kamati ya ufundi
JF-Expert Member
- Sep 30, 2014
- 416
- 439
*MTATIRO, CHADEMA, TATIZO LA CUF SIO MUTUNGI, TATIZO NI KATIBA YA CUF*
Kushambulia mtu ni jambo rahisi Sana kuliko kuelezea ukweli wa mambo.
Ukiwasoma vijana wa CHADEMA, wanavyolalama juu ya sakata la CUF na msimamo wa jaji mutungi kama msajili wa vyama vya siasa nchini,
Ukamsoma Julius Mtatiro anavyolalama kuhusiana na jambo hilo hilo,
Ukapata nafasi ya kupitia maandiko ya wafuasi wa karibu wa maalim seif juu ya suala hilo hilo.
Utagundua jambo moja muhimu kubwa.
Jambo hilo ni kutokuelewa wapi walipojikwaa,
Maalim Seif na timu yake wamejikwaa, wanajua walipojikwaa lakini ama wanajitia upofu au wanajitia uchizi kutokuelewa walipojikwalia ili wainuke wasonge mbele.
WAMEJIKWAA WAPI? .
maalim Seif na wenzake wamejikwaa kwenye katiba ya Chama Chao, katiba yao wenyewe walioitunga na kuisimamia Sasa wamejikwaa nayo na imewaangusha mpaka chini wanampa kazi Jaji Mutungi.
Ukiwasikiliza Kina Mtatiro wanaishia kusema *"alijiuzulu mwenyewe, Sasa kwanini anataka kurudi ".*
au wanasema *"Alituacha kwenye mapambano vitani akatukimbia sasa anarudi kufata nini?".*
Wanaongeza kusema *"Msaliti huyu anatumiwa na CCM na serikali kutupoteza kwenye msingi wetu"..*
Ama wanasema *" Tulimuomba Sana alijiuzulu mpaka mashehe tukawatuma kwake, lakini alikataa akajiuzulu, sasa Leo anataka nini tena CUF? ".*
Hayo ndio maneno na msingi wa malalamiko yao.
Hawajawahi kusema popote kwamba Katiba ya Chama Chao inasemaje kiongozi anapotaka kujiuzulu? .
Hawasemi kwamba katiba ya CUF inamtaka kiongozi mkuu aliyechaguliwa na mkutano mkuu kabla hajakubaliwa kujiuzulu kwake basi mkutano mkuu uliomchagua ukutane kuidhinisha ama kukataa jambo hilo,
Hawazungumzi ukweli, Hawasemi kwamba Maalim Seif na wenzake wamezidiwa maarifa padogo tu na lipumba, pale alipoamua kung'ang'ania kutumia Katiba ya Chama chao,
Kwa hali ilivyotokea Maalim Seif kama katibu mkuu angeweza kuitisha mkutano mkuu wa CUF mapema Sana Mara tu baada ya Lipumba kujiuzulu mwezi wa nane mwaka 2015 na mkutano ule ungeridhia bila ya shida yoyote kumtimua Lipumba hasa kutokana na hali ilivyokuwa ya kisiasa nchini.
Maalim Seif na wenzake hawakutaka kufuata katiba yao, wameruhusu Kwa kusubili Lipumba kaji mobilize kajirudisha kwenye Chama ndio wameshtuka wakaitisha mkutano mkuu kumjadili Lipumba ( Mwaka mmoja baadae, hii wazungu wanaiita Too late )
Yaliyotokea kwenye mkutano yakawa mambo ya aibu Kwa seif, maana ilionyesha dhahiri kwamba Lipumba alikuwa amejiandaa na kujidhatiti kurudi kwenye Chama.
MUTUNGI ANAINGIAJE? .
Mutungi hajajipeleka kutoa maelekezo juu ya mgogoro wa CUF,
Mutungi amepokea malalamiko kutoka Kwa Wana Chama zaidi ya 300 wa CUF yeye akiwa kama mlezi na msajili wa vyama vyote vya siasa hapa nchini,
Akapokea tena na malalamiko ya Lipumba juu ya dhamira yake ya kutaka kurejea kwenye Chama chake Kwa mujibu wa katiba yao.
Mutungi kama msajili akaziita pande zote, upande wa Maalim Seif na Upande wa Lipumba, akajadiliana nao , kila upande ukatoa hoja zao, kwa mazungumzo na kwa maandishi.
Mwisho Mutungi akatoa ushauri kwa mujibu wa katiba ya CUF.
KESI MAHAKAMANI
Kitendo cha Wakina Maalim Seif kwenda mahakamani ni kithibitisho kuwa uamuzi uliotolewa na MUTUNGI ni halali kisheria kwa mujibu wa sheria na kanuni zinazoongoza usajili na uendeshaji wa vyama vya siasa,
Ndio maana kina Mtatiro wakaenda kukata rufaa mahakamani, maana yake wanaitaka mahakama itengue uamuzi wa msajili wa vyama vya siasa kutokana na hoja walizozitoa ambazo pengine wanaamini zitawasaidia.
Kwa watu wenye hekima na wanaoheshimu utawala wa sheria hii ilikuwa ni hatua muhimu kabisa ya kudai haki.
Lakini kukesha mitandaoni na kwenye magazeti kumtukana msajili wa vyama vya siasa ni UZUZU usio kuwa na kifani,
Kusema tatizo lote la CUF ni msajili ni kumuonea, tatizo la CUF ni wao wenyewe kutokuheshimu na kuifuata katiba yao walioindika wenyewe.
Kama ambavyo akina maalim seif walikuwa na Imani na msajili wa vyama vya siasa na kuitikia wito kujibu malalamiko ya wanachama na msimamo wa Lipumba,
Ndivyo hivyo wanapaswa kumuheshimu na kuyaheshimu maamuzi yake mpaka hapo baadae kama mahakama itaamua vinginevyo.
Nina hakina na ni dhahiri kwamba hata kama maamuzi ya Mutungi yangekuwa upande wa maalim seif basi upande wa lipumba nao ungelalama hivi hivi.
Kuendelea kumtukana Mutungi na kumuhusisha kuihujumu CUF hakuondoi sintofahamu iliyopo ndani ya Chama hicho kikongwe.
Dalili zinaonyesha kwamba hivi sasa pande zote mbili zinavutana zikiwa na mahusiano ya nje ya Chama chao.
Naomba niishie hapa kwa sasa. Namaliza kwa kusema kuwa Kina Mtatiro kumtukana jaji Mutungi sio Dawa, Dawa ni kuitukana katiba yao iliyowafikisha hapo.