Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amepata dhamana na yuko huru. Kila mtu alitaka Lema atendewe haki. Lakini nimesikitishwa na kitendo cha Polisi wa Arusha kuwapiga na kuwaumiza wananchi wasiokuwa na hatia ati kwa sababu wamekwenda mahakamani kwenye kesi ya Lema. Leo kwenda mahakamani ni dhambi? Kwenda mahakamani ni laana? Jana nilimsikia Rais anahubiri amani na utulivu huko Lindi? Leo Polisi wake wanatia raia ulemavu na maumivu yasiyoelezeka. Hivi anayeharibu amani ya nchi hii ni raia waliokwenda mahakamani kwa amani au ni wanasiasa wanaotuma vyombo vya dola vipige na kuumiza raia bila sababu? Nchi hii ina mambo yanaudhi na kuumiza sana lakini mambo hayo ndiyo yanawakomaza wananchi, maana ili mbegu iote, huoza kwanza.
[HASHTAG]#JSM[/HASHTAG].
Tunisia?Hakuna taasisi ya ulinzi ya ovyo kama Polisi wa Tunisia
CDM jifunzeni kutii sheria kwa hiyari, mpaka mpaka mpigwe virungu ndo mnaelewa ?!Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amepata dhamana na yuko huru. Kila mtu alitaka Lema atendewe haki. Lakini nimesikitishwa na kitendo cha Polisi wa Arusha kuwapiga na kuwaumiza wananchi wasiokuwa na hatia ati kwa sababu wamekwenda mahakamani kwenye kesi ya Lema. Leo kwenda mahakamani ni dhambi? Kwenda mahakamani ni laana? Jana nilimsikia Rais anahubiri amani na utulivu huko Lindi? Leo Polisi wake wanatia raia ulemavu na maumivu yasiyoelezeka. Hivi anayeharibu amani ya nchi hii ni raia waliokwenda mahakamani kwa amani au ni wanasiasa wanaotuma vyombo vya dola vipige na kuumiza raia bila sababu? Nchi hii ina mambo yanaudhi na kuumiza sana lakini mambo hayo ndiyo yanawakomaza wananchi, maana ili mbegu iote, huoza kwanza.
[HASHTAG]#JSM[/HASHTAG].
Glory Siah Rimoy kutoka Arusha anaripoti kuwa Polisi mkoani humo wamepiga wananchi waliokusanyika eneo la mahakama kuu kusikiliza kesi ya Mhe.Lema. Baadhi ya wananchi wamejeruhiwa vibaya kwa virungu na wengine wamekamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi kati na kuswekwa rumande bila kosa lolote. Watu wanne wamekimbizwa hospitali ya rufaa Mt.Meru kufuatia kipigo kikali cha polisi, kilichosababisha majeraha na wengine kupoteza fahamu. Magari ya kuwasha, police wenye silaha nzito wamezingira eneo lote la mahakama. Watu wamezuiwa kuingia, na maeneo ya nje ya mahakama ni virungu na kipigo kikali kwa raia.