Aidha ni kweli kwamba mahusiano haya ya kibiashara ni mazuri isipokuwa hayana mizania sawa. (Esposito M, 2015)
*Mikataba ya Ulaghai Iliyoiponza Tanzania toka Enzi za Karls Peters ipo Mingi sasa tulitarajia baada ya Uhuru na hasa kipindi hiki Waafrika wenzetu wawe chachu ya kung’amua kuandamizaji aina yoyote. Vita hii si ya Rais Magufuli pekee yake. Ndio maana Fanon F aliandika kitabu Kwa anuani “ The Black Skin White Marsk akitusema weusi tuliokengeuka na kuwa tayari kujilimbikizia mali. Tunarudia kuwa vita ya Kiuchumi asiachiwee Mh Rais Pekee yake, Kila Muhimili una wajibu wa kujipambanua vizri katika vita hii*
Ujumbe wa Taifa la ujerumani uliongozwa na Karl Peters na Dr. Karl Juhlke, Pfeil na August Otto ulikutana na Chifu Magungo katika ikulu ya Msovero eneo la Usagara ambapo Karl Peters na wenzake walitumia ulagha, ujanja na hila kuingia mkataba na Chifu huyo. Mkataba huo ulilenga kukabidhi eneo la Tanganyika lote na watu wake kwa Taifa la ujerumani. Leo bado kuwa watu Kwa rushwa na hila zao wanatamani Tanzania iuzwe. ( Ole wenu).
Misingi ya mahusiano ya kidiplomasia ya siasa na uchumi huwekwa katika mikataba baina ya nchi na nchi au nchi na wawekezaji. Mfano kwa kwanza, Jinamizi la mikataba mibovu katika sekta ya nishati na madini imeliingiza Taifa hili katika hasara kubwa ya kuhakikisha nishati na madini inakuwa rasilimali isiyo na tija Kwa Taifa. Leo hii Dkt Magufuli ameanza kwa kasi kulinda na kutetea rasilimali madini ili iwe na tija Kwa taifa. Akifanya hvy bado kuwa watu walimshangaaa, wakampinga, wakamkejelii tena Kwa rushwa na hila na uzandiki. Mikataba iliyoingiwa Tanesco na IPTL ni mifano michache ya mikataba inavyoiponza Tanzania na ambayo iliingiwa na wasomi walioaminiwa na Taifa letu. Inasikitisha sana.
Rais John P. Magufuli amefanikiwa sana kuongeza umakini katika eneo zima la mikataba kuliko awamu zingine zote na kuhakikisha rasilimali za Taifa zinawanufaisha watanzania. Rejea ripoti ya kamati ya Osoro na marekebisho mbalimbali ya sheria tangu 2016 hadi leo. Pamoja na Kamati au Tume zingine alizoundaa ili kuhakikisha Mtanzania ananufaika. Ndio maana leo vituo vya afya, barabara viwanja vya Ndege, ndege, Mafao Kwa wastaafu, vyote vinaendelea Kwa kasi kubwa.
Mfano wa pili, Sekta tu ya madini kwa Mkoa wa Mbeya wilaya ya Chunya pekee yake, tangu tufungue soko la Madini hatujawahi kuuza chini ya Gram 2000... yaan kila siku tunauza zaidi ya milioni 295 kwa siku ambapo mauzo hayo yalikua mauzo ya miezi zaidi ya kumi kabla ya uwepo wa soko. Swali la wazi, Je asingelikuwa Rais Magufuli kutufumbua macho nani angetuamsha??. Labda wataalamu wa Madini wangetuamsha au wangetufanya tusinzie zaidi...huo ni Mfano tu wa dhamira njema ya Serikali hii ya awamu ya tano. Watanzania twende taratibu mtaelewa vema nani ni mtetezi na nani ni mwizi mla rushwa na Mzandiki wa Taifa hiliii.
*Kusitisha Mkataba siyo Kukataa Mradi*
Serikali ya Tanzania kupitia kwa waziri mwenye dhamana alisema kuwa Tanzania imesitisha mradi kwa sababu ya kutofautiana kwenye baadhi ya masharti (tumeshayataja hapo juu) hata hivyo ipo tayari kuhuisha majadiliano ikiwa wawekezaji wabia watakua tayari kukubaliana na masharti yaliyotolewa na Serikali ya Tanzania.
Aidha mwisho wa siku unaweza kuwa na Bandari ambayo haitaweza kuinufaisha Tanzania na Taifa Kwa ujumla kama tulivyoibiwa kwa miaka mingi kwenye sekta ya madini.
Iwe ni muda muafaka kutarihi mifano kadhaa iliyojitokeza katika mataifa anuai. Mwaka jana Bandari ya Hambatonta nchini Sri-Lanka imechukuliwa na Wachina kwa miaka 99 baada ya Serikali ya Sri-Lanka kushindwa kulipa deni la ujenzi wa Bandari hiyo. Mfano huu tuuangaliee kwa jicho la uchambuzi linganifu (comparative analysis) na Taifa letu kama tu serikali ingeingia katika mkataba usiokua na tija kwa Taifa.
Utekelezaji wa miradi mingi ya ujenzi ni ufadhili toka sehemu mbalimbali nchini au nje ya Taifa letu. Miradi hiyo ama ni mikopo au vinginevyo. Data jarabati ( empirical data) zinaonesha wazi kuwa kwa kiasi kikubwa miradi mikubwa ya ujenzi katika nchi za Afrika inafadhiliwa na mataifa makubwa na kujengwa na kampuni zinazomilikiwa na serikali ya watu wa China - China Ocean Shipping Company na China Merchants Group.
Kama ilivyokuwa wakati ule wa ukoloni, Mataifa makubwa yalihangaika kuuhudumia mfumo wa kibepari na kibeberu kwa kuhakikisha wanainyonya Afrika na kuitawala kisiasa, kiuchumi na hata kidiplomasia. Kumbe, leo China imeweka dango na rajua ( vision and mission) ambayo inalenga kukuza uchumi wa Taifa hilo na ikibidi kuwa hegemony wa uchumi wa Dunia. Katika kufikia Lengo hilo China imeendelea kuimarisha biashara na Afrika kwa kiwango kikubwa kwa kuchukua mali-ghafi kisha kuzichakata na kuzirudisha Afrika tena kama bidhaa za viwandani licha ya kubadili approach yao kwenye Capital Export. Leo Lao wala sio baya kama sisi Watanzania tutakuwa na nia njema.
Tukirudi nyuma kidogo katika historia yetu utakumbuka kuwa haya ndiyo yalikua malengo ya ukoloni mkongwe na sasa ukoloni mambo leo wa kiuchumi. "Colonialism under debt-trap diplomacy"
Tahariri ya Jarida la Trumpet imeielezea Kenya kama mnufaika lakini pia kama muathirika wa miradi ya aina kama huu ambao Serikali ya Tanzania imejipa muda wa kutafakari kwa maslahi ya umma wote bila
Kujali vyama vyetu. Kwamba Kenya wako mbioni kuikabidhi China Exim Bank Bandari ya Mombasa kwa kushindwa kulipa deni la mradi wa SGR waliokopa kutoka Benki hiyo takribani Dola Billioni 4.9. Pengine tutumie muda kdg kuwakumbusha kuwa Rais Magufuli hufanya maamuzi ambayo Tanzania Inapona. SGR inayojengwa TANZANIA leo inajengwa Kwa pesa kdg kuliko ile inayotumika nchi jiran ya Kenya. Ubora ni ule ule na ufanisi ni ule ule.
Maamuzi yanayolenga kuinufaisha nchi ni maamuzi ambayo hayafanywi na yoyote aitwaye kiongozi, mara zote hufanywa na wazalendo wa kweli wenye hofu ya Mungu kama Dkt Magufuli. Kilichotokea kukwamisha maendeleo ya nchi nyingi za Kiafrika ni rushwa ambayo ilikuwa inafanywa kwa conspiracy kati ya viongoz wa serikali baadhi na wahisani, wakopeshaji, wajenzi, nk. Hakuna kitu chochote katika Uchumi ambacho hutokea Kwa bahati mbaya. Vingi huwa ni mipango kati ya walioaminiwa na majangili wa kibeberu ambao kwa miaka mingi wametumia furusa hiyo. Rejea kitabu cha Makuadi wa Soko Huria cha Hayati Prof Chachage.
Pia Tujifunze kutoka Sri-Lanka ambao wamekubali kuikabidhii China bandari yao kwa miaka 99. Ndg zangu hebu tafakarini miaka 99 ni lini?. Bandari iliyo ndani ya nchi yako inakuwa mali ya mwingine Kwa miongo 10 yaan Karne moja. Ndio mnavyotaka Kwa Tanzania??? Ndg zangu Watanzania tunaomba sana tulienii sana na elewenii dhamira ya Rais Magufulii Kwa Tanzania. Wapo wezi, wala rushwa wameanza kuropoka na kubezaa yaliyotokea. Plz plz wapuuzeni pengine wanatumiwaaaa
Pamoja Mfano huo hebu tu jifunze tena kutoka zambia ambao wachina wanachukua Shirika lao la Utangazaji na Airport kutokana na mikataba iliyoingiwa. Sasa sijui watakuwa wanatangaza the beauty of Zambia in Zambia au the beauty of China in Zambia???
Kitendo cha serikali ya Tanzania kusitisha mkataba kwenye mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kwa sababu mkataba hauna maslahi kwa Taifa siyo UOGA bali ni uchungu kwa Kizazi cha Tanzania na maslahi mapana ya Taifa kwa kizazi kijacho.
Mikataba ya namna hii katika sekta ya madini ndiyo imefilisi Taifa letu. Sekta ya Madini Kwa baadhi ya maeneo yamebaki mashimo tu. Ulichonufaika nacho ni kujengewa vyoo kwenye baadhi ya shule . Mfano wakazi wa Nyamongo Tanzania wameshuhudia ujenzi wa matundu ya vyoo, madarasa unaofanywa na BARRICK kwamba ndio manufaaa ya mgodi ukiacha mirabaha.
Hii ni mikataba ambayo watu wenye Mamlaka wakiwemo Mawaziri walioaminiwa walikuwa wanamfuata mwekezaji Hotelini na kusaini mkataba ambao hauna tija kwa taifa lakini wenye tija Kwa familia zao. Rejea kilichotokea Buzwagi.
Huu mtindo wa baadhi ya viongozi wetu kupewa lunch halafu kufanyiwa audio-visual presentation ndiyo ilimfanya Robert Mugabe kuingia mkataba na wachina mwaka 2014 ambao kiasi cha fedha hakikuwahi kuwa na tija au manufaaa kwa umma. Kwa nini leo Rais Magufuli anahangaika kuitindua nchi ambayo ilingozwa na wasomi Kwa miongo mingi tangu uhuru. Nafasi ya Msomi yoyote aliyeamimiwa tangu miaka yote hasa baaada ya Mwl Nyerere ilikuwa wapi. Mikataba kama hiyoo kwanini ilisainiwa bila kuangalia Mstakabali wa leo na kesho wa taifa letu??? Makosa hayo yalifanywa na nani? Kwa nini hawakugundua kasoro za kimikataba???Je Agenda yao ilikuwa ni nini??? Leo hii Mh Magufuli anafanya kosa au anapatia???? Kila mmoja achungulie nafsi yake na umadhubuti wa roho yake katika kulitumia Taifa.
Tunamsifu Rais Magufulii hadharani lakini vifichoni hatuchezi Kwa dhamira nia yake na malengo yake katika kumtumikia masikini wa Tanzania. Unafiki kama huu ni janga Sugu sana Kwa wazawa. Tumuunge Mkono Kwa maslahi ya wenzetu maskini na future ya Taifa letu Kwa Ujumla. Tusijitazame sisi tu, tulitazame Taifa na vizazi vijavyo. Bunge, serikali, na mahakama Ndio mihimili Mama ya Taifa. Mtuwakilishe vema Kwa kuiponya Tanzania. Mambo yanayofanywa na Rais Magufuli huenda yalishindikana hapo kale Kwa sababu dhamira ilikuwa kujinufaisha Kwannza ndiooo walikumbuke Taifa na Masikini wa Tanzania. Pengine kuna watu wamelishwa pesa za rushwa, pengine kuna madalal ambao waliwahiidi Wachina kuwa mkataba utapita bila kupingwa, pengine hela walizopewa zililenga kuuza Tanzania, tunahitimisha Kwa kusema pesa hizo kama ni kweli basi mlikunywa maji ya Betri. Nia ovu imegonga Mwamba.
Dady Igogo- Mhadhiri Msaidizi RUCU Iringa & Albert Chalamila RC Mbeya