Miaka nenda tumeshuhudia nchi za africa zisivyoweza ku manage rasilimali zake na nchi zikiwa kubwa sana na zenye rasilimali nyingi kwa mfano DRC Congo na Sudan zinakua unstable sana na zile rasilimali zinageuka kuwa laana badala ya baraka, nchi haiendelei ni vita tu miaka nenda miaka rudi.
Tukirudi kwenye nchi yetu hii wenyewe tunashuhudia maendeleo, miradi mingi ya maendeleo na mipango ijayo ya maendeleo ni kwa Dar es Salaam kwa asilimia kubwa.
Yapo maeneo mengi kigoma, mtwara na ruvuma huko barabara zake hazipitiki kabisa kipindi cha mvua kwa kua hakuna barabara za lami, lakini ukija dar kuna barabara zimejengwa na kwa pesa nyingi sana kama hii ya mabasi ya mwendo kasi, lakini haijatumika hadi leo miaka 4, na sijui zitatumika lini na hata zikitumika zitaleta ufanisi na tija gani.
Bila kusahau kuna flyover zinazopigiwa hesabu kujengwa wakati kuna wilaya nyingi Tanzania hazina hata kilomita moja ya lami.
Dar kuna magari mengi sana kiasi kwamba kuendesha gari kwa km 1 unaweza tumia zaidi ya nusu saa, wakati kuna baadhi ya wilaya nzima gari lililnalopita ni la mkuu wa wilaya tu,.
Mgawanyo wa watu, maendeleo na fursa za kiuchumi kuna gap kubwa sana.
sasa nikawaza hivi tukigawa hii nchi tutaleta unafuu kwenye hili au vip?
fikiria nchi kama Rwanda ambayo inafanana kwa vitu vingi sana na mkoa wa kigoma, kwa eneo, watu, hali ya hewa na vitega uchumi, lakini maendeleo yake hayakaribiani hata kidogo.
Nchi inapokua na eneo dogo kusimamia rasilimali zake na kugawana keki ya taifa, inakua ni rahisi hasa kwa sisi waafrica ambao tuna matatizo ya kusimamia rasilimali zetu, rushwa, ukabila na udini.
Nchi ndogo pia zinakua stable na mshikamano zaidi kuliko nchi kubwa, hata wakipata msaada kutoka nje ukitolewa utanufaisha zaidi kwa kua watu ni wachache na kupiga panga inakua sio rahisi.
Kugawa nchi inaonekana ni mpango ambao hauwezekani, pengine hata kutoa hili wazo naonekana mchochezi,lakini hakuna mfumo wa utawala ambao tunaweza kuuweka kila mkoa ukawa unapata share nzuri zaidi ya maendeleo kuliko sasa?