Mtazamo wangu kwa Flora (Mbasha) kufunga ndoa ya pili

baba anjela

JF-Expert Member
Mar 17, 2013
431
310
Kwa mtazamo wangu Flora kufunga ndoa ya pili yuko sahihi kabisa...hila yuko sahihi kwa mtazamo wake yeye mwenyewe.

Ila kwa mtazamo wa wakristu ni kosa kubwa, Flora umetibu mwili tu.. Na mwili siku zote ndiyo chanzo cha kwenda kinyume na maisha matakatifu...
Wafilipi 4:13 nayaweza yote katika yeye anitiaye nguvu..
Swali langu ...flora umeyaweza kupitia nani??

Wakati umekwenda kinyume na yeye atupaye nguvu ( Yesu)

Flora unawafundisha nini wengine....Wagalatia 2:14 walakini nilipoona ya kuwa njia yao haiendi sawasawa na ile ya injili , nalimwambia Kefa mbele ya wote, ikiwa wewe myaudi wafuata desturi za mataifa(watu ambao hawaja mpokea yesu) wala si wayaudi,kwa nini unawashurutisha mataifa kufuata desturi za wayaudi...

Ufunuo wa Yohana 2:26 na yeye ashindaye ,na kuyatunza matendo yangu hata mwisho ,nitampa mamlaka juu ya mataifa....Flora mbona umetupa hazina .

1Yohana 4:6 sisi twatokana na mungu .yeye amjuaye Mungu atusikia .yeye asiyetokana na mungu hatusikii.katika hili twamjua Roho wa kweli n Roho wa upotevu...Je Flora umeongozwa na roho wa kweli au wa upotevu?.??

Waefeso 5:11 wala msishirikiane na matendo yanayozaa giza,bali myakemee... Flora utaweza kuyakemea ....???

Mathayo19:5 akasema kwa sbb hiyo .mtu atamwacha babaye na mamaye ,ataambatana na mkewe ,na hao watakuwa mwili mmoja ..basi aliowaunganisha mungu,mwanadamu asiwatenganishe.

Pia Mungu amekataza kabisa mke asiachane na mumewe na mume asiachane na mkewe na endapo wataachana na wakae vivyo hivyo bila kuoa wala kuolewa... 1KORINTHO 7:10-11

... Ufunuo wa yohana 2:4 Basi kumbuka ni wapi ulikoanguka ,ukatubu,ukayafanye matendo ya kwanza...lakini usipofanya hivyo,naja kwako ,nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake.. USIPOTUBUU.
 
Ingekua mbasha ndio kaoa tena watu wangempongeza na kumuita jembe na mistari ya biblia tusingeiona hapa ila kisa flora ni mwanamke basi mnamtungia majina yenu khaa wivu mbaya wakuu.
Hapo kwenye suti ya blue, huyo ni binti wa flora na e mbasha

Kwa hii picha ya bwana harusi hapo nguo ya blue(suti) wacha tu flora azuzuke
 

Attachments

  • 18160392_1450345641695397_8947746393284411392_n.jpg
    119.3 KB · Views: 309
Waimbaji na wahubiri wengi huwa wanawahubiri wengine lakini wao hawajihubiri wenyewe.

Kwa mfano ni kwa Frola mwenyewe aliimba wimbo Fulani unaohusu majaribu kwa kusema kuwa jipe moyo utayashinda.

Kipindi cha majaribu kilipomjia kipindi ambacho alitakiwa kuonyesha mfano kwa matendo kwa kujipa moyo na kusimama ndipo alipojiona kuwa hiyo ndiyo fursa yake ya kukimbia.

Kwa kuwa waimbaji na wahubiri wengi Mara nyingi wamejikita kuwahubiria wengine kwa kuwachukulia kuwa wao ndio watenda dhambi wakati wao wenyewe Wako kinyume na kile wanachokihubiri na kukiimba
 
~~~>>>Hivi huko shule mnaenda kusomea Ujinga maana huo Uandishi wako ni wa hovyo hovyo....

Heo muda unaoutumia kufuata mambo ya Flora ungeutumia kujifunza namna ya kuandika ..


Kama unaona Flora amekosea hebu olewa wewe. . Watanzania tutaacha lini tabia ya kufuata fuata mambo yasiyo kuhusu ..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…