Mtangazaji wa Global TV anusurika kula kichapo

chiefnyumbanitu

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
906
426
Katika tukio la jana kunyesha mvua kubwa Jijini Dar mpaka kutokea mafuriko na mwananchi mmoja kupoteza maisha kutokana na hayo mafuriko, mtangazaji wa Global TV alienda pale na kuanza kuhoji mashuhuda.

Shuhuda moja baada ya kutaka kuhojiwa alifoka na kumwambia mtangazaji, "sipendi kuhojiwa ntakupiga vitasa". Mtangazaji akaondoka kwa aibu na kusogea sehemu nyingne.

Nimeamini kazi ya utangazaji ina ugumu wake.
 
Angempiga ndo angeona nini kingemtokea...kwani ukisema sitaki tu hutaeleweka?
 
Hao vijana wa Shigongo wanastahili vitasa,wamedhalilisha watu wengi sana kupitia the so called OFM.

Huyo jamaa atakuwa majeruhi wa OFM tu bado ana-hangover ya hasira.
 
Huyo aliyekataa kuhojiwa ujue mfukoni ana bangi au kiroba.
 
Kelvin ni mtangazaji anayechipukia, kwanza hawezi kupigana na mtu sababu ni mpole, mstaarabu hata mwili wake sio wa kibabe. Huyo jamaa alitaka kumuonea mtoto wa watu. Anakupa nafasi ya kujieleza, ukishindwa basi wala hakulazimishi hata ukimtukana yeye anacheka tu. Ndo maana uliona anaaondoka na kuendelea kuhoji watu wengine.

Namkubali sana dogo.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…